Kadri mambo yanavyokwenda,nadhani JK na EL watageuka kuwa maadui kama paka na panya.Wahenga walisema USHIRIKA WA WACHAWI HAUDUMU
Na hilo ndilo hasa!
Lakini la kufurahisha ni kwamba hao mafisadi waliobaki humo serikalini sasa watakuwa wanajiuliza mara mbilimbili kabla ya kufanya uhujumu wao. Mosi, kwa kuwaogopa mafisadi waliotupwa nje, kwani wanazijua njia zao zote; pili, hao walio ndani kwa miaka hii mitatu iliyosalia kabla ya uchaguzi hakuna atakayethubutu kuwaibia mali wananchi, unless kama yeye ni 'professional' thief. Sana sana watabaki kubembelezea vinafasi vyao ili wapite tena hapo 2010, na ulaji wa nguvu uanze upya.