Ninajibu hiyo bolded kama ulivyouliza. Mimi naelewa ngono zembe kuwa ni ile inayoweza kusababisha mimba na/au magonjwa ya zinaa. Na ninaelewa kuwa mtu akitumia kondomu kwa usahihi na kwa kila tendo la ngono, basi hiyo ni ngono salama (kinyume cha ngono zembe). Nimekuwa nikifanya hivyo katika ngono zote nilizoshiriki, isipokuwa moja tu niliyokuwa nikifanyishwa nikiwa mtoto wa miaka 10 (18 years ago) ndiyo niliyokwenda kavu, na ndipo nilipojifunzia ngono.
Kwa uelewa wangu VVU vinaingia kwa urahisi kwenye via vya uzazi, na hasa kama kuna michubuko. Sijawahi kupata mchubuko huo maana siku zote nakuwa nimevaa kondomu.
Siwezi kumwomba msamaha huyo dada maana kufanya hivyo ni sawa na self-implication kwa kosa lisilokuwa langu. Hakuna baina yetu mwenye uhakika kama kabla hatujakutana nae alikuwa nayo hiyo HIV au la. Siko tayari kujinyanyapaa kwa kitu kisicho na ushahidi.
Kuhusu kumsifu huyo uliyesema, niwie radhi mshikaji maana mie na hizo dini za kukopa kwa watu wa middle east tuko mbalimbali. Wanaohusika nae watamsifu tu hamna noma.