Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mimi ni baba wa familia(nimeoa) kabla ya kuoa nilikuwa na rafiki yangu wa kike ambae nilidumu nae kwa miaka mitatu hivi. nilipokuwa tayari kuoa nilimtaarifu mwenzangu kuwa nataka kujitokeza kwao aliniambia kuwa kwa wakati huo hayupo tayari kuolewa kwa sababu bado hajajiandaa na wazazi wake hawawezi kukubali na pia alikuwa na plan ya kuendelea kusoma. kwa sababu nilikuwa nimeweka malengo yangu kuwa ikifika age fulani nioe nilichukua uamuzi wa kutafuta mtu mwingine aliyetayari kuolewa na mungu si athumani nikampata. baada ya kumpata nilitumia busara yangu kumjulisha kuwa nimeamua kutafuta mwingine aliye tayari kuolewa na nimeshampata so no need kuendelea kuwa na mahusiano nae, alikubali ingawaje kwa shingo upande na kwa kulia sana baada ya hapo tuliendelea kuwasiliana kama marafiki wa kawaida kwa sababu hatukugombana. sasa ni miaka mitatu imeshapita ametokea kuwa karibu tofauti na ilivyo kawaida na pia amekuwa akilalamika kila siku kuwa boyfriend wake hamkidhi mahitaji yake(sex) nimekuwa nikimshauri awe mvumilivu na ampeleke kwa washauri wa mahusiano lakini kali ni last week alipoanza kuniambia live kuwa hatokuwa na maana yoyote kama hatozaa nami maana ni mwanaume pekee ambaye nimebaki na nafasi katika moyo wake so anachoomba yeye si kurudiana bali niweze kuzaa naye ili iweze kuwa kumbu kumbu yake for rest of her life, kwangu imekuwa ni mtihani sana kwa sababu ya urafiki wetu hata baada ya mimi kuoa. ushauri wenu wanajf
Unakaribia kufanya kosa kubwa sana katika maisha yako! Do you think you are that special? Achana nae kibaraka wa ibirisi huyo.
nashukuru sana kwa ushauri wako wenye kujenga mkuu. issue yakunishirikisha mambo yake ananishirikisha na pia huwa namshirkisha wife wangu maana wanafahamiana so if the is any family she tends to inform us and viceversamkuu,
Heshimu ndoa yako! Na kama ni mkristo inabidi ujitahidi umsahau huyo dada, na ningekushauri upunguze ukaribu naye kwa kadiri inavyowezekana.
Kwa maelezo yako inaonesha bado mpo karibu kimawasiliano. Ningependa nikushauri umwache huru ajiamulie mambo yake mwenyewe. Akutafute kama ana shida za kibinadamu za kawaida, tena akushirikishe mbele ya mkeo.
Inawezekana kweli ulimpenda, ni kweli, lakini mwangalie pia mkeo. maana akifahamu utamweka katika mazingira magumu na kuhatarisha ndoa yako nzuri.
nimekusoma mkuu thxUmeoa kaka tulia na wako usihangaike utadhurika bure
mara nyingine maji huzidi unga but all in all nashukuru kwa ushauri wako ambao ni very constructiveMwambie haiwezekani!!Kama ambavyo yeye hakutaka kuharibiwa maisha yake huko nyuma ndivyo atakavyokuharibia ya kwako sasa hivi au mbeleni!!Kua mwanaume!!!:embarassed2:
..... ni last week alipoanza kuniambia live kuwa hatokuwa na maana yoyote kama hatozaa nami maana ni mwanaume pekee ambaye nimebaki na nafasi katika moyo wake so anachoomba yeye si kurudiana bali niweze kuzaa naye ili iweze kuwa kumbu kumbu yake for rest of her life, kwangu imekuwa ni mtihani sana kwa sababu ya urafiki wetu hata baada ya mimi kuoa. ushauri wenu wanajf
Tuna masuala mengi muhimu ya kushauri hili lipo ndani ya uwezo wako. Kwa ufupi mpe msimamo wako kuwa kwa sasa hana nafasi na huna mpango wa kuzaa nje ya ndoa.