Exclusive: Haya ndio mambo ambayo Alikiba anahisi kufanyiwa ili asifanikiwe

Exclusive: Haya ndio mambo ambayo Alikiba anahisi kufanyiwa ili asifanikiwe

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Bongo5 imemtafuta mtu wa karibu kwenye uongozi wa Alikiba kutaka kujua kile ambacho wanahisi msanii wao anafanyiwa na wengi hawavijui.

Mtu huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe, alidai kuwa kuna watu ambao wamekuwa wakifanya kila wawezalo ili kuhakikisha kuwa Alikiba hafanikiwi kimataifa.

Ametolea mfano video za Mwana na Chekecha Cheketua pamoja na kuwa na viwango vinavyokubalika na kuongozwa na waongozaji mahiri barani Afrika, kituo cha MTV Base hakijawahi kuzicheza na wanapokuwa wakiuliza sababu wameshindwa kupewa maelezo yasioeleweka.

Tunawatumia MTV Base, video wanazipokea na wanatuma confirmation ya kuzipitisha lakini hatuelewi kwanini hawazichezi tena, amesema.

Amedai kuwa waliwapa Soundcity kipaumbele cha kucheza video ya Mwana kwa mara ya kwanza lakini baada ya hapo video hiyo haikuwahi kuchezwa tena.

Hata zile Top Ten East yao haikustahili kuingia kweli? Kuna video ngapi za Afrika Mashariki zinaingia kwenye top ten na zingine ni za kawaida tu iweje Mwana isichezwe? amehoji.

Kinachoshangaza zaidi, kuna watu wanawaambiaga wasanii ukitaka kutoboa tobo kimataifa lazima upitie kwao.

Kwa mifano hiyo amedai kuwa Alikiba anahisi kuna watu wanaofanya kila njia hata kwa kumwaga fedha ili kuhakikisha kuwa jitihada anazozifanya hazifiki popote na kwamba kitu hicho kinamnyong'onyeza sana.

Ametoa mfano jinsi ambavyo Alikiba anakubalika nchini Kenya anakopachukulia kama nyumbani pia.

Ametolea mfano wimbo wa Nagharamia alioshirikishwa na Christian Bella kuchezwa kwa zaidi ya mara 10 kwenye kipindi cha Classic 105 Maina In The Morning kinachoendeshwa na Maina Kageni aliyewaambia kuwa hakijawahi kutokea kitu kama hicho kwenye historia ya show hiyo.

Kuhusu tuzo, amesema uongozi pamoja na Alikiba mwenyewe wameamua sasa kutojihusisha na na baadhi ya tuzo wanazohisi zina mrengo wa kibiashara zaidi.

Ali ameamua kuweka focus yake zaidi kwenye muziki wake na mashabiki na sio tuzo, amesema.

Hafanyi muziki ili apate tuzo anafanya muziki kwa ajili ya mashabiki zake. Tuzo zitakuja tu by the way lakini sio his main focus. Why Tuzo nyingi duniani siku hizi zinaanzishwa au zinaendeshwa kibiashara zaidi.

Ni tuzo chache ambazo zimebaki kwenye misingi na zina credibility ya kueleweka. Kwa mfano tuzo zile Afrimma za US walimuweka kwenye kipengele cha upcoming, Ali ni legend. So unaweza kuona kabisa kwamba hawafutilii wanaweka tu watu ili tuzo zao zipate kiki, amesisitiza.

So alichoamua yeye baada ya kuzungumza na management kwamba from now on hatojihusisha kabisa na awards ambazo hazina credibility,ambazo zimeanzishwa au zipo kwa ajili ya kutumia wasanii kibiashara au kwa manufaa binafsi ya waandaji na sio kuwatuza kutokana na ubora wa kazi zao.

Ali atashiriki kwenye awards lakini zile ambazo zina mrengo wa kuwatuza wasanii kwa ubora wa kazi na sio zenye mlengo wa kuwatumia kibiashara na mwishowe zinatengeneza vita/uhusiano mbaya baina ya wasanii.

Mfano mwingine ni hii Afrima ya Nigeria walimuweka kwenye categories ambazo hakustahili kama Album of the year, Ali hajatoa albam since 2009! Hizi zote zinaonyesha hawana umakini na wanafanya tu vitu kwa kukurupuka bila ufuatiliaji mzuri, hence no credibility.

Pamoja na yote hayo Alikiba anadai anapenda watu wafahamu kuwa yeye si mtu mwenye kinyongo na mafanikio ya wasanii wengine na kwenye mahojiano na Diva aliwapongeza Diamond na Vanessa Mdee kwa ushindi wao.

Wengi hawanijui tabia yangu lakini wanahisi labda mimi nina wivu ama nini. Hapana mimi nasupport muziki na nampenda kila mtu,alisema Kiba.


Chanzo:
bongo5
 
Kujistukia kubaya sana unaweza dhani kila mtu ni adui yako...
 
Basi sawa. Tumekuelewa kaka,endeleza mapambano.
 
Eeeh atachagua tuzo za kuwania kama Afrima ilikuwa haina umuhimu na sio kusaidia wasanii mbona hakuandika kuomba wamtoe kwenye kuwania tuzo

Amekwisha kabisa huyo mbaba kwakweli anatia aibu taifa letu

Wivu umemjaaa akae na akwende zake hukoooooo mfano mbaya kwa wasanii machipukizi wasisikilize kabisa pumba zake.
 
joto hasira hakuna ligi bila kombe kubali tu umeshindwa pumzika kibakuli wakati wako kushney waachie kina harmonize sasa
 
Eeeh atachagua tuzo za kuwania kama Afrima ilikuwa haina umuhimu na sio kusaidia wasanii mbona hakuandika kuomba wamtoe kwenye kuwania tuzo

Amekwisha kanisa huyo mbaba kwakweli anatia aibu taifa letu

Wivu umemjaaa akae na akwende zake hukoooooo mfano mbaya kwa wasanii machipukizi wasisikilize kabisa pumba zake.

hana lolote....apumzike tu sasa alee watoto wake...maana ameshaishiwa huyu
 
Well ngoja tumpe kiki mara ya mwishomwisho maana ndio anachotaka

Na kama ndio hawa watu wanaomzunguka na kumpa ushauri basi anahitaji mfungo wa maombi

+Yupo kwenye game tokea 2004 hukoo diamond amekuja kusikika 2009, je aliwahi kupata tuzo gani kabla ya mafanikio ya diamond?? je aliwahi kufanikiwa kucheza video yake kwenye kituo gani cha kimataifa mpaka uje useme anafanyiwa hujuma??

+Alivyo boya, wanalalamikia Sound city top ten east, kipindi ambacho hakikuwepo ila Diamond Platnumz alivyotoka ndio akawaomba waanzishe 2014 akafanikiwa kwa hilo, wasanii wetu wakaanza kuonekana hiyo tv, Lakini hawajatoa shukrani za dhati zozote kwake ndio kwanza wanampandikizia chuki..

+Kusema kuna hujuma MTVBASE, TRACE TV, SOUND CITY, hahaha ni vile tu ni msanii mdogo maana ingekuwa Diamond hiviii hiyo ishu ingemuaribia mnooo maana ingekuwa imesambaa sana Afrika kwenye blogs kuwa na baadh ya tv... Hapo hajui kwamba anavituhumu vituo vyenye heshima kubwa Afrika kwamba ni corrupt, na havizingatii maadili ya kazi, upuuuuzi uliopitiliza..!!


Wanasema hawana wivu na maendeleo ha Diamond na Vanessa ila mwisho wa siku wanahoji kwanini wao tu ndio wanafanikiwa, saaaa mbovuu kweli!!!!!!!
 
Kwahyo anamaanisha watu walifanya figisufigisu ili asihudhurie kwenye utoaji wa tuzo!!!
 
Useless..kiki za kipimbi. Si akavue dagaa tu. Hu hit kuna mwisho. Hata Icon muda wake ukifika atakaa tu.
 
endeleeni kununua
Kidingi kawauliza je, kabla ya DIAMOND kutoka mulishapata tuzo au nyimbo zenu kuchezwa tv na radio za kimataifa ????
Alipopata tuzo za pombe alijiona yeye ndio yeye anajua muziki kelele nyingi sasa kanyooshwa anaanza kutoa visababu imekula kwake kule hayupo Wema Sepetu ampigie debe kule ni ubora wako ndio unakupa tuzo.
 
Last edited by a moderator:
Kidingi kawauliza je, kabla ya DIAMOND kutoka mulishapata tuzo au nyimbo zenu kuchezwa tv na radio za kimataifa ????
Alipopata tuzo za pombe alijiona yeye ndio yeye anajua muziki kelele nyingi sasa kanyooshwa anaanza kutoa visababu imekula kwake kule hayupo Wema Sepetu ampigie debe kule ni ubora wako ndio unakupa tuzo.
endeleeni tu. ila ipo siku mtaelewa tu
 
Last edited by a moderator:
endeleeni tu. ila ipo siku mtaelewa tu

Yani tokea tumewanyoosha wenzako wamekimbia kabisa, hivi imewauma sana? hahahaha le super mubebez nimemmis mnooo cute b king kiba ashagharamiwa na chibu dangote huku hahaha tumenunua kifurushi cha tuzo cha miaka 10 na tunampango wa kuongeza ili tumuachie kabisa na harmonize...!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom