Asante sana kwa kutoa fursa hii Jamii Forums - Siasa.
Mimi ninafarijika sana na dhanira ya serikali ya CHADEMA ya kurejesha mchakato wa KATIBA MPYA. Kwa sababu matatizo mengi tunayokabiliana nayo kama taifa ama jamii - hususan ambayo yamejidhihirisha waziwazi katika miaka hii mitano iliyopita - ni ya kimfumo (structural). Kupatikana kwa Katiba Mpya sio tu itakuwa ni sisi kujitendea haki, bali pia tutakuwa tunawatendea haki watoto wetu, wajukuu wetu, na vitukuu wetu!
SWALI 1: Mojawapo ya UFISADI (kleptocracy) mkubwa ulioratibiwa na serikali za CCM ni malipo ya kufuru kwa wabunge. Ndio maana haishangazi viongozi wastaafu wanafanya kila liwezekanalo kuwapenyeza wake na watoto wao Bungeni. Je, serikali ya CHADEMA itakuwa tayari kufutilia mbali UFISADI wa aina hii? Je, unaweza kulidokeza tatizo hili katika kampeni zako za sasa?
SWALI 2: Wapinzani/washindani wako wameanza kupiga propoganda za kupotosha dhana ya 'maendeleo ya watu'. Je, unaweza kujitahidi kuifafanua kwa kutumia mifano kuntu kama ulivyofanya leo (10/14) katika mkutano wako wa Ukerewe kwamba tunaposema maendeleo ya watu haina maana hatupangi maendeleo ya vitu. Tunapanga maendeleoa ya watu kwa vipaumbele. Badala ya kujenfa daraja la Salender au uwanja wa ndege kijijini kwa Rais Lissu, tunajenga daraja la Kisorya au tunaboresha miundombinu ya Jangwani ili kukabiliana na tatizo la mafuriko linalojitokeza kila msimu wa mvua tokea tupate uhuru!
SWALI 3: Mimi ni m-diaspora. Je, serikali ya CHADEMA ina mpango gani kulinda haki za kuzaliwa, za kibinadamu na za kikatiba za waDiaspora?
SWALI 4: M-diaspora akitaka kuchangia mafuta na maji kufanikisha kampeni zako, atume wapi mchango huo?