Ex wangu nampenda ila kampa mimba mwanamke mwingine

Nimerudii tena mimi kadogo2 safari hii nina majonzi

Kuna story nilishaitoaga hapa kuhusu kumuacha Ex wangu kwa mambo Fulani fulani.. sasa bhn sababu kubwa niwe mkweli huyu ex wangu alikuwa anashauku sana ya kuwa na mtoto yaani hii ndio sababu ilifanya nikamuacha

Mimi na ex wangu Kama hajanidanganya Miaka yake basi tupo Sawa 25 kanizidi miezi michache tu yaani wote tuna Miaka 25

Kipindi tunakutana tulikuwa na Miaka 23 alitaka nimzalie ila sikufanya hivyo.. ugomvi ulipotokea tukaachana Kama mwaka hivi ila ndani ya huo mwaka tunatafutana tunarudiana tunaachana tenaa

Sasa mahusiano yalirudi rasmi kuanzia mwezi wa 3 mwaka huu tena yeye akilazimisha zaidii turudiane nikaona Hakuna tatizo maana mimi pia nilikuwa single

Kilichonileta hapa ex wangu nimegundua kuwa anaishi na mwanamke mwinginee tena huyo mwanamke ana ujauzito wake.. niligundua kupitia ndugu yake maana huwa nawasiliana nae nikaomba anichunguzie maana kuna vitu niliona sivielewi.. maana yeye kapanga mkoa X na anafanyia kazi mkoa mwinginee.. nilimuulizaga kwake anakaa nani akawa hana majibu ya kueleweka ikabidi nimuulize ndugu yake ndio kuniambia kuwa kuna mdada anamuonaona pale inasemekana wanaishi wote ila hakuniambia suala la kuwa mjamzito hilo niliambiwa na muhusika mwenyewe

Sasa ex wangu katika kuongeaongea akaanza kunilaumu kwanini nilimuacha mwaka mzima.. ikabidi nimuulize kama kuna mtu yupo nae.. akaniambia kweli anae mtu na hawezi kumuacha kwasababu ana mtoto wake tumboni..

Imebidi nishangae ndani ya mwaka mtu katafuta mwanamke na kampachika ujauzito alikuwa na haraka gani ya kufanya hivyo.. kumbuka ndani ya huo mwaka sio kwamba tuliachana moja kwa moja tulikuwa tunawasiliana sana na tunarudiana tunagombana tena tunapumzishana

Namuuliza kwanini umefanya hivyo anasema kwamba mimi nilimnyima mtoto na yeye hajui atakufa lini Akifa ghafla nani atarithi mali zake… kusema ukweli hili jambo limeniumiza sana sanaa sijaumia yeye kuwa na mtu kilichoniuma ni yeye kumpa na mimba juu huyo mdada… kusema ule ukweli mimi tangu niachane nae niliamua kutulia tu sikuhitaji mwanaume… maana nilijipa muda wa kutuliza akili ila sikutegemea mwenzangu amemoveon kiasi hiki

Nimemuuliza kuhusu mimi na yeye uhusiano wetu unakuaje anasema mimi ananipenda na hataki kuniacha ila yule mwanamke ana mtoto wake hivyo hawezi kumuacha pia.. kiufupi ni kuwa anatutaka wote

Mimi huyu mwanaume nina mpenda ila sasa nitakuaje nae na tayari kuna mwanamke ana mimba yake na mbaya zaidi kamuweka kwake Halafu anataka na mimi anipangie sehemu nyingine

Daah hata Kama ni malipo ila haya ni too much.. kwani mimi nilifanya makosa gani Miaka 23 kweli anataka tuzae hata ingekuwa ni wewe ungenishauri nimuache

Naombeni ushauri wowote tu nifanye nini juu ya hili jambo
Navoandika hapa ananitumia sms kila saa na nimeshamwambia sitaki anitafute ila bado hakomi huyu anataka nini kwangu jmn [emoji24][emoji24]
Na umeshamuita ni "X"! Sasa unataka nini tena?Au x ina maana gani?
 
Watu wanataka watoto wewe unadengua wakati wanawake wengi wapo tayari, ata ungekuwa unahitaji mtoto alafu mwenza wako hataki ungefanya nini maana yeye kioaumbele chake awe na mtoto.
 
Sawa sasa wote tulikuwa na Miaka 23 mimi sina kazi japo yeye alikuwa nayo… kweli ningemzaliaje hapo..

Na mpango wa kuoa bado hata sasa bado hawezi kunioa kwasababu ya mambo fulani fulani kazini kwake

Nimeogopa kuwa single maza
Mambo flani flani kazini kwake, kwani ni mwanajeshi hajamaliza mkataba?

Halafu thread yako yote hii haujasema ulitaka nini katika mahusiano yenu hadi akakuona wewe ni mpuuzi akatafuta mwanamke mwingine?

Kuzaa unasema bado wewe mdogo, mwenzako alikuweka wazi kuwa umri wa kuzaa tayari na anataka mzae, wewe hukutaka na haukuweka wazi kwa mwenzako umri ambao ulitaka uanze kuzaa.

Mwenzako alikuona misimamo na malengo yenu haviendani ndiyo maana akatafuta mtu wanayeendana naye.

Kusema anaendelea kukupenda yawezekana anasema ukweli.

Chemistry ya kiume inaruhusu kupenda mwanamke zaidi ya mmoja na maisha yakasonga.

Sasa kuwa mke wake wa pili, maana sifa za kuwa mke wake wa kipekee uliipoteza.

Siwezi kukushauri vinginevyo mama, maana penzi la watu huwa halivunjwi na wapambe bali huvunjwa na wao wenyewe.
 
Kwanza haujieelewi binti, pia haujui unataka nini.
Pili sina cha kukushauri zaidi ya kukusisitiza ufanye kile utakacho ona kinakufaa pasipo kuomba ushauri kwa mtu yeyote.
 
Nimerudii tena mimi kadogo2 safari hii nina majonzi

Kuna story nilishaitoaga hapa kuhusu kumuacha Ex wangu kwa mambo Fulani fulani.. sasa bhn sababu kubwa niwe mkweli huyu ex wangu alikuwa anashauku sana ya kuwa na mtoto yaani hii ndio sababu ilifanya nikamuacha

Mimi na ex wangu Kama hajanidanganya Miaka yake basi tupo Sawa 25 kanizidi miezi michache tu yaani wote tuna Miaka 25

Kipindi tunakutana tulikuwa na Miaka 23 alitaka nimzalie ila sikufanya hivyo.. ugomvi ulipotokea tukaachana Kama mwaka hivi ila ndani ya huo mwaka tunatafutana tunarudiana tunaachana tenaa

Sasa mahusiano yalirudi rasmi kuanzia mwezi wa 3 mwaka huu tena yeye akilazimisha zaidii turudiane nikaona Hakuna tatizo maana mimi pia nilikuwa single

Kilichonileta hapa ex wangu nimegundua kuwa anaishi na mwanamke mwinginee tena huyo mwanamke ana ujauzito wake.. niligundua kupitia ndugu yake maana huwa nawasiliana nae nikaomba anichunguzie maana kuna vitu niliona sivielewi.. maana yeye kapanga mkoa X na anafanyia kazi mkoa mwinginee.. nilimuulizaga kwake anakaa nani akawa hana majibu ya kueleweka ikabidi nimuulize ndugu yake ndio kuniambia kuwa kuna mdada anamuonaona pale inasemekana wanaishi wote ila hakuniambia suala la kuwa mjamzito hilo niliambiwa na muhusika mwenyewe

Sasa ex wangu katika kuongeaongea akaanza kunilaumu kwanini nilimuacha mwaka mzima.. ikabidi nimuulize kama kuna mtu yupo nae.. akaniambia kweli anae mtu na hawezi kumuacha kwasababu ana mtoto wake tumboni..

Imebidi nishangae ndani ya mwaka mtu katafuta mwanamke na kampachika ujauzito alikuwa na haraka gani ya kufanya hivyo.. kumbuka ndani ya huo mwaka sio kwamba tuliachana moja kwa moja tulikuwa tunawasiliana sana na tunarudiana tunagombana tena tunapumzishana

Namuuliza kwanini umefanya hivyo anasema kwamba mimi nilimnyima mtoto na yeye hajui atakufa lini Akifa ghafla nani atarithi mali zake… kusema ukweli hili jambo limeniumiza sana sanaa sijaumia yeye kuwa na mtu kilichoniuma ni yeye kumpa na mimba juu huyo mdada… kusema ule ukweli mimi tangu niachane nae niliamua kutulia tu sikuhitaji mwanaume… maana nilijipa muda wa kutuliza akili ila sikutegemea mwenzangu amemoveon kiasi hiki

Nimemuuliza kuhusu mimi na yeye uhusiano wetu unakuaje anasema mimi ananipenda na hataki kuniacha ila yule mwanamke ana mtoto wake hivyo hawezi kumuacha pia.. kiufupi ni kuwa anatutaka wote

Mimi huyu mwanaume nina mpenda ila sasa nitakuaje nae na tayari kuna mwanamke ana mimba yake na mbaya zaidi kamuweka kwake Halafu anataka na mimi anipangie sehemu nyingine

Daah hata Kama ni malipo ila haya ni too much.. kwani mimi nilifanya makosa gani Miaka 23 kweli anataka tuzae hata ingekuwa ni wewe ungenishauri nimuache

Naombeni ushauri wowote tu nifanye nini juu ya hili jambo
Navoandika hapa ananitumia sms kila saa na nimeshamwambia sitaki anitafute ila bado hakomi huyu anataka nini kwangu jmn [emoji24][emoji24]
Yaani mwanamke miaka 23 unajiona mdogo kuzaa?
Mwanamke umri ukishafika miaka 21 tu ujue soko lako litaporomoka kila uchwao maana hapo unakimbilia kwenye 30's ambapo ni mshangazi tayari.
 
Binafsi nasimama na mtoa mada huwezi kubali kubeba ujauzito wakati hujui hatma yenu ya mahusiano

Mwisho wa siku aje kupondwa hapa kisa single mom kama hujaolewa na matumaini ya kuolewa epuka kuzaa mapema full stop.
 
  • Thanks
Reactions: _ly
Achana naye huyo mwanaume endelea na maisha yako na kama unakubali kuendelea naye kubali uke wenza na kumbuka huyo amekutangulia kumzalia huyo jamaa kwaiyo atakuwa na nguvu hata hapo baadae pengine yeye anaweza onekana ni mke wa kwanza wewe ndio mke wa pili...
 
Huna msimamo unaendeshwa na mihemko umekurupuka kumpa mimba mwanamke mwinginee for the sake of unahitaji mtoto under 27 una presha ya kupata mtoto hivyo
Wamekuwa n mahusiano ya mwaka mzima, mtu ana umri wa 25 na Ana kazi then unasema amekurupuka kumpa mtoto.

"Mwanamke mwengine" minimize this act huyo ni mwanamke wake na si mwanamke mwengine bali mwanamke mwingine ni wewe hapa.

Unafosi maono yako kua maono ya wenzio, yeye anataka mtoto wewe hukutaka amempata aliyekuwa na maono sawa wamezaa why uje kufosi kuingilia maono yao na wewe si utafute asiyehitaji mtoto mwenzio.

Kitu pekee hapa ulikuwa na haki ya kuongea ni kukurudia huku akiwa na mwanamke mwengine sio blaa blame za mwak mmoj, kisasi, kisasi watu mmeacha as if mtu mkiachana bado unamiliki.

Komaa kiakili sio Hisia Hisia
 
Watu wanataka watoto wewe unadengua wakati wanawake wengi wapo tayari, ata ungekuwa unahitaji mtoto alafu mwenza wako hataki ungefanya nini maana yeye kioaumbele chake awe na mtoto.

Sawa mimi siwezi kuzaa na mwanaume ambae sio mume labdaa itokee bahatii mbaya siwezi ku risk maisha yangu anaenipenda na mwenye utayari wa kuoa kwa wakati huo hanaga hizo slogan za nizalie mtoto kizazi changu sio cha majaribio
 
Back
Top Bottom