Exclusive: Diamond aeleza kwanini 'alidedicate' tuzo za Afrimma kwa Princess Tiffah

Exclusive: Diamond aeleza kwanini 'alidedicate' tuzo za Afrimma kwa Princess Tiffah

Kidingi

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2012
Posts
1,872
Reaction score
1,832
Muimbaji huyo aliyeshinda tuzo tatu za Afrimma Jumapili hii ameiambia ya XXL ya Clouds FM kuwa amefanya hivyo kwa sababu mafanikio yake yanachangiwa na mtoto wake huyo.

“Unajua ilikuwa ni moja ya ndoto zangu, kwamba hiyo siku nikipata tuzo halafu nina mtoto na nikaidedicate hiyo tuzo kwa mwanangu. Inaleta picha nzuri sana na ukizingatia najitahidi kufanya kazi kwa umakini ili kesho na kesho kutwa mwanangu amezaliwa baba yake nikiwa fulani halafu akue anikute nimefulia kweli? Itakuwa hata kumtazama naona aibu. Napenda mwanangu anikute wakati Diamond yupo kwenye ukubwa wake,” alisisitiza Diamond.

Aliongeza, “amekuwa akinipa changamoto sana, kama kuimba niimbe sana, kutunga nitunge sana, kama kujituma nijitume sana. Kwahiyo nakuwa namuwaza kwenye kichwa ndio maana nikasema nimdedicate hii tuzo kwake. Unajua zamani nilikuwa nikisikia wazazi wanapenda watoto wao naona sometimes ni maneno yao tu. Lakini sasa hivi nafeel kabisa upendo yaani hata mtu akiweka picha mbili akinidiss mimi akamsifia mwanangu hainiumi sana kama kanidiss naona bora alivyomsifia mwanangu.”
 
DIAMOND wewe unajua na mbinu zinazokufanya uwe juu kwa sasa zifanye mara 100 ya hapo ili hawa waliojivisha u-king wajute kujilinganisha na wewe.
 
Back
Top Bottom