Ex wangu na mwanamke wake wananisumbua

Ex wangu na mwanamke wake wananisumbua

Nipo na makasiriko pamoja na huzuni.. daah nyie wanaume mtakuja kutuua wanawake

Basi bwana nina huyo ex wangu king’ang’anizi yaani hataki kuachana na Mimi iwe jua ama mvua…

Kuna mwanamke anaishi nae ana ujauzito nahisi miezi 7 or 8 hiko ndio kitu kilichofanya nisitake kurudiana nae

Sasa mimi nimeamua ku move on na maisha yangu, akinipigia simu sipokei wala sijibu sms zake huu ni mwezi wa 2 Ila yeye kila siku kunitafuta hachoki yaani Kama chakula, Asubuhi mchana jioni

Jana nikashanga namba ngeni ila ina picha ya huyo ex wangu dp.. nikajua ni yeye nikaona nimjibu maana mpk anatumia namba ngeni labda kuna jambo la muhimu… huwezi amini hilo ndio kosa nimejutia kufanya mpk najisikia vibaya

Ile namba ni namba ya huyo dada wanaeishi pamoja sijui kakuta sms za zamani na miamala ya pesa nikitumiwa mimi ugomvi ukaanzia hapo akawa anajibamiza et atoe mimba mara anataka kujiua( Hii nimepewa na wifi yaani dada ake ex wangu) kwaiyo dada ndio akaamua kunitafuta

Kusema ukweli nilikwaZika nikaona Kama wananisumbua yeye na mpenzi wake maana alikuwa ananitambia ooh sijui nini nikajisikia vibaya na Mimi nikaanza kumwambia habari za uongo kusema ukweli tumetukanana sana

Hapa sasa najisikia vibaya kwa niliyoyafanya nimejisikia huruma ila pia najisikia kuumia moyo wangu sina raha

Sikuwai kuwaza Kama nitakuja kugombania mwanaume na kuzozana na mwanamke mwenzangu kisa mwanaume

Ex wangu nampenda ila sina namna ya kuwa nae

Wote tuna Miaka 24 kuanzia mwanaume mimi na huyo mwanamke wake

Nimechoka kujielezea
mpe nafasi mwanaume mwingine achana na mume wa mtu
 
Ndio nimeamka najutia kupoteza muda wangu kutukanana na wapumbavu
 
Haya bana, hili nalo ni la kuomba ushauri?

Mtumie text hii.

"Badilika muda haumsubiri mtu, tulia na mama watoto mtarajiwa. Sina muda na upumbavu wetu wa zamani. Kama umeamua kubakia katika huo upumbavu baki mwenyewe"

Tatizo baada ya muda mfupi utamuomba muamala ingawa unatuambia ume move on
 
tumblr_bd82b25e76b6ffe1737db8ef3b7d7fd0_7d7c4ec6_500.gif
 
Hayo yoote ili nikuone nikitongoze
 
Nipo na makasiriko pamoja na huzuni.. daah nyie wanaume mtakuja kutuua wanawake

Basi bwana nina huyo ex wangu king’ang’anizi yaani hataki kuachana na Mimi iwe jua ama mvua…

Kuna mwanamke anaishi nae ana ujauzito nahisi miezi 7 or 8 hiko ndio kitu kilichofanya nisitake kurudiana nae

Sasa mimi nimeamua ku move on na maisha yangu, akinipigia simu sipokei wala sijibu sms zake huu ni mwezi wa 2 Ila yeye kila siku kunitafuta hachoki yaani Kama chakula, Asubuhi mchana jioni

Jana nikashanga namba ngeni ila ina picha ya huyo ex wangu dp.. nikajua ni yeye nikaona nimjibu maana mpk anatumia namba ngeni labda kuna jambo la muhimu… huwezi amini hilo ndio kosa nimejutia kufanya mpk najisikia vibaya

Ile namba ni namba ya huyo dada wanaeishi pamoja sijui kakuta sms za zamani na miamala ya pesa nikitumiwa mimi ugomvi ukaanzia hapo akawa anajibamiza et atoe mimba mara anataka kujiua( Hii nimepewa na wifi yaani dada ake ex wangu) kwaiyo dada ndio akaamua kunitafuta

Kusema ukweli nilikwaZika nikaona Kama wananisumbua yeye na mpenzi wake maana alikuwa ananitambia ooh sijui nini nikajisikia vibaya na Mimi nikaanza kumwambia habari za uongo kusema ukweli tumetukanana sana

Hapa sasa najisikia vibaya kwa niliyoyafanya nimejisikia huruma ila pia najisikia kuumia moyo wangu sina raha

Sikuwai kuwaza Kama nitakuja kugombania mwanaume na kuzozana na mwanamke mwenzangu kisa mwanaume

Ex wangu nampenda ila sina namna ya kuwa nae

Wote tuna Miaka 24 kuanzia mwanaume mimi na huyo mwanamke wake

Nimechoka kujielezea
Hii stori ilishawaig kuletwa hapa jf, hii ni marudio, umefanya marudio kma movie za azam wanavozirudia rudia
 
sijui kakuta sms za zamani na miamala ya pesa nikitumiwa mimi 😆😆

Ex wangu nampenda ila sina namna ya kuwa nae😄😄
 
Back
Top Bottom