Exchange rate msaada

Exchange rate msaada

Mupirocin

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
1,739
Reaction score
748
Wakuu leo hii kwa msaada wa website ya NBC exchange rate kwa 1$, buying ni 1531.40 na selling ni 1616.40,
swali langu naomba wachumi mnisaidie je hapa exchange rate ya leo ni shilling ngapi? Je nachukua ile ya buying au ile ya selling au kuna formular maalum.
Mimi mara nyingi huwa nachukua ile ya selling ndo najua kuwa labda leo 1$=1616.40, Je huwa nipo sahihi? Naomba nifahamu nisiwe nabuni tena.
Natanguliza shukrani zangu za dhati.
 
Unatumia buying unaponunua dola bank au duka la kubadilisha fedha. Unatumia selling unapouza dola(unapobadilisha dola kupata pesa za tanzania) tofauti selling na buying ndio faida ya duka la kubadilsha fedha.
 
Sorry Buying unapobadilisha dola kupata tsh na selling unaponunua dola ie kubadilisha tsh kupata dola.
 
Sasa mkuu mfano nataka kununua air time ya dstv na wao wanauza in usd sasa hapa nitumie ile ya buying au ile ya selling, please
 
Sasa mkuu mfano nataka kununua air time ya dstv na wao wanauza in usd sasa hapa nitumie ile ya buying au ile ya selling, please

Hapa unatumia ya selling mkuu. Tena wao (DSTv, Hotels etc) huwa wana rate zao kwa siku husika. Kwahiyo tarajia kukuta wana rate kubwa zaidi (yaani wanakuibia zaidi) kuliko hizo ulizoziona benki.
 
Asante sana mkuu, sasa nimeelewa
 
Back
Top Bottom