Mheshiwa mimi nashauri kwakuwa mwaka 2015 kwa mujibu wa tume CCM ilipata kura nyingi kanda ya ziwa. Nakuomba uweke nguvu sana maeneo hayo.
Pili, haya maeneo yote ambayo JPM hataweza kufika jitahidi ufike uyakamate kwani njia nyeupe kwenye maeneo hayo.
Halafu weka nguvu uchukue Morogoro, Zanzibar, Lindi na Mtwara , Mara,Pwani na Dar , Arusha, Singida, Kilimanjaro , Kigoma,Mbeya na Iringa.
Yale maeneo ambayo mlipoteza 2015 jitahidi ufike mwenyewe.
Hapo itabakia Tanga , Dodoma na Tabora ambazo naamini mtaziwekea mpango wake maalum.
Ningependa pia kuona video fupi za kusambaza social media uongee na wapiga kura zikiendana na count down ya kuelekea kwenye uchaguzi hadi siku moja kabla.
Mwisho naomba mtoe list ya wagombea ubunge wote wa CDM nchi nzima wapangwe kimkoa isambazwe kwenye mitandao ili wajulikane. Mkiweza iwe printed hard copy watu wapewe especially mikoani.
Mwisho naomba tujitahidi kuchangia kampeni ili Mheshimiwa afike maeneo mengi zaidi.
Ahsante.