Afisa Mteule Drj 2
JF-Expert Member
- Mar 21, 2017
- 3,865
- 4,506
Du sijui na sisi 2020 itakuwa hivi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Akina Ruttashobolwa hawataki hayo mambo yenu ya uwazi! Wanasema yataleta vurugu!! Ukitenda haki au kudai haki kwao ni vurugu!ndiyo maana hapa ukijaribu kumwonyesha mbele penye mto yeye analazimisha kuwa kwa Nini tusiuvuke kinyumenyume!!Africa ni bara la ajabu mno mno maana always tunaangalia tulipoangukia sio kujikwaa,ni huzuni mno maisha ya binadamu wenzetu yanapotea hivi bila ya sababu maalum,why kura zikishapigwa kituoni ,kuhesabiwa pale na kuingizwa moja kwa moja katika mfumo mkuu wa matokeo kuwa tatizo ?mbona wenzetu hapa hapa SADC wanafanya hili kwa hiyo aliyeko nyumbani,au kwenye ktuo kikuu cha makusanyio ya kura unapata matokeo moja kwa moja,wote mnaangalia kwenye big screen kura zikiingia na mshindi kuanza kuonekana mapema ?
Acha ulongo wako! Nani kasimlia kuwa mwanamke alimwambia kuwa wapite barabara fulani! Wakati waliokuwa wawili na wote wamekufa! Ukamatwe kusaidia polisi!Baada ya taarifa ya Kifo cha aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IECB Bwana Chris Musando kutokea jana niliweza kujiridhisha ' Kitaarifa ' zaidi kutoka kwa ' Wadau ' mbalimbali wa Kenya ambao baadhi yao wanahusika moja kwa moja ya masuala ya Uchaguzi Mkuu ujao huku wengine wakiwa ni ' Wabobezi ' wa Investigative Journalism huko Kenya ambapo kwa pamoja walinithibitishia mambo makubwa saba ( 7 ) yaliyopelekea Kifo hiko cha ' Kikatili ' kabisa.
Yafuatayo ni matukio ambayo Marehemu aliyafanya siku nne ( 4 ) tu zilizopita kabla ya hayo ' Mauaji ' yake ya ' Kikatili ' kutokea hivyo nitayaweka hapa kwenu ili kila mmoja ayaangalie na ayafanyie ' tathmini ' mwenyewe ' Kimoyomoyo ' kisha mwishoni wote tutajua ni nani ' Kamuua ' Marehemu Chris Msando.
Tukio #1.
Kwa niaba ya Tume nzima ya IECB Marehemu alipeleka ombi Serikalini la kupewa Ulinzi wa Yeye na wenzake wote lakini hadi mauti yanamkuta hakujibiwa wakati alipopeleka maombi ya mengine yahusuyo ufanikishaji wa ' Oparesheni ' za IECB alijibiwa na kupewa ' Ushirikiano haraka sana.
Tukio #2.
Siku tatu kabla ya Kifo chake Marehemu alikwenda Police kupeleka taarifa za Yeye ' Kutishiwa ' maisha na Watu asiowajua lakini hakuna ' Ulinzi ' aliopewa hadi Umauti yanamkuta hiyo jana.
Tukio #3.
Marehemu huko nyuma alishapewa ' Onyo ' kali la kutozungumza na Chombo chochote cha Habari nchini Kenya na ' Mamlaka ' na kuambiwa kwamba Mtu pekee ambaye angetakiwa kuzungumza na Media basi ni Waziri tu husika wa Habari na Mawasiliano.
Tukio #4.
Siku mbili tu kabla ya Kifo chake Marehemu Msando ' alikaidi ' hiyo amri kutoka katika ' Mamlaka ' ambapo alikubali mualiko wa kwenda kufanya interview na Kituo Kimoja cha Television nchini Kenya ambapo aliyoyasema huko inasemekana kuwa ndiyo yaliharakisha ' mauaji ' yake.
Tukio #5.
Wakati akiwa ' mubashara ' kabisa akizungumza katika hicho Chombo cha Habari Marehemu alisikika ' akiwahakikishia ' Wakenya wote kuwa kwa jinsi alivyotengeneza ' Mfumo ' wa Kimawasiliano wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya ya IECB hakuna Mtu yeyote yule atakayeweza ' Kuudukua ' hata iweje na akaenda mbele kusema kwamba Mtu akitaka ku ' hack ' taarifa zozote za Tume ya Uchaguzi IECB basi labda akatwe ' Kiganja ' chake kwani ili upate taarifa zao ni mpaka Yeye ( Marehemu ) atumie ' Kiganja ' chake cha Mkono ndipo Mtu mwingine apate taarifa za Tume.
Tukio #6.
Marehemu bila kujua mbinu za ' Kimafia ' na labda pengine alijisahau kuwa siku zote ukitaka tu ' Kuuawa ' Kimafia basi Mtu wako wa Karibu sana ama Nduguyo au Mpenzi wako au Rafiki yako tu wa karibu ndiyo hutumika sana kukumaliza. Marehemu usiku kabla hajafariki alifuatwa na ' Mwanamke ' ambaye inasemekana anamuamini sana ndipo huyo ' Mwanamke ' kwakuwa tayari alishapewa maagizo yote ya ' Kimafia ' ndipo akamtega Marehemu kuwa wapite barabara fulani ambapo kumbe huko mbele ' Wauaji ' wake wale ' Mafia ' walikuwepo.
Tukio #7.
Ili kuonyesha kuwa ama hakika ' Wauaji ' wake wa ' Kimafia ' walichukizwa na Kitendo cha Marehemu kwenda mbele ya Media na kusema kwamba safari hii katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya hakuna ' Udukuzi 'wowote utatokea kama ilivyokuwa Uchaguzi uliopita labda akatwe Kiganja ' chake ndipo hata katika ' mauaji ' yake ya juzi ' Kiganja ' chake cha Mkono ndiyo kilikatwa na kuondoka / kuchukuliwa na hao ' Wauaji ' na kuuacha mwili wake ukiwa na majeraha mengine shingoni, machoni na tumboni.
Na kama zilivyo Kanuni Kuu za Kimafia dunia nzima ni kwamba Yule ambaye atakuwa kafanikisha ' mauaji ' ya Mtu fulani aliyelengwa basi ni lazima nae pia mwishoni auawe ili kufuta ama kuondoa kabisa ushahidi wote kitu ambacho ' Wauaji ' hawa walikifanya kwa ' Kumuua ' na Yule Dada ( Mwanamke ) pamoja na Marehemu na hatimaye mwishoni ikawa ' Mission Accomplished '.
Soma tu kimoyomoyo na ukishamjua ' Muuaji ' Mkuu wa Marehemu Chris Musando basi baki nalo pia moyoni. Mwishoni jiulize tu swali kwamba ni kwanini Marehemu alipoomba msaada wa Police hakupata ushirikiano ila baada ya kufariki jana Police wa Kenya wameonyesha ' Ushirikiano ' mkubwa Kwake ( Maiti ) huku wakiwazuia hadi Watu wengine sasa kwenda kuuangalia mwili wa Msando na kukataa kufanyike independent post-mortem ambapo hata Balozi wa Marekani nchini Kenya alikuwa tayari kuigharamia kutokana na kwamba hata wao Wamarekani ' wamechoka ' na haya mauaji ya ghafla na ya kusikitisha yanayotokea nchini Kenya kila uchao halafu Serikali haichukui hatua yoyote ile kuyakabili / kuyadhibiti.
Nawasilisha.
I like your thinking. Mm tangu ile food poisoining nilianza kuihoji sana. Inawezekana vipi muaji apate nafasi ya kukuwekea sumu halafu iyo sumu isiwe ile inayiua kwa upesi zaidi.Maelezo yako mbona yana hitimisha kuwa kuwa Jubilee ndio wamehusika? Kwanini si NASA kwa kutafuta public sympathy kupitia mgongo wa Kura kuibiwa na kuingiza nchi kwenye machafuko? NASA hata kabla ya kupotea kwa msando walileta story za kuibiwa kura na hata baada ya Msando kupatikana ndio wameonesha wazi kuwa hawana imani na mfumo wa matokeo ,,,,Kwanini sio kwamba hili jambo limepangwa ili kuonesha ulimwengu kuwa Kura zinaibiwa?
Mimi bado nina wasi wasi kabisa na pande zote kuhusika........maana mazingira ya kifo cha Msando bado kina waweka kwenye mashaka pande zote mbili kuhusika...
Maelezo ya huyo mwanamke nani aliyatoa na kufanikisha kuandika? Kama Watu wamezuiliwa ni nani ameona kwamba kidole kimekatwa! Nani anajua kuwa huyo mwanamke alikuwa msiri wake??
Wew na baba jesca hakuna utofauti...soma tena na tumia akili yako ya kibashite kujijibuMaelezo ya huyo mwanamke nani aliyatoa na kufanikisha kuandika? Kama Watu wamezuiliwa ni nani ameona kwamba kidole kimekatwa! Nani anajua kuwa huyo mwanamke alikuwa msiri wake??
Ukweli ni kwamba ukiliangalia hili jambo kwa umakini utagundua kuwa NASA wamesha shindwa sasa wanacho tafuta ni kuhalilisha kura zimeibiwa na hawashindwi kufanya chochote... ni Jana NASA wamehoji usalama wa Kura zao ati kwa sababu Msando aliuwawa...sasa bado najaribu ku connect dot isije kuwa ilikuwa njia ya kuhalalisha kuwa Kura zinaibiwa na kukataa matokeo haya..I like your thinking. Mm tangu ile food poisoining nilianza kuihoji sana. Inawezekana vipi muaji apate nafasi ya kukuwekea sumu halafu iyo sumu isiwe ile inayiua kwa upesi zaidi.
Hapa unahitaji independent thinking kufikiri in 3D
unaemuuliza ni nani haswa?Maelezo ya huyo mwanamke nani aliyatoa na kufanikisha kuandika? Kama Watu wamezuiliwa ni nani ameona kwamba kidole kimekatwa! Nani anajua kuwa huyo mwanamke alikuwa msiri wake??
mawazo ya mwanaCCM utayajua tuUkweli ni kwamba ukiliangalia hili jambo kwa umakini utagundua kuwa NASA wamesha shindwa sasa wanacho tafuta ni kuhalilisha kura zimeibiwa na hawashindwi kufanya chochote... ni Jana NASA wamehoji usalama wa Kura zao ati kwa sababu Msando aliuwawa...sasa bado najaribu ku connect dot isije kuwa ilikuwa njia ya kuhalalisha kuwa Kura zinaibiwa na kukataa matokeo haya..
Kwa Vyovyote vile hakuna upande wowote utakaoshindwa na kukubali matokeo hasa NASA..
Mimi naona kuepusha vurugu ni Kura kuhesabiwa Manually....
Naskia Raila anataka proffesional IT atoke Uingereza kukaimu nafasi ya Msando....
Najiuliza hawa wazungu hatakuwa na interest zao wakamweka atakaye kuja kuangalia maslai yao?...
Tunaweza kusema kuwa tume ya uchaguzi ya kenya ni huru zaidi na Ndiyo maana option pekee wanayoona inafaa kwa sasa ni labda kuondoa uhai wa mtu!! Kama iNgekuwa ya hovyo kama ya Tanzania basi ilikuwa ni suala la kumpigia simu mwenyekiti wa tume aende ikulu akachukue 'draft' la matokeo yanavyopaswa kuwa! Same ol rubbish!Rutta: afrika hakuna tume huru za uchaguzi jamaa kauawa ili wafanikishe kurudi madarakani kwa mlango wa nyuma, kwani naibu waziri wa mambo ya ndani wa kenye naye yuko upande fulani hata wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa waziri wa wizara hiyo last month aliwataka wakenya kupiga kura na kurudi nyumbani na akaahidi kumwaga askari wengi siku hiyo. No democracy in kenya
Sent using Jamii Forums mobile app
"Upumbavu wetu waafrica na madictator wengine popote duniani ungeelekezwa zaidi katika kuutangazia umma wa wananchi kuwa hatuna haja ya kufanya uchaguzi"Ni kweli alikuwa na upande ambao ni upande wa haki kitu kinachoendana na kiapo chake. Mawazo yako yanafikirisha lakini yamekaa 'kikwenu' zaidi. Nadhani upumbavu wetu waafrika na madikteta wengine duniani katika ujasiri wa kuiba kura ungeelekezwa katika ujasiri wa kuwatangazia wananchi kuwa "hatuna haja ya uchaguzi" ingelikuwa na maana zaidi kuliko kupoteza muda na watu muhimu!
BBC walikwisha ripoti kuwa marehemu alikatwa mkonoMaelezo ya huyo mwanamke nani aliyatoa na kufanikisha kuandika? Kama Watu wamezuiliwa ni nani ameona kwamba kidole kimekatwa! Nani anajua kuwa huyo mwanamke alikuwa msiri wake??