ex-girlfriend anataka nizae nae

hili limekuwa tatizo kwa mabinti na wanaume wengi, baada ya kukata mahusiano hujikuta wakitakakuyarudia, sasa kama ulishafanya maamuzi ya kuoa kwa nini unaendelea kumuintatain huyo ex? mwambie ukweli, vinginevyo na wewe utakuwa na sitaki nataka.
 

Unakaribia kufanya kosa kubwa sana katika maisha yako! Do you think you are that special? Achana nae kibaraka wa ibirisi huyo.
 
Jamani mimi nina wasiwasi na huyo exgf wako shida yake sio kuzaa na wewe tuu shida yake ni kumkomoa mkeo
 
jamani wana jf kuna mambo kuomba msaada jamani....sio kitu kama hiki ambacho kiko streit fowadi.....huyu haheshimu ndoa yake.....

hili swala linahusu maisha yako na wewe na familia yako halafu unaona kabisa tayari umeshaoa na una mke halafu unakuja hapa kuuliza kitu ambacho wewe mwenyewe ni injinia wake....na pengine umetembea nae huyo dada baada ya kuwa umeoa na huku ukimwambia kuwa ....oooo darl unajua nilioa kwa bahati mbaya..mhmhh yaani wewe ndio uko moyoni...na sasa anataka mtoto then unaanza kutoa macho.... na kutuuliza sisi huku?!!!...cha kufanya nenda nyumbani kwako mwambie mkeo hii habari then chukua ushauri wake full stop.....
 
Unakaribia kufanya kosa kubwa sana katika maisha yako! Do you think you are that special? Achana nae kibaraka wa ibirisi huyo.

huyu mleta mada ndo ana makosa.........yule dada hana tatizo....huyu jamaa hajachukua hatua madhubuti isipokuwa anabembeleza urafiki...ni unafiki mkubwa sana........so ibirisi ni huyu..

mapenzi siku zote ni kujifunza...amtose huyo dada then akae mwaka mmoja kama hajasikia kazaa ma mtu mwingine na hapo atalnganisha na kauli ya huyo dada kuwa hana thamana kama asipozaa nae.....we should think beyond the next meal!!!
 
Kwani bado mnachakachuana mpaka afikie kukwambia kuwa anataka azae nawewe? kama hamchakachuani Jaribu upunguze ukaribu naye kwani wewe una mke hm sasa.
 
nashukuru kwa ushauri ila ingekuwa ni suala kutaka nisingepata wakati mgumu wa kuamua
 
simchakachui boss wangu ila tuna ukaribu wa mawasiliano tu
 
thx kwa ushauri lakini hilo la kumshirikisha my wife itakuwa ni dharau kubwa sana kwake. na ndio maana nimeiweka hapa kupitia ushauri wenu nifikie uamuzi ambao utakuwa mzuri kwangu na familia yangu
 
nashukuru sana kwa ushauri wako wenye kujenga mkuu. issue yakunishirikisha mambo yake ananishirikisha na pia huwa namshirkisha wife wangu maana wanafahamiana so if the is any family she tends to inform us and viceversa
 
Mwambie haiwezekani!!Kama ambavyo yeye hakutaka kuharibiwa maisha yake huko nyuma ndivyo atakavyokuharibia ya kwako sasa hivi au mbeleni!!Kua mwanaume!!!:embarassed2:
mara nyingine maji huzidi unga but all in all nashukuru kwa ushauri wako ambao ni very constructive
 
wewe ni mtu mzima, hivi kweli ni sawa kuzaa nje ya ndoa? hivi mkeo naye akiamua kuomba ushauri kama wakwako utajisikiaje? mimi nijuavyo mtu anayeheshimu familia yake asingeomba ushauri kwa jambo kama hili,kwanza ni aibu
 
Bwana wewe umeona una mtoto sijui watoto, unataka ushauri hapa tena wa kutoka nje ya ndoa yako???

Pole sana tulia na wako kaka mambo yenyewe siku hizi mambo si mambo
 

Hapo huna ujanja inabidi uzae nae tu:confused3:!
 
Tuna masuala mengi muhimu ya kushauri hili lipo ndani ya uwezo wako. Kwa ufupi mpe msimamo wako kuwa kwa sasa hana nafasi na huna mpango wa kuzaa nje ya ndoa.

Jamaa anaonekana ana Mpango hu lakini na kwa maelezo yake ni tosha kusema kuwa jamaa ana mchakachua huyo ex-wake
 
usizae nae utaiingiza familia yako kwenye matatizo bure ipende na ijali familia yako
akatafute mtu mwingine
 
labda mimi sijakuelewa vizuri, wewe tayari umeoa na familia yako sasa unavyoendeleza communication na exgirlfriend maana yake nini? wewe kaa kimya uone kama hata loose interest na wewe, hivyo unavyozidi kumpa sikio basi anajua kuwa you are still attracted na yeye na ndio likaja suala la nipe mimba. kama kweli hutaki, basi kaa mbali naye, acha contact naye. naye atapata ujumbe na kusonga mbele mbele kutafuta njemba mwingine wa kuzaa naye
 
Dah, lakini mi naona na wewe unampenda sijui, unapenda kuzaa naye.
Dah, hebu msaidie basi, manake najua kabisa hicho anachokifikiria hakita kuja kumpa furaha mbele ya safari.

Anachowaza huyu dada, nadhani anajutia kukukosa tu, lkn mwambie kuna mzuri zaidi yako atatokea na atamfanya ayaone
maisha ni mazuri tu.

Mi nawaza hivyo, msaidie, ajitambue.
 
Uliheshim uamzi wake ukamwacha akaenda kusoma, Sasa kamaliza mambo yake eti anarud tena! Huo ni ubinafs wa hali ya juu, kataa pendekezo lake kwa nguvu zako zote na kwa moyo wako wote na kwa akili yako yote. Hata kuchakachua kwa condom kuepuke maana anaweza kuihujum huku akiwa amekulengesha kwny cku za rutuba ili atimize lengo lake, in short heshim ndoa yako vivyo hivyo naye muhimize aieshim.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…