Exclusive interview: Diamond na Vanessa Mdee baada ya kupata tuzo

Exclusive interview: Diamond na Vanessa Mdee baada ya kupata tuzo

Hilo tatizo la directors wa kibongo ni ugonjwa wa wabongo wengi sana.
Hata mama muuza chapati akiona anapata wateja wengi huwa haonyeshi kujali wateja mpaka pale wateja watakapoanza kumkimbia.

Umeonaeee
 
Ndo maana watu wanasema ukileta ushikaji kwenye kazi kazi haifanyiki ukileta undugu kwenye biashara unafilisika safi sana diamond kwa misimamo yako utafika mbali

Well said, hapo bila ushabik diamond kaongea fact, na hz production bomu za kbongo ndo znachangia kuua huu mziki, acha kaka mond afanye yake anayejua maana ya tym management huwa hana muda wa kuipoteza hta dk1
 
Nafikiri imeshaanza kuchezwa na uko

10568058_320116788157657_1571268119_n.jpg


5326_776616179026865_6305633365773555151_n.jpg

Hiyo ya MTV Base ni wimbo wa Shetta aliomshirikisha Diamond. Iko namba 6 wiki hii.
Bum Bum ilipigwa Trace kabla haijapigwa huku, ila haijaingia kwenye chart.

Ila kwa kukusaidia STV Music sio channel kubwa kama ulivyotaka watu waamini hapa.
 
Hongera,penye mafanikio lazima wsnafiki wawepo
 
Diamond namkubali sababu nimkweli na anasimamia humohumo..waTZ Tukiacha chuki kwa wenyekupiga hatua kuyaelekea maendeleo tutafika mbalisana..

Ni moja kati ya wasanii wachache wanaosema ukweli. Hafichi kama kakulia tandale na hamfichi mama yake mzazi! Kiukweli hata anaposema anajituma kwa kuwa hataki kurudi kwenye maisha ya dhiki aliyoishi utotoni hilo ni somo kwa wenzake. Pamoja na yote aniboa sehemu moja tu,anatangaza kwa mbwembwe mallaya aliotembea nao!..ummalaya sio sifa hata kidogo!
 
Hii interview imefanyika leo 7/31/2014

AZUNGUMZIA KUFANYA VIDEO NJE YA NCHI:

''Unajua madongo mengi yanayorushwa kuhusu wasanii wa bongo kufanyia video nje najua narushiwa mimi ila naamua kukaa kimya tu''...........

Anaendelea..." Mie siwezi kufanya video na madirector wa kibongo kwa sasa kwa sababu ni wazinguaji sana....Tatizo sio quality inayonikimbiza bongo ila utendaji wa kazi haswa ndio tatizo kubwa, hawathamini wateja wao(directors).

Mtu unamlipa pesa ila kufanya kazi inabidi umbembeleze,Nimeshawahi kususa video mbili kwa director nikiwa nimeshazilipia kila kitu, baada ya kuzifatilia nakuishia kuzungushwa miezi minne.

Ni video ya 'Nimpende nani na Lala salama', Nimeshawahi kumlipia ticket ya ndege director twende tukashoot South Africa na akaishia kunizingua.
Mtu unaamshwa na director saa kumi na mbili asubuhi ufike location, unafika unamsubiria yeye anatokea saa 4.

MaDirector wa nje wanakutreat mpaka unaona thamani yako kama msanii, pia wanaangaikia mpaka kukuconnect na media kubwa. Hapa kwetu ukisharecord unaangaika mwenyewe na bado mtu anakutreat kama anakupa msaada wakati pesa yote aliyotaka umempa''.

Azungumzia Changamoto:

''Changamoto kubwa ni kupata lawama, ujue kwa sasa nina marafiki wengi na najuana na watu wengi sasa kumridhisha kila mtu inafika kipindi nashindwa.

Unakuta unapata maombi mengi mfano ya interview mfano, sasa ratiba yangu ni tai sana ata muda wa kupumzika nakosa na ninatakiwa uku na uku, nikikosa uku unakuta mtu anajisikia vibaya anaona umeanza kumdharau na ata nafasi ya kumwelewesha nashindwa Dah hicho kitu uwa kinaniumiza sanakuliko vyote sababu mie sipendi kumuudhi mtu anayenisapot ila kama binadamu sometimes nashindwa you know msayn! ''.

'' Changamoto nyingineyo, nina watu wanaonpenda na kuniamini sana na wanaamini sitowaangusha ata siku moja. So wanafanya nifanye kazi kwa nguvu nyingi nisiwaangushe''........Anaendelea.''

Unakuta mtu ni shabiki wako mnakutana airport,umechoka kinoma unawaza kupumzika tu, anatokea anaomba mpige picha, inabidi ukubali na utupie na tabasamu japo upo hoi''

Aulizwa na Vanessa kama ana uwezo wa kurap, anaomba apewe beat achane....apewa beat ya laini aikataa anaomba beat ngumu........Anaonyesha uwezo wa kurap pia.


MENGINE ALIYOONGEA

'' Unajua muziki wako kwa sasa ukipita Nigeria ndio umepita Africa''.

'' Passport yangu ya pili inakaribia kuisha hapa nilipo nina visa kibao mkononi...unajua nasafiri sana ninachoka lakini siwezi kukaa chini inabidi nitumie huu wakati''

'' Wategemee collabo ya nyingi sana, zingine ni za nje ya Africa....nikitoka hapa naenda studiio kurekodi nyimbo ya collabo na Case wa Nigeria ni nyimbo yake''

'' Idea ya video ya Mdogomdogo ilianzia kwa Adam Kuambiana, baadae tukaiboresha mimi na Wema''

'' Nimemuona Rihana LIVE, alikaa nyuma yangu siku iyo.....yani nilikuwa sielewi chochote kugeuka nyuma namuona mtu kama Rihana, sikuamini ikabidi nigeuka zaidi ya mara mbili uku najiuliza hivi uyu si Rihana uyu?

Ikabidi nipotezee kama sijashtuka vile,ila kwa kweli kushangaa sio siri hakuniishi sababu vitu vingi tulikuwa tunavisikia tu nakuviona vya ajabu''
Fanya kazi diamond mungu atakubaliki kijana wewe ndo I cone wa Tanzania for now najua wanakuponda but Simu zao zimejaa nyimbo zako Wabongo wengi no wanafiki hata A.Y alishasema.. Jitahidi utoke na nje ya Afrika..jitahidi na wewe uwashilikishe Kwa sana.. God be with you..
 
Fanya kazi kijana achana na hao madirector viazi hela yako mwenyewe halafu unyanyasike we songa mbele watapika majungu wee siku wakiyapakua we haupo hapo tena wanakuona diamond yuleeeee
 
Kiukweli huyu jamaa anajitahidi sana kuanzia kuimba na hapa performances zake jukwaani! Amesema ma-director wa kibongo ni bomu, japo pia video za kibongo quality pia ni nzuri lakini mimi hapa nakataa, video nyingi alizofanyia nje zina quality nzuri sana! Hii iwe changamoto tu kwa video producers pamoja na ma-director wa kibongo bongo!
 
Hongera sana kaza buti achana na haya maneno ya walio shindwa wasije wakakufanya nawe ushindwe
 
I wish diamond afanikiwe zaidi na wote wanaojituma kama yeye. Japo sitapata faida yoyote zaidi ya burudani kutokana na nymbo zake. Goodluck mtt wa Tandale
 
Back
Top Bottom