Hii ni very exclusive and the best ever interview kati ya mtangazaji mwanadada huyu wa NijuzeNews TV na Wakili Msomi Peter Madeleka juu ya mambo mbalimbali ya nchi na taifa letu
Peter Madeleka udhaifu wake katika baadhi ya maamuzi yake kama binadamu. Mfano kukataa kuwa kauli mbiu ya CHADEMA ya NO REFORMS NO ELECTION haina mchango ktk mabadiliko yatakayotokea muda si mrefu ktk mifumo yetu ya utawala na uchaguzi ni kujitoa ufahamu kwa kiwango cha juu sana..
Peter Madeleka anasema, mabadiliko yanayokuja ya kisheria, kikatiba na utawala ni kwa sbb yeye aliamua kushiriki uchaguzi wa 29/10/2025 na kuona mauchafu hayo na kwa sbb hiyo, ndio maana anasukuma mabadiliko Leo๐๐
Huu ndio udhaifu wake kwa sbb huu ni uongo na ni kuchezea akili za watu wenye ufahamu..
===============
Generally, katika interview hii amefanya vizuri na ametoa hoja nyingi za msingi na zenye kufungua ufahamu na elewa wa wengi...
Kwa ufupi amesema yafuatayo;
1. Ameiponda Tume ya pili ya Rais Samia baada ya ile ya Jaji Chande iliyochunguza matukio ya wao waliiyaita "ya uvunjivu wa amani ya 29/10". Hii ya pili chini ya Jaji Mstaafu Lilla inachunguza kitu kilekile tena lakini imeongezewa kitu kimoja tu "kuchunguza jinai" na hadidu zao za rejea ktk uchunguzi wao ni:
โ Kina nani walikuwa chanzo?
โKina nani walitoa fedha kuwapa waandamanaji?
Wakili Peter Madeleka anauliza: kama hizo ndizo hadidu za rejea, mbona ya KINA NANI WALIUA WATU HAIPO??
2. Ameponda uongo wa serikali kuhusu uwepo wa ugaidi Tanzania. Amesema kuwa, ni wazi kuwa viongozi wa serikali ni kama hawana akili na pengine wamechanganyikiwa. Amemponda sana Patrobas Katambi na maelezo yake ya kujichanganya kuhusu ugaidi. Amesema, unaweza ukawa kiongozi mwenye cheo lakini ukawa huna akili, ufahamu wala uelewa wa mambo hususani sheria. Ndivyo alivyo Patrobas Katambi. Ni kiongozi na waziri lakini ni mjinga!!
Ukitaka kupata ufahamu zaidi, fuatilia interview hii mpaka mwisho. Peter Madeleka ana udhaifu wake kama binadamu. Lakini, hapa amefanya vizuri sana. Watu wengi tumemwelewa!