Exclusive: Jay Dee afunguka, atoa sababu za kuitosa ndoa yake

Exclusive: Jay Dee afunguka, atoa sababu za kuitosa ndoa yake

Yaa kauliza kuwa amjibu huyu anaye jifanya malaika aliye kosewa? Ningekuwa G ninge kaa kimya kabisa kujibishana na mwanamke tena kama Jide ni kama vita tuu! Maana hayato kwisha leo wala kesho akianza kumjibu!Naamini jide si malaika na yeye ana makosa yake lakini kujibishana nae ni kupoteza muda.View attachment 226884
Jionee hapa!
Cc.
Heaven on Earth
warumi
Mtende
mwallu

Haaaaaaaaaaa ngoja nikacheki mwenyewe..... amjibu tuone another side ya stori though swala la ukitombi inajulikana tu ni kitombi....
 
Last edited by a moderator:
Pamoja na yote mabaya ya Gardner aliyoyaeleza Jide, hili suala la kupiga mwanamke ni la kishamba sana! Sikuwa nimefikiri kwamba mpaka leo hii mjini kuna mwanaume anapiga mwanamke aisee!!!! Kumbe jamaa ni mshamba hivyo?!!!

Wewe umeamua kuamini tu kuwa ni kweli Gardner alikuwa akimpiga huyo mwanamke?

Hujawaza hata kidogo huenda labda huyo mwanamke kwa sababu za kinyongo anataka tu kumchafua Gardner kwa kumpaka matope?

Kuna ushahidi gani kuwa kweli Gardner alikuwa akimpiga? Kuna taarifa za polisi?

Yeye huyo mwanamke hakuwahi kumpiga Gardner?

Na la muhimu zaidi ni kwamba hii habari haina uwiano mzuri kwa sababu ni ya upande mmoja tu.

Hivyo si vyema kurukia kuhitimisha kuwa Gardner ni mtu mbaya au sijui ni mshamba wakati bado hatujasikia maelezo ya upande wake.

Au naye keshaongea tayari?
 
Makubwa,naona movie ndio inaanza. Gadner anyamaze tu ni utoto kuanza kutoleana siri za ndani. Unajua wanawake ndio wanapenda kuropoka ovyo bali wanaume si watu wa kuongea ovyo.
 
Makubwa,naona movie ndio inaanza. Gadner anyamaze tu ni utoto kuanza kutoleana siri za ndani. Unajua wanawake ndio wanapenda kuropoka ovyo bali wanaume si watu wa kuongea ovyo.

Kwa nini anyamaze tu ilhali kuna watu wanaamini kabisa alichokiongea huyo mwanamke kuwa ndo ukweli wenyewe wakati huenda si kila kitu alichokisema ni cha kweli?
 
Pamoja na yote mabaya ya Gardner aliyoyaeleza Jide, hili suala la kupiga mwanamke ni la kishamba sana! Sikuwa nimefikiri kwamba mpaka leo hii mjini kuna mwanaume anapiga mwanamke aisee!!!! Kumbe jamaa ni mshamba hivyo?!!!

Kaka..wanaopiga wapenzi wao ni wengi. ..wasomi kwa mbumbumbu....wa mjini na wa kijijini. .yaani ni tabu tupu
 
Shkamoo zake Jide...hv hata ile Siwema alimwimbia Gadna nini 😷😷😷
 
Yaa kauliza kuwa amjibu huyu anaye jifanya malaika aliye kosewa? Ningekuwa G ninge kaa kimya kabisa kujibishana na mwanamke tena kama Jide ni kama vita tuu! Maana hayato kwisha leo wala kesho akianza kumjibu!Naamini jide si malaika na yeye ana makosa yake lakini kujibishana nae ni kupoteza muda.View attachment 226884
Jionee hapa!
Cc.
Heaven on Earth
warumi
Mtende
mwallu

mimi sioni tija ya hawa jamaa kujibzana mtandaon,kama wameachacha au kama mmoja kaachwa basi kila mtu amtake mwenzake heri masha yaendelee,
 
Haaaaa my dear leo umechapia sehem nyingi kuandika Lols..

Kuna the other side of story kutoka kwa G.. maana hauwezi kusema Jay D ni saint kabisa katika ndoa na Gardner ndio mbaya completely.... so we are missing another side of the coin

yani shoga angu nmesoma hii habari nikaona nisptwe, sasa nlikua naandka huku namlsha bebi, mimi nadhani its not right kwa jide kuanika mapungufu ya ndoa yao hadharani, kama wameachana basi angekaa kimya maisha yaendelee
 
Ulikuwapo wakati Jide anamseduce Gardner? Kwann siyo Gardner ndiye aliyemseduce Jide? Tena Gardner ndiye wa kupaswa kulaumiwa! Si muaminifu ni cheater & a liar! Alijua wazi ameoa na sheria inamfunga kwa mwanamke mmoja! Alianzaje kutoka na kuanza kutongoza wanawake wengine???

Yaani wewe bado huelewi maybe ukicalm down...kwa akili yako unadhani jide hakuzijua tabia za G???? Yet she forced it...kiufupi my point ipoo hivi,jide aliuficha moto kwa kuukalia akitegemea nguo hazitoungua,zimeungua ndio anakimbilia sympathy ya kijinga kama hio....
Mwisho nikuulize ewee Dada,unaweza mkubali mwanaume ambae ameoa akadai atamwacha mkewe ili akuoe wewe????
 
Na kule kwa mke wa kwanza kilimtoa nini? Mbona yule alizaa na akamuacha?
Kifupi ni kunguru asiyeweza kufugwa!

Lakini bado akadhani anaweza kumfuga....yaani bado hupati kitu hapo????
 
wewe nawe umelikomalia ishu ya jaydee,eti amekuwa zaidi ya mume ...umeambiwa alikuwa anampiga,anamuonyesha vituko vya kipuuzi wazi wazi......bado unataka dada wa watu aendelee kusuffer kisaikolojia,kulia kila siku kwa kuonyeshwa hajaliwi/hapendwi............ bado mnaexpect mtu aendelee kuishi ndoani kuwaridhisha nyie, na akitoka msione wote wako rensponsible kwa ndoa kuvunjika, mnamnyooshea mtu mmoja kidole,........SAY NO TO UNHAPPY MARRIAGE....:embarrassed1:

Ya Jide unayajua?? yeye kama kamuacha mbona ndio anarudi kulilalia mitandaoni, ye si alikuwa right kwa kila kitu unatua mzigo lakini bado mzigo unakusumbua lazima kuna tatizo.
 
Wewe umeamua kuamini tu kuwa ni kweli Gardner alikuwa akimpiga huyo mwanamke?

Hujawaza hata kidogo huenda labda huyo mwanamke kwa sababu za kinyongo anataka tu kumchafua Gardner kwa kumpaka matope?

Kuna ushahidi gani kuwa kweli Gardner alikuwa akimpiga? Kuna taarifa za polisi?

Yeye huyo mwanamke hakuwahi kumpiga Gardner?

Na la muhimu zaidi ni kwamba hii habari haina uwiano mzuri kwa sababu ni ya upande mmoja tu.

Hivyo si vyema kurukia kuhitimisha kuwa Gardner ni mtu mbaya au sijui ni mshamba wakati bado hatujasikia maelezo ya upande wake.

Au naye keshaongea tayari?

Asante mdau...
Watu hapa kwa kuwa wanajua mapungufu ya G basi ndo wamegeuka mahakama....
Kuyajua mapungufu ya G na kutoyafahamu ya jide hakutakiwi kuwapa sababu ya kuelemea upande mmoja.
 
Ya Jide unayajua?? yeye kama kamuacha mbona ndio anarudi kulilalia mitandaoni, ye si alikuwa right kwa kila kitu unatua mzigo lakini bado mzigo unakusumbua lazima kuna tatizo.

Yaani wengi bado hawastuki sijui kwann...
 
Matokeo ya kutumia pesa kupata wanaume ndo haya. Gadna roho yake ilikuwa kwa Fauzia, secretary wa
Joseph Kusaga. Gadna pale alikuwa kafa kaoza and it was real love sababu Gadna hakuwa na kitu na
Fauzia alikuwa kasecretary tu.

Akaja Jide na mihela yake pakawa hapakaliki. Gadna akamwacha Fauzia akaenda kwa jide coz of money but
after few months akaona hawezi ishi bila Fauzia akarudi tena kwa Fauzia
wakaendelea na mapenzi yao ya kimaskini.

After few months akaona mapenzi bila hela sio matamu sana akaona bora aende kwenye hela akarudi tena kwa Jide.

Hapa naongelea around 2002 hivi jamani.
Clouds fm palikuwa hapakaliki ni machozi na ngumi tu. Jide alikuwa akimuona Gadna na fauzia analia mpaka kamasi zinamtoka tena mbele
za watu na akipata mwanya
anamrukia Fauzia anamchapa kama kamzaa kisa Gadna.

Gadna alikuwa anashindwa kuwa na uamuzi maana
one side kuna pesa, the other side ndo roho yake ilipo. Kuna siku nakumbuka enzi za Blue palms Jide alimkuta Gadna na Fauzi hapo, Gadna akawa anajifanya kama hamuoni Jide
vile yupo busy na malovey dovey na Fauzia. Jide aliangua kilio mbele za watu kama kafiwa tena kipindi hiko ndio video ya machozi aliyo act
Frank Gonga imetoka.
akawa anamtuliza Jide asianzishe vagi, for some reason Jide akamsilikiza Frank sababu ni Mkurya mwenzie. Jide kateseka na Gadna
even before ndoa,

toka wanadate ilikuwa ni relationship ya mateso ila
aliamua kung’ang’ana na kumuhonga Gadna. Like always, in the end money
won and Gadna married JIDE.
Problem is he never fell in love with her alikuwa pale kimaslahi na alikuwa anawaambia watu hana stimu kabisa na Jide ndo maana alikuwa anatia tia nje kila siku.

Lesson to learn today: money cant buy you love. Happy Valentines wana Jf

sorry hyo fauza ndyo yule wa sugu? halafu niliskiaga frank gonga ana skendo ya ukameruni ni kweli????//////
 
Jide & Flora Mbasha!!

v/s

Gardner & Emmanuel Mbasha!!
 
sorry hyo fauza ndyo yule wa sugu? halafu niliskiaga frank gonga ana skendo ya ukameruni ni kweli????//////

Hapana sio wa Sugu ni Fauzia mwingine kabisa..

Hizo za Gonga kuwa shoga ndio nazisikia kwako... so sina ninalolijua hapo
 
NO: 10

SWALI: Tunasikia umeachana na mume ni kweli au uzushi?

JIBU : Hatujaachana niliamua kumuacha

SWALI: Kwanini umeachana/umemuacha mume?

JIBU : Nimemuacha kutokana na kuwa Ndoa inatakiwa iwe na maelewano, furaha, amani na upendo, ila kwa bahati mbaya vyote hivyo havikuwepo, sikuwa tayari kuendelea kuishi kwa maumivu huku niki pretend ili kuiridhisha jamii.

SWALI: Huoni kama umejishushia heshma kuachana na mume?

JIBU : Sioni hivyo, ila naona nilikuwa najishushia heshima zaidi kuishi na mume asie na heshima, anaeweza kutongoza na kushika wanawake makalio wakati mi niko jukwaani naimba. Kuwapa mademu magari yangu waendeshe na kuyagonga wakati niko safarini.

Ukiachilia mbali vipigo. Kutembea na wahudumu wa restaurant yangu. Ushahidi ninao; niliwahi mkuta anawashika mapaja na akakiri kosa. Bado kupigana na kuwatusi wateja pia. Kifupi ilikuwa ni ndoa ya mateso!

SWALI: Baada ya kuachana unategemea kuolewa tena?

JIBU : Ni mapema kujihakikishia uolewaji mwingine, ila haimaanishi kuwa sitopenda tena. Nahitaji kuwa makini zaidi Kuchagua mtu sahihi wa kumpa moyo wangu.

SWALI: Kwanini usirudiane na mumeo?

JIBU : Siwezi kurudi nyuma tena, huwa nina misimamo thabiti. Mpaka kuamua kuondoka na uvumilivu nilionao mjue ni maji ya shingo. When i say never, I mean Never.

SWALI: Uliwezaje kuishi na mume mlevi namna ile?

JIBU : Nilidhani angebadilika, so nilikuwa natoa nafasi. Iliposhindikana nikaona isiwe tabu, kila mtu na aubebe mzigo wake. Ukizingatia ananizidi umri miaka mingi, alitakiwa yeye anielekeze zaidi kuliko mimi kumuelekeza maisha mtu mzima.

SWALI: Uliwezaje kuondoka?

JIBU : Nilipoamua kuwa na iwe basi, Nilitoka bila kubeba kitu. Nikasafiri kwenda USA, nikakaa huko mwezi mzima ku refresh na kujipima kama kweli ntaweza ku move on? Niliporudi Tanzania sikukanyaga tena nyumbani, mpaka muda huu nnapo type na ku post haya majibu. Kwa ki fupi ni kuwa nili ondoka bila kuaga, sikuona sababu ya kuaga.

Asanteni jamani, nafikiri nimejibu yote.
VERY HARD LOOKING.Ana bahati alimpata mtu wakumwangalia sura Yake kila siku na kumdanganya " your beautiful".ana sura ya binti chura
 
Sasa wewe umemchoka komando wetu mkuu???
Nivizuri kusema ukweli jAYDE anasura mbaya na mwanaume yoyote atakaempata atakuwa analiwa pesa zake.wanaume wakitanzania wanavyopenda wanawake wazuri .sura Yake Kama WASHAWASHA
 
Sioni cha ajabu sana alichofanya G ambacho wanaume wengine hatufanyi au wazee wetu hawakufanya lakini maisha yanaendelea.

Kama namuona vile commando.

Kumbe mnajijua na mnafanyaga kusudi eeh...?
Bora yeye kaondoka, wanawake wengine wakichoka vituko wanaamua moja tu.
Fanya vurugu zako, siku akichoka unapelekwa kwenye nyumba ya milele.
 
Back
Top Bottom