Exclusive: Jay Dee afunguka, atoa sababu za kuitosa ndoa yake


H.O.E this is pathetic n so sad...! Imenifanya nikumbuke nyimbo za Alicious ft Juliana MPITA NJIA hasa ule ubeti usemao 'mwizi wa mapenzi Asante yake mateke kwako hatakaa milele na ule wa Phill Collins nafikiri DON'T FALL IN LOVE WITH A DREAMER
 
Ninachompendea Jide ni misimamo yake, na uwezo wake wa kumanage maisha binafsi yasiingiliane na maisha ya usanii. Pamoja na matatizo aliyokuwa nayo kwenye ndoa, bado kaweza kuhimili kwenye muziki bila kutetereka.
 

Unajua Jide ni mkorofi sana daa yani hapo kashahamua liwalo na liwe yuko tayari kwa vita nyingine! Unajua mimi mwenyewe sijapenda Jide kuyaongelea hayo lakini niligundua Jide ana mzigo mkubwa na kuanzia kichwani hadi moyoni pengine huu ndio mwanzo wa kupunguza mizigo!
 
Au tatizo la kutopata mtoto ndo lilichangia haya yote?
 
Walivyokuwa wana act kwenye DIARY, utadhani kweli wako kwenye ndoa ya furaha+
Mapenzi haya!
 

Mkuu yule Dada anatapatapa....na anadhani ndio relief hiyoo..
 
Yeah siku hazigandi sema Jide alimpenda saana Gardner... mambo ya kuolewa ba mtu ukiamini He will change, nitambadilisha kumbe hamba kitu
tume will heal her broken heart

Na hapo ndio hoja yangu ilipo asante madam.....kwa akili ya kawaida mtu anayeweza kukupenda wewe baada ya kumshawishi amuache mwenzake aliyenae,huyooo sio mtu mzuri na usitarajie mabadiliko kwake..

So hiki anachokilalamikia hapa she's the source of it....asitafute sympathy za kilofa....alidhani chozi la mwanamke mwenzake lingeenda bure kama la.samaki????
 

Dah hivi kama kweli unampenda mtu unaweza kushawishiwa umuache.. huyo Gardner alimuacha mkewe kwa maamuzi yake mwenyewe mbona umekazania jayd ndo kasababisha halaf Gardner humuongelei.
Mnaovunja ndoa ni nyie wenyewe wanandoa na sio mtu wa nje.. kama wangekua dhabit kwenye ndoa yao unadhan wangeachana??
 
Mi kwa upande wangu naamin Jide ndie mwenye maumivu makali sana moyoni.kwani ndie aliempenda G ,haya yoote mala nyingi watu wa mujini husema HAYO NI MANENO YA MKOSAJI......Jide wakati anatumia pesa kumpata G aliumiza sana moyo wa dada Mmoja hivi huko Mwanza dada huyo aliitwa Idda,Idda ndie alizaa na G Mtoto Mmoja wa kike,aliteseka sana na Hali Kama hii baada ya dada yetu kuingilia Penzi Lao,huyu Jide ni MSHAHARA WA YALE ALIYOTENDA.......Nina iman Jide anayo mateso Makubwa sana juu ya kuachana na G.......kamwe jambo hili haliweZi toka mapema kichwani mwake maana ndie hasa alikuwa mwenye Penzi kwa G......pole sana Jide
 
Sasa ni zamu yako kunywa pombe kukesha kwenye Bar kutembelea hata wale ambao hukuwahi kufikilia kufika kwao kwa kesi hii woote utaona kuwa nao utapata nafuu.....pole sana Jide kipindi unatumia pesa kumpata G mwenzio alikuwa hapati usingiZi hawezi kula akakonda Mawazo Mengi mabaya yalimwijia,alichoka sana Sasa zamu yako Idda alishazoea kaolewa na Adamu wana maisha safi wamezaa Watoto wanafurha ya kutosha maisha Yao mazuri,maumivu ya matendo yako yalishakwisha na SASA NI ZAMU YAKO........pole sana Mdogo wangu Jide........
 

Nasikitika kumaliza kusoma post hii, natamani engeendelea! Hatariii
 

Sababu ya mm.kumuongelea yeye ni hiyo ya kutaka tuamini she's innocent ktk hili......huwezi panda miiba utarajie iote nanasi..
Gardner simuongelei coz jide knew kila kitu abt mitabia ya Gardner,ila akaamua tu kuforce mahusiano na hatimaye ndoa,huku amkimfanyia vituko mwanamke mwenzake(kweli adui ya mwanamke ni mwanamke mwenzake)
hicho tu.
 
Hongera sana jide, maana kama unaishi na Mume ambaye ni Malaya mwisho atakuuwa kwa ukimwi. Bora nusu shari
 
Wasiwasi wangu ni nyie wanawake watarajiwa mnajifunza nini?

Wanawake watarajiwa wanajifunza kuwa wakichoka hakuna haja ya kupigishana kelele kubeba vitu hapana ,Ni kwenda tu kazini na hurudi tena na simu unamblock maisha yanaendelea
 
Wanawake watarajiwa wanajifunza kuwa wakichoka hakuna haja ya kupigishana kelele kubeba vitu hapana ,Ni kwenda tu kazini na hurudi tena na simu unamblock maisha yanaendelea

Haaaaaaaa kwani na wewe ni mwanamke mbona umetusemea hivyo lol
 
daah yaani nilivyokuwaga nawaona kwenye diary nlidhani wanafuraha....kumbe.......

Huku Flora...huku Jide

Nadhani kuna haja hii taasisi ya ndoa iandaliwe mtaala chuo kikuu...wanaohitimu tu ndio waingie.....muda si mrefu tutamsikia na yule binti mwenye Quarter Faraja naye anamwaga ya kwake...."yaani nimeteseka na yule baba mpaka yamenifika kooni"
 
Wanawake watarajiwa wanajifunza kuwa wakichoka hakuna haja ya kupigishana kelele kubeba vitu hapana ,Ni kwenda tu kazini na hurudi tena na simu unamblock maisha yanaendelea

Mawasiliano yanakuwa kupitia IJUMAA,KIU,AMANI,FACE BOOK,INSTAGRAM,WHATUP,JF,TANGO ETC SIO?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…