Nimerudii tena mimi kadogo2 safari hii nina majonzi
Kuna story nilishaitoaga hapa kuhusu kumuacha Ex wangu kwa mambo Fulani fulani.. sasa bhn sababu kubwa niwe mkweli huyu ex wangu alikuwa anashauku sana ya kuwa na mtoto yaani hii ndio sababu ilifanya nikamuacha
Mimi na ex wangu Kama hajanidanganya Miaka yake basi tupo Sawa 25 kanizidi miezi michache tu yaani wote tuna Miaka 25
Kipindi tunakutana tulikuwa na Miaka 23 alitaka nimzalie ila sikufanya hivyo.. ugomvi ulipotokea tukaachana Kama mwaka hivi ila ndani ya huo mwaka tunatafutana tunarudiana tunaachana tenaa
Sasa mahusiano yalirudi rasmi kuanzia mwezi wa 3 mwaka huu tena yeye akilazimisha zaidii turudiane nikaona Hakuna tatizo maana mimi pia nilikuwa single
Kilichonileta hapa ex wangu nimegundua kuwa anaishi na mwanamke mwinginee tena huyo mwanamke ana ujauzito wake.. niligundua kupitia ndugu yake maana huwa nawasiliana nae nikaomba anichunguzie maana kuna vitu niliona sivielewi.. maana yeye kapanga mkoa X na anafanyia kazi mkoa mwinginee.. nilimuulizaga kwake anakaa nani akawa hana majibu ya kueleweka ikabidi nimuulize ndugu yake ndio kuniambia kuwa kuna mdada anamuonaona pale inasemekana wanaishi wote ila hakuniambia suala la kuwa mjamzito hilo niliambiwa na muhusika mwenyewe
Sasa ex wangu katika kuongeaongea akaanza kunilaumu kwanini nilimuacha mwaka mzima.. ikabidi nimuulize kama kuna mtu yupo nae.. akaniambia kweli anae mtu na hawezi kumuacha kwasababu ana mtoto wake tumboni..
Imebidi nishangae ndani ya mwaka mtu katafuta mwanamke na kampachika ujauzito alikuwa na haraka gani ya kufanya hivyo.. kumbuka ndani ya huo mwaka sio kwamba tuliachana moja kwa moja tulikuwa tunawasiliana sana na tunarudiana tunagombana tena tunapumzishana
Namuuliza kwanini umefanya hivyo anasema kwamba mimi nilimnyima mtoto na yeye hajui atakufa lini Akifa ghafla nani atarithi mali zake⦠kusema ukweli hili jambo limeniumiza sana sanaa sijaumia yeye kuwa na mtu kilichoniuma ni yeye kumpa na mimba juu huyo mdada⦠kusema ule ukweli mimi tangu niachane nae niliamua kutulia tu sikuhitaji mwanaume⦠maana nilijipa muda wa kutuliza akili ila sikutegemea mwenzangu amemoveon kiasi hiki
Nimemuuliza kuhusu mimi na yeye uhusiano wetu unakuaje anasema mimi ananipenda na hataki kuniacha ila yule mwanamke ana mtoto wake hivyo hawezi kumuacha pia.. kiufupi ni kuwa anatutaka wote
Mimi huyu mwanaume nina mpenda ila sasa nitakuaje nae na tayari kuna mwanamke ana mimba yake na mbaya zaidi kamuweka kwake Halafu anataka na mimi anipangie sehemu nyingine
Daah hata Kama ni malipo ila haya ni too much.. kwani mimi nilifanya makosa gani Miaka 23 kweli anataka tuzae hata ingekuwa ni wewe ungenishauri nimuache
Naombeni ushauri wowote tu nifanye nini juu ya hili jambo
Navoandika hapa ananitumia sms kila saa na nimeshamwambia sitaki anitafute ila bado hakomi huyu anataka nini kwangu jmn [emoji24][emoji24]