Exclusive: Bifu zito kati ya Diamond na Rommy Jones

Exclusive: Bifu zito kati ya Diamond na Rommy Jones

Sasa we unaona sawa mwanaume kulelewa lelewa hadi boxa ununuliwe na nduguyo, najua we unaona kawaida make hata mshkaji wako kiba bado analelewa home mara alelewe kwa kidoti.... Sioni shida atalelewa na diamond hadi lini kwani ye ni tiffah
Sasa harmonize na rommy jons nani anafaa kusaidiwa we vp wewe"
 
Nani kakwambia Rommy katelekezwa? Acheni uchonganishi! Kama una ushahidi ana uza madawa weka hapa ushahidi..
Swala la romy kutelekezwa muulize mleta thread
Swala la madawa unamjua chief kiumbe tuanzie hapo"
 
Sio kweli unapoteza muda kuwachonganisha ndugu.
How nawachonganisha?! Kwa sababu ipi?! Penye ukweli uwongo hujitenga. Subiri utasikia yote soon binafsi sijafurahi ninayo yao na sina sababu hamna anaeniongezea wala kupunguza kitu kwako nasema ninachokijua kutoka huko huko kwao...na nishaona haina haja ya kuende coz hamna atakae amini...time will tell
 
Nilichosikia ni mambo ya kishirikina kua romy nyota yake imeshaisha so akiendelea kufuatana nae ni hatari so wamemuondoa kiaina na mama ndio alimwita kumwambia...siwezi mtaja alosema hayo ila mtakuja yasikia mda utafika tu
Hayo mambo ya kishirikina hata bikira wa kisukuma alishawahi kusema kwamba jamaa ni noma kipindi ommy dimples kachukua tuzo uk
 
Nilichosikia ni mambo ya kishirikina kua romy nyota yake imeshaisha so akiendelea kufuatana nae ni hatari so wamemuondoa kiaina na mama ndio alimwita kumwambia...siwezi mtaja alosema hayo ila mtakuja yasikia mda utafika tu

Mhhhhhhhh...... mabig haya
 
Swala la romy kutelekezwa muulize mleta thread
Swala la madawa unamjua chief kiumbe tuanzie hapo"
Kwa hiyo chief kuuza na D anauza? Una ushahidi lakini?
 
Nilichosikia ni mambo ya kishirikina kua romy nyota yake imeshaisha so akiendelea kufuatana nae ni hatari so wamemuondoa kiaina na mama ndio alimwita kumwambia...siwezi mtaja alosema hayo ila mtakuja yasikia mda utafika tu
Aisee hii siwezi kuamini kamwe...eti nyota imeshaisha daaa...
 
Watakuwa hawamfanyii vema rommy Jones ,rommy Jones ndo aliyekuwa clouds enzi diamond hajatoka,na akawa anarudia sana kupiga nyimbo za diamond na kuomba washikaji wapige simu za kuiomba ipate airtime ionekane diamond anapendwa,halafu Leo anamtosa?

Kuna ubaya kuandaliwa kujitegemea au labda mimi sijaelewa
 
Kuna bifu kubwa linaendelea chini chini kati ya Diamond Platinumz na binamu yake na mtu wake wa karibu Rommy Jones.

Chanzo cha bifu hilo japo wenyewe hawataki kuweka wazi inasemekana ni kitendo cha Diamond kumwambia Rommy aweke utaratibu wa kujitegemea yeye mwenyewe alafu yeye atamsapoti. Inasemekana Rommy hakufurahi kaona kama kadhalilishwa, kumbukeni Rommy hajui ata bei ya viatu kila kitu anawezeshwa na Diamond.

Wengine wanasema chanzo ni Zari inasemekana Rommy ambae ni swaiba wake na Wema alikuwa anajaribu kumshawishi kwa muda mrefu Diamond arudishe mapenzi kwa Wema huku akisaidiwa na Aunt. Hii ilimuuzi sana Diamond maana Diamond kwa sasa jicho lake lote lipo kwa mwanae Tiffa na mpenzi wake Zari sasa kuona mtu wake wa karibu anamshawishi kuvuruga furaha yake ikaleta doa kwenye uswahiba wao.

Kingine ni ishu ya Wasafi records label mpya ya Diamond ambayo kawekeza pesa ndefu lakini kampa usimamizi ndugu yake mwingine anaitwa Ricardo kuisimamia upande wa wasanii na studio na upande wa photo point kampa kifesi ambaye amemnunulia vifaa vya kisasa toka South Africa. Rommy anaona kama kawekwa kando kwenye ufalme wa Wasafi. Mama Diamond nae analaumiwa sababu ameegemea upande wa mwanae.

Mimi nawashauri awa watu wamalize tofauti zao wakae chini waelewane Rommy ajaribu kumwelewa Diamond kwa sasa ni baba hivyo kuna vitu lazima vibadilike akilini mwake hawezi tena kuwa yule Diamond aliokuwa anasikiliza ushauri wako na Halima na Petii.

Pia Dangote ajitahidi kumwelewa cousin wake ni mtu wa aina gani hawezi kubadilika fasta kama unavyotaka Rommy starehe ujiko na show off ndio imekuwa maisha yake tangia utoto awezi kufikiria kama wewe unaewaza future ya mwanao na mama na dada zako.

Copyright Jamiiforums

Acha uongo ndugu! wangekuwa na bifu ommy asingempost diamond cheki hii picha daki chache zilizopita
 
Attachments

  • 1450638310367.jpg
    1450638310367.jpg
    41.5 KB · Views: 557
Acha uongo ndugu! wangekuwa na bifu ommy asingempost diamond cheki hii picha daki chache zilizopita

Hiyo pic anazuga tu, ili kufunga watu midomo, maana watu wakiendelea kujadili mengi yatajulikana, ?a hawa ni ndugu, usishangae hata kesho D na R waka post pic wakiwa pamoja,
 
Back
Top Bottom