يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَسْخَرْ قَوْمٌ مِّن قَوْمٍ عَسَىٰ أَن يَكُونُوا خَيْرًا مِّنْهُمْ وَلَا نِسَاءٌ مِّن نِّسَاءٍ عَسَىٰ أَن يَكُنَّ خَيْرًا مِّنْهُنَّ ۖ وَلَا تَلْمِزُوا أَنفُسَكُمْ وَلَا تَنَابَزُوا بِالْأَلْقَابِ ۖ بِئْسَ الِاسْمُ الْفُسُوقُ بَعْدَ الْإِيمَانِ ۚ وَمَن لَّمْ يَتُبْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿١١﴾ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اجْتَنِبُوا كَثِيرًا مِّنَ الظَّنِّ إِنَّ بَعْضَ الظَّنِّ إِثْمٌ ۖ وَلَا تَجَسَّسُوا وَلَا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا ۚ أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَن يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيهِ مَيْتًا فَكَرِهْتُمُوهُ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ تَوَّابٌ رَّحِيمٌ ﴿١٢﴾
Enyi mlioamini! Watu (wanaume) wasiwadharau watu (wengineo, kwani) huenda (waliodharauliwa) wakawa bora kuliko wao. Na wala wanawake (wasiwadharau) wanawake (wengineo), huenda (waliodharauliwa) wakawa bora kuliko wao. Na wala msikashifeni, na wala msiitane majina ya utani (mabaya). Uovu ulioje wa jina la ufasiki baada ya iymaan. Na yeyote asiyetubu, basi hao ndio madhalimu. Enyi mlioamini! Jieupusheni sana na dhana, kwani hakika baadhi ya dhana ni dhambi. Na wala msipelelezane, na wala wasisengenyane baadhi yenu wengineo. Je, anapenda mmoja wenu kula nyama ya nduguye aliyekufa? Mkalichukia hilo! Na mcheni Allaah! Hakika Allaah ni Tawwaabur-Rahiym (Mwingi wa kupokea tawbah - Mwenye kurehemu).[2]