1. Mh Lissu unaweza ukaelezea ni kwanini uchaguzi wa mwaka huu (2020) umeuita kama uchaguzi wa kufa na kupona ?
2. Moja kati ya nyimbo za kampeni zako unasema "Lissu tuvushe" kwa nadharia hiyo hiyo kwanini Lissu na sio Mtetezi wa Wanyonge John Pombe Magufuli?
3. Kauli ya "Lissu ni kibaraka wa mabeberu" kauli hii unaitafsiri vipi kwako kama mgombea wa CHADEMA na mgombea katika taifa lenye rasirimali nyingi kama Tanzania?
4. Kauli ya "CCM= Uchaguzi huu ni mwepesi mno kutokana na mgombea wetu alivyoweza kusimamia vyema rasirimali za taifa, kajenga tanzania ya viwanda , katengeneza ajira kedekede, kajenga uwajibikaji ndani ya serikali" kauli ya CHADEMA= Uchaguzi huu ni mwepesi mno kutokana na sera zetu za uhuru, haki na maemdeleo ya watu.....kauli hizi mbili tofauti zina maana gani kwako kama mgombea dhidi ya mpinzani wako wa CCM?