Exclusive: Diamond aeleza jinsi alivyolipokea shavu la Swizbeats

Exclusive: Diamond aeleza jinsi alivyolipokea shavu la Swizbeats

Kidingi

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2012
Posts
1,872
Reaction score
1,832
Diamond Platnumz ni mtu mwenye furaha kubwa baada ya producer maarufu wa Marekani, Swizz Beatz kupost video mbili kwenye Instagram zikimuonesha yeye na binti yake, Nicole Dean wakisikiliza nyimbo zake.

Diamond ameiambia 255 ya XXL kupitia Clouds FM kuwa, baada ya kugundua Swizz amepost video hiyo, aliamua kupost picha akiwa na Ne-Yo studio ili kuionyesha dunia kuwa kuna mengi mazuri yanakuja kutoka kwake.

“Nilikuwa nipo studio narekodi,” amesema muimbaji huyo. “Kidogo nikaambiwa Swizz kapost wimbo wako. Nikaona kama ananitania! Nikaangalia kweli, kidogo nikaona jamaa kanifollow, nikasikia raha. Nikakaa, nikabidi nitumie ujanja. Ikanibidi nirepost picha moja nikiwa na rekodi na Ne-Yo ili kutengeneza mazingira anapo ni preview aone hawa jamaa wapo vizuri, kuna kolabo ya Ne-Yo karibu inatoka. Kukaa dakika mbili akapost Nataka Kulewa. Ikabidi ni repost Nataka Kulewa. Kwanza nilitaka nirepost Nana, nikasema nikirepost Nana wanaigeria wataona kama Swizz kasilikiza nyimbo kupitia Nigeria. Ndio maana nikarepost Nataka Kulewa ili kuwaonyesha wanaigeria ni muziki wa Tanzania unakubalika,” ameongeza.

“Kwa mtazamo wangu mimi naona muziki wa Tanzania unaendelea kufanya vizuri. Unaonyesha zaidi kwamba unakubalika. Unajua sisi tunaimba Kiswahili na nyimbo ambazo tunaimba Kiswahili hawazielewi, kwahiyo ukiona wanasikiliza ujue tumepiga hatua. Huu ni wakati wasanii kushirikiana ili kufikisha muziki wetu mbali.”
 
Nikakaa, nikabidi nitumie ujanja. Ikanibidi nirepost picha moja nikiwa na rekodi na Ne-Yo ili kutengeneza mazingira anapo ni preview aone hawa jamaa wapo vizuri, kuna kolabo ya Ne-Yo karibu inatoka. Kukaa dakika mbili akapost Nataka Kulewa. Ikabidi ni repost Nataka Kulewa. Kwanza nilitaka nirepost Nana, nikasema nikirepost Nana wanaigeria wataona kama Swizz kasilikiza nyimbo kupitia Nigeria. Ndio maana nikarepost Nataka Kulewa ili kuwaonyesha wanaigeria ni muziki wa Tanzania unakubalika," ameongeza.

Hapo ndipo tunaita akili ya kazi. Kila opportunity haipaswi kwenda bure, lazima itumike ipasavyo. Mswahili wa Tandale uliyetumwa kutengeneza pesa.
 
una hakika au unaropoka tu
Basi usiwe mkali hujapandishwa coaster ila ulienda mwenyewe kuzomea, vp dhumuni lilikuwa nini???????? je, lengo lenu limefanikiwa?????????? vp munaposikia mafanikio ya muliyemzomea si ndo munajiba limewakwama kooni kabisa mana lengo lenu alijafikiwa ????????? vp mumebakisha silaha gani mana zile za, mchawi,freemason,anaiba nyimbo, anategemea wanigeria, na hii ya sasa ya mtoto si wake kufeli munakuja na ipi tena ??????
 
Basi usiwe mkali hujapandishwa coaster ila ulienda mwenyewe kuzomea, vp dhumuni lilikuwa nini???????? je, lengo lenu limefanikiwa?????????? vp munaposikia mafanikio ya muliyemzomea si ndo munajiba limewakwama kooni kabisa mana lengo lenu alijafikiwa ????????? vp mumebakisha silaha gani mana zile za, mchawi,freemason,anaiba nyimbo, anategemea wanigeria, na hii ya sasa ya mtoto si wake kufeli munakuja na ipi tena ??????
toa ujinga huo.
 
Big up do
Very creative waswahili watakuja kusema ulienda kwa mganga Morogoro wakati mganga ni wewe mwenyewe. Tumia akili yako na Nguvu zako utajingangia mwenyewe
 
Wasanii wengne kwanin nao wasijitume ben pol, barnaba kuna belle 9 kwanini wasitafute managment nzuri ikawasimamia mziki wetu wa Tanzania nataka uwe unasikilizwa dunia nzima! Diamond na Ommy Dimpoy ndiyo walio kuwa wanakuja kwa kasi ya ajabu ila dimpoz sijui kaishia wapi nae tena wakati kila nyimbo anayotoa inakuwa nzuri!
 
Back
Top Bottom