Exclusive: Jay Dee afunguka, atoa sababu za kuitosa ndoa yake

Exclusive: Jay Dee afunguka, atoa sababu za kuitosa ndoa yake

Yaani walioko ndani wanataka kutoka.., tulioko nje tunataka kuingia..
sikutaka kuquot hapo juu kwenye maelzo yako nakumbuka miaka hiyo ilisemekana Gadner alikua na mke sijui kama ilikua kweli au udaku. Yalisemwa meengi kuwa Gadner aliacha mkewe kisa JD
 
Gadner ana mapungufu yake, lakini kuishi na mwanamke kama Jide nayo inahitaji kipaji,mwanamke hajui kujishusha anapenda maugomvi angalia list ya aliogombana nao Clouds, Shigongo,FA, Matonya unaweza ukapata picha ni mwanamke wa aina gani. Nadhani Gadner alikuwa mtumwa ndani ya ndoa yao.

Pamoja na hayo kumpiga mwanamke bado sijuelewa kabisa naona ni udhaifu mkubwa ..
 
Kumseduce mume wa mwenzako ni kumpora mwenzako pia.....I guess maana ya kupora au kuiba wewe ndo umeielewa hiyo ya furushi tuu???

Ulikuwapo wakati Jide anamseduce Gardner? Kwann siyo Gardner ndiye aliyemseduce Jide? Tena Gardner ndiye wa kupaswa kulaumiwa! Si muaminifu ni cheater & a liar! Alijua wazi ameoa na sheria inamfunga kwa mwanamke mmoja! Alianzaje kutoka na kuanza kutongoza wanawake wengine???
 
NO: 10

SWALI: Tunasikia umeachana na mume ni kweli au uzushi?

JIBU : Hatujaachana niliamua kumuacha

SWALI: Kwanini umeachana/umemuacha mume?

JIBU : Nimemuacha kutokana na kuwa Ndoa inatakiwa iwe na maelewano, furaha, amani na upendo, ila kwa bahati mbaya vyote hivyo havikuwepo, sikuwa tayari kuendelea kuishi kwa maumivu huku niki pretend ili kuiridhisha jamii.

SWALI: Huoni kama umejishushia heshma kuachana na mume?

JIBU : Sioni hivyo, ila naona nilikuwa najishushia heshima zaidi kuishi na mume asie na heshima, anaeweza kutongoza na kushika wanawake makalio wakati mi niko jukwaani naimba. Kuwapa mademu magari yangu waendeshe na kuyagonga wakati niko safarini.

Ukiachilia mbali vipigo. Kutembea na wahudumu wa restaurant yangu. Ushahidi ninao; niliwahi mkuta anawashika mapaja na akakiri kosa. Bado kupigana na kuwatusi wateja pia. Kifupi ilikuwa ni ndoa ya mateso!

SWALI: Baada ya kuachana unategemea kuolewa tena?

JIBU : Ni mapema kujihakikishia uolewaji mwingine, ila haimaanishi kuwa sitopenda tena. Nahitaji kuwa makini zaidi Kuchagua mtu sahihi wa kumpa moyo wangu.

SWALI: Kwanini usirudiane na mumeo?

JIBU : Siwezi kurudi nyuma tena, huwa nina misimamo thabiti. Mpaka kuamua kuondoka na uvumilivu nilionao mjue ni maji ya shingo. When i say never, I mean Never.

SWALI: Uliwezaje kuishi na mume mlevi namna ile?

JIBU : Nilidhani angebadilika, so nilikuwa natoa nafasi. Iliposhindikana nikaona isiwe tabu, kila mtu na aubebe mzigo wake. Ukizingatia ananizidi umri miaka mingi, alitakiwa yeye anielekeze zaidi kuliko mimi kumuelekeza maisha mtu mzima.

SWALI: Uliwezaje kuondoka?

JIBU : Nilipoamua kuwa na iwe basi, Nilitoka bila kubeba kitu. Nikasafiri kwenda USA, nikakaa huko mwezi mzima ku refresh na kujipima kama kweli ntaweza ku move on? Niliporudi Tanzania sikukanyaga tena nyumbani, mpaka muda huu nnapo type na ku post haya majibu. Kwa ki fupi ni kuwa nili ondoka bila kuaga, sikuona sababu ya kuaga.

Asanteni jamani, nafikiri nimejibu yote.

h stor ngebalance kama tungepata the other sde of the stoe, gadna nae aseme yake, may be jde alkua n sababu ya gadna kuchepuka kas hhcho au kwa namna moja ama nyngne alchanga kutokumarka kwa ndoa yake, unajua ndoa na mambo meng sana na l kuelewana n lazma wote mjshushe regardless nan kamzd mwenze ur,kpato, elmu,nk anyways asante kwa ubuyu
 
This has nothing to do with media love bali hii ni hali halisi ya ndoa nyingi za Waafrika ni za kinafiki,maigizo na kiunafiki hata kama uonekani kwenye media unapo ingia kwenye ndoa lazima uwe mnafiki,muigizaji na mvumilivu ndio utaweza kudumu japo hata miaka 11 kabla ujamwaga manyanga.

Yaani ni kweli kabisa unafiki ndiyo motto katika ndoa nyingi! Kwa nje unaweza kuona kama ziko sawa lakini ndani kunawaka moto! Yaani lawyer kula likes mingimingi!
 
pole jide. kwanza ni uvumilivu wa hali ya juu na inaonesha dhahiri Gadna ana tabia moja chafu sana adi kufikia kushika watu makalio wakati mkewe anasaka ugali duu hapo Jide alidharaulika sana na huyu jamaa na asipoangalia ataishia pabaya huyu mshkaji.
 
sikutaka kuquot hapo juu kwenye maelzo yako nakumbuka miaka hiyo ilisemekana Gadner alikua na mke sijui kama ilikua kweli au udaku. Yalisemwa meengi kuwa Gadner aliacha mkewe kisa JD

Yeah alikua na mke huko Mwanza wamezaa nae mtoto mmoja ni kweli kabisa... alivyokuja Dar akawa na mtoto Fauzia.. baadae Jide ko mpambano bado ulikuwepo kati ya baby mama wa Gardner na Jide mwenyewe...
 
h stor ngebalance kama tungepata the other sde of the stoe, gadna nae aseme yake, may be jde alkua n sababu ya gadna kuchepuka kas hhcho au kwa namna moja ama nyngne alchanga kutokumarka kwa ndoa yake, unajua ndoa na mambo meng sana na l kuelewana n lazma wote mjshushe regardless nan kamzd mwenze ur,kpato, elmu,nk anyways asante kwa ubuyu

Haaaaa my dear leo umechapia sehem nyingi kuandika Lols..

Kuna the other side of story kutoka kwa G.. maana hauwezi kusema Jay D ni saint kabisa katika ndoa na Gardner ndio mbaya completely.... so we are missing another side of the coin
 
Matokeo ya kutumia pesa kupata wanaume ndo haya. Gadna roho yake ilikuwa kwa Fauzia, secretary wa
Joseph Kusaga. Gadna pale alikuwa kafa kaoza and it was real love sababu Gadna hakuwa na kitu na
Fauzia alikuwa kasecretary tu.

Akaja Jide na mihela yake pakawa hapakaliki. Gadna akamwacha Fauzia akaenda kwa jide coz of money but
after few months akaona hawezi ishi bila Fauzia akarudi tena kwa Fauzia
wakaendelea na mapenzi yao ya kimaskini.

After few months akaona mapenzi bila hela sio matamu sana akaona bora aende kwenye hela akarudi tena kwa Jide.

Hapa naongelea around 2002 hivi jamani.
Clouds fm palikuwa hapakaliki ni machozi na ngumi tu. Jide alikuwa akimuona Gadna na fauzia analia mpaka kamasi zinamtoka tena mbele
za watu na akipata mwanya
anamrukia Fauzia anamchapa kama kamzaa kisa Gadna.

Gadna alikuwa anashindwa kuwa na uamuzi maana
one side kuna pesa, the other side ndo roho yake ilipo. Kuna siku nakumbuka enzi za Blue palms Jide alimkuta Gadna na Fauzi hapo, Gadna akawa anajifanya kama hamuoni Jide
vile yupo busy na malovey dovey na Fauzia. Jide aliangua kilio mbele za watu kama kafiwa tena kipindi hiko ndio video ya machozi aliyo act
Frank Gonga imetoka.
akawa anamtuliza Jide asianzishe vagi, for some reason Jide akamsilikiza Frank sababu ni Mkurya mwenzie. Jide kateseka na Gadna
even before ndoa,

toka wanadate ilikuwa ni relationship ya mateso ila
aliamua kung’ang’ana na kumuhonga Gadna. Like always, in the end money
won and Gadna married JIDE.
Problem is he never fell in love with her alikuwa pale kimaslahi na alikuwa anawaambia watu hana stimu kabisa na Jide ndo maana alikuwa anatia tia nje kila siku.


Lesson to learn today: money cant buy you love. Happy Valentines wana Jf

Happy valentine to you....
Nimeelewa aisseh, kweli life is all about pretending
 
Naona hii vita karibia inaanza upya G anauliza kama amjibu jide au lah! Very interesting!
 
Unapenda kusikia upande wa pili? G anauliza amjibu huyu anaye jiona malaika?

mh makubwa!!! kaulizia wapi tena? anyamaze tu maana wataonekana wote hawana akili. Mi naamini wote wana matatizo na ni busara pia kukaa kimya. Wengine tukisema yaliyomo ndani ya ndoa zetu!!! Jide na Gadner mbona watajiona wao wana afadhari.
 
mh makubwa!!! kaulizia wapi tena? anyamaze tu maana wataonekana wote hawana akili. Mi naamini wote wana matatizo na ni busara pia kukaa kimya. Wengine tukisema yaliyomo ndani ya ndoa zetu!!! Jide na Gadner mbona watajiona wao wana afadhari.

Yaa kauliza kuwa amjibu huyu anaye jifanya malaika aliye kosewa? Ningekuwa G ninge kaa kimya kabisa kujibishana na mwanamke tena kama Jide ni kama vita tuu! Maana hayato kwisha leo wala kesho akianza kumjibu!Naamini jide si malaika na yeye ana makosa yake lakini kujibishana nae ni kupoteza muda. 1423931787734.jpg
Jionee hapa!
Cc.
Heaven on Earth
warumi
Mtende
mwallu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom