Wanabodi,
Kusema kweli inabidi tuzame zaidi ktk kufikiria hili na wala sii non issue kabisa..Hali ya chumi duniani ni mbaya na tupende tusipende kuna kimbunga kinakuja..
Tatizo la wazo zima la Mkutano huu wa G5 ambazo ni nchi maskini kuliko zote dunani, una chemsha bongo zangu kujaribu kufahamu watazungumzia kitu gani..
Pengine JK anataka kuwauliza Kenya na Uganda waliweza vipi kupita kipindi kigumu cha mwaka 1982 ingawa sababu za recession hizi mbili hazifanani?
Pili, laukama kuna nchi tajiri zitaalikwa ktk mazungumzo hayo na tumika baadhi ya mazungumzo ya IMF ktk kujitangaza labda inaweza kusaidia, lakini sisi maskini kukutana wakati hatuna ndururu mfukoni, kula yetu shida, kila mtu anatazama tumbo lake na kusubiri nani ata cover the bill ni kujitafutia matatizo tu..
Kama walivyosema wanabodi wengine huko nyuma,
Ni muhimu kwa Tanzania leo hii kutazama matatizo yetu na jinsi gani tumejiandaa sisi wenyewe kabla ya kuwakilisha hoja nzima..Kenya haiwezi kutusaidia wala hakuna maandalizi yoyote yanayoweza kufanywa na nchi zetu kwa pamoja ktk ku create ajira ambazo zinapotea kwa kasi kubwa..Chumi zam nchi tajiri zinamilikiwa na watu wachache sana lakini wanaozalisha ni zaidi ya asilimia 95..Hivyo kukosekana kwa kazi ni pigo kubwa sana ktk uchumi wao, mzunguko wa fedha ktk asilimia hiyo 95 ukiyumba tu basi nchi hizo huteteleka kiuchumi, wakati sisi wamiliki wa mali zetu ni wageni na wafanyakazi ni aslimia chini ya 50 miaka nenda miaka rudi.. As a fact, serikali (huduma) zetu zinaajiri over 60 ya ajira zote za kila nchi..Tutazalisha wapi na lini?..Mungu ndiye anajua.
Haya ndio maswali ya kujiuliza sisi wenyewe na kuutazama mzungumko mzima kwa kila nchi..kila nchi ni lazima itazame mzunguko wake unaanzia wapi na kukwazwa wapi ili kupata kuelewa wapi utakapo anzia..laa sivyo ni kujaribu kuunganisha mizunguko mitano ya Olyimpic rings in a real world!.. kweli tunaweza au mazingaombwe yenyewe hayo!
Leo hii mkutano wa G5 hata kama ni kuvutia nchi tajiri ktk Utalii au uwekezaji tutafanya nini kwa pamoja ilkiwa hatuna ushirikiano toka mwanzo..kila nchi inajiendesha kivyake tena tunagombania wateja na sii ruksa wala rahisi kwa shirika la Kenya kufanya biashara Tanzania..Utafikiria maskini ombaomba pale msikitini wa Ujumaa baada ya sala..
Soko la mali zetu limeporomoka kutokana na ughali wa maisha nchini..Pamoja na umaskini wetu mali zinazotengenezwa nchini ni ghali mara 10 ya ile inayotoka China, Taiwan na India..Sisi tumekuwa Obsessed na mali za nje kiasi tumetupa hata majembe..tuna consume 90 % ya junk products..mpango ni misheni town tu, mikataba feki, kusaka madini, kununua mitumba hata chakula na madawa leo tunaagiza toka nje tena feki..toka mchele hadi chunvi tunaagiza toka nje ya Uvinza haifai tena..Sii Kenya wala Tanzania sote ni importers wakubwa toka tunaamka asubuhi hadi tunalala usiku asilimia 80 ya matumizi yetu ni mali toka nje..sasa hapa tutajadiliana kitu gani ikiwa sisi ndio soko la mali mbovu na kwa kiasi tumechangia kupandisha bei za mali nyingi za nje kinyume cha actual value ya vitu hivyo.
Kama walivyosema wengine mikutano kama hii kwa wakati huu haina manufaa hata kidogo. Ni muhimu tutafute mbinu za kuinua upya uchumi wetu ktk sekta ambazo tunafahamu zinaongeza kazi na mavuno yake yatakuwa na manufaa kwetu baadaye..NGUVU za UMEME, MAJI, KILIMO cha Umwagiliaji, UFUGAJI, UVUVI, UTALII wa kisasa na mikataba ya Madini ni sehemu ambazo zinatakiwa kupewa nafasi ya kwanza ktk mazungumzo yetu ya ndani..