Kwanza, hongera kwa kampeni zako ambazo kweli zinamwitikio mkubwa kuliko mgombea yeyote.
Pili, pole ni mbinu chafu zinazofanywa na dola kukukwamisha katika kampeni zako, lakini hata hivyo naamini ukisimama kupiga kampeni leo, bado utapata kura za tufani kwa kuwa watanzania wameikataa CCM kwa nguvu kwa mateso ya kila aina tupitiayo.
Maswali yangu kwako ni haya:-
1. Je, kama utakuwa umeshinda, alafu usitangazwe, utachukua hatua gani? Je, hutatuacha solemba kama Lowassa aliyeshindwa kutetea haki yetu ya kupigania ushindi?
2. Tume ya Uchaguzi imekataza Mawakala kuingia na simu vituoni. Je, hii haitaathiri ushahidi wa matokeo?
3. Tumesikia fununu kuwa timu ileile ya Masaki iliyochakachua matokeo 2015 kabla ya kuwasilishwa Tume kwamba ipo Dodoma. Je, kama chama mmefuatilia hili?
Nakutakia kila la heri, tuko nyuma yako.