*KUELEKEA UCHAGUZI WA KENYA LEO 08/08/2017,NANI ATAIBUKA KIDEDEA KATI YA KENYATTA NA ODINGA*
Na
Abdul Nondo.
Uchaguzi wa kenya umekuwa uchaguzi wenye msisimko na wenye hamasa saana tangu kampeni kuanza hadi kufungwa kwake.
Huu msisimko ni kutokana na uwepo wa ushindani mkubwa wenye kuacha maswali mengi kichwani mwa watu na watu kupata wakati mgumu kutokana ushindani kuwa mkubwa Kati ya pande mbili NASA na JUBILEE PARTY.
NASA yaani NATIONAL SUPER ALLIANCE ni muunganiko (coalition) wa vyama tofauti tofauti vya upinzani, mfano.Aman National Alliance cha Musalia Mudavid, ODM cha Agwambo Raila Jaramog Amolo Odinga, wiper democratic movement cha kalonzo Musyoka,Ford Kenya cha Moses Watenge, na CCM (chama cha mashinan) cha lsaac Ruto.
Jubilee yupo Uhuru Kenyatta na William Rutto, ingawa na Jubilee ni muungano wa chama cha Kenyatta (Kenya alliance party) na William Rutto (united Republic party). Tangu 2016,walipo fanya Coalition ya vyama vyao na kupata Jubilee party.
Hivi ndio vyama vinavyopambana kwa hali ya juu saana, kuelekea katika sanduku la kupiga kura, katika kupiga kura kuna aina tatu za Tabia, na mwenendo wa upigaji kura tunaosoma political science, tunaita *VOTING TREND AND BEHAVIOR*
watu hupiga kura kwa kuchagua njia moja au tabia moja ya upigaji kura kati ya njia Tatu, na zote hutumika kumpa mtu ushindi na kumnyima mwingine.ndizo ambazo pia zitatumika kwa Raia kenya katika kufanya maamuzi.
1 *PARTY IDENTIFICATION MODEL*.
hii ni aina ya upigaji kura ambapo mwananchi ana piga kura kwa kuangalia yupo chama gani, haangalii sera, haangalii mtu, anaangalia chama chake anachokiamini hawa nchini kenya wapo, wapo watakaomchagua mgombea kutoka chama cha jubilee, wapo watakao chagua mgombea kutoka NASA sababu ndani ya muungano kutakuwa na chama chake anachokiamini.watu wa aina hii wengi watapigia NASA, sababu NASA imechukua vyama vingi katika umoja wao Tofauti na JUBILEE ambapo watakaopigia JUBILEE ni JUBILEE TUU, ila NASA anaweza kuwa ni mtu wa aman national alliance, ODM, wiper Democratic movement, Ford kenya ,na CCM (chama cha mashinani.).hivyo kwa aina ya wapiga kura wa Tabia ya aina hii ni faida kubwa kwa NASA.
2 *RATIONAL CHOICE MODEL*
hii ni aina ya upigaji kura ambapo mwananchi anaangalia sera zinazompendeza yeye kutoka kwa mgombea na vipaumbele vyake , bila kujali udini, ukabila, uchama, ukanda, hii nchini Kenya watu watapiga kura kwa kiongozi mwenye sera za kueleweka, mfano. uhuru Kenyatta sasa amekuwa akinadi aliyoyafanya, na ambayo anatarajia kwenda kuyamaliza *Kenyans, give me your votes so that we can go to finish what we have already begun* na mengine mapya anayotarajia kufanya mfano .Elimu bure, NHIF, ulinzi dhidi ya ugaidi ,pia amekuwa akitumia muda kujibu makombora ya viongozi wa NASA dhidi yake ili kujisafisha.
Upande wa Raila odinga, amekuwa akionesha matarajio yake kipi anatarajia kufanya akiwa rais, mfano kufuta karo, kushusha bei ya chakula, kupunguza deni la taifa, pia ODINGA amekuwa mgombea ambaye anapita katika makosa mpinzani wake Kenyatta mfano ,anapinga kupeleka majeshi ya kenya Somalia, mauaji ya Chris msando ambaye alikuwa na msimamo juu kura za electronic, rushwa dhidi ya 1.2 billion katika shirika la taifa la vijana (NYS) na ufisadi wa EUROBOND ,kununua mahindi Mexico yasiofa na kuacha kununua mahindi ya wakenya,kumkosoa kuwa standard gauge railway ulikuwa ni mradi tangu serikali ya mpito ,na yeye akiwa kama waziri mkuu,mauaji ya 2008,kupendelea wa kikuyu.
Hii aina inamfanya mwananchi aangalie sera ipi inafaa ya chama kipi, hivyo kuna watakaopiga kura sababu ya kupendezwa na sera fulani. Aidha ya Kenyatta au odinga ingawa odinga hana histori ya kusema alifanya nini ingawa amewahi hudumu kama waziri mkuu, pia Kenyatta kinachomuumiza ni ahadi ambazo hakuzitekeleza na kasoro zilizojitokeza katika uongozi.
3. *SOCIOLOGICAL MODEL*
hii ni tabia ya upigaji kura ambapo mwananchi mpiga kura, haangalii chama, wala sera ila anaangalia zaidi *ukabila*,ukanda, udini,
Na hii ndio aina ya upigaji kura ulioenea nchini Kenya huwezi kwepa ukabila kenya utakuwa mnafiki.
kenya kuna makabila 43,makabila makubwa ni Kikuyu 22% kabila la Kenyatta, kalenjini 12% la Rutto, viongozi wa Jubilee party, hivyo watapigiwa kura na watu wakabila lao, pia NASA huu muungano umeteka na kujumuisha makabila mengi kupitia viongozi wake tofauti, luo 13% waliokenya watampa odinga, kamba idadi ni 11% ambao watampa kalonzo musyoka, luhya ambao wapo 14% ambao watampa musalia mudavida.na kalenjine ambao wapo 15% ambao watampa isaac RUTO, hizi za kalenjine zitagawanyika na zile za William Rutto.
Na 15% zingine ni za makabila mengine hasa jamii za kiislamu zilizopo mombasa na lamu ambazo kwa umoja zinaonesha kuungamkono NASA sababu ya kumfuata na kushawishika na governor wao HUSSEIN JOHO wa mombasa ambapo amekuwa akisema wa mombasa wametengwa, hivyo NASA kuaminika saana kama mbadala.
Hivyo,kupitia him unaweza ona namna gani hesabu za NASA zipo calculated, ila lazima tukumbuke ingawa twaweza sema kabila hizo mbili sio zaidi ya kabila zote za viongozi walioungana NASA ,ila cha msingi kukitambua ni kuwa kabila hizi mbili KIKUYU na kalenjini ni kabila zenye nguvu, mamlaka, na watu walio katika sekta mbalimbali na ambao wameotamizizi katika serikali kwa muda mrefu.
Ndio makabila mawili ambayo yamekuwa katika uongozi tangu kenya kupata uhuru.
1963-1978 kenya chini ya jomokenyata alikuwa mkikuyu, 1978-2002,daniel arap moi alikuwa mkalenjini, 2002 had 2013 alikuwa mwai kibaki ambaye ni mkikuyu, 2013-2017 ni uhuru Kenyatta ambaye no mkikuyu, hivyo haya makabila ni mawili ila yanaonekana kuwa na kunguvu ya kuota mizizi, linawafanyabiashara wakubwa, watendaji wa serikali, pia jeshi ngazi za juu, na wengi katika maamuzi.
Pia lazima tujue kwa nchi zetu za Afrika kuwa kuna ugumu wa hali ya juu kumtoa mgombea ambaye ni rais anaendelea muhula mwingine huwa kuna ugumu wake lazima tulijue na hilo.
Pia ukanda, imeonesha kuwa NASA imevunja ngome za jubilee party, mfano .kaunti ya meru, bonde la ufa, tharatha nitha, embu, kuwa ni ngome za jubilee ambayo matatizo yao hayajatatuliwa hivyo wamegeuka kusupport NASA ingawa Jubilee wanadai hizo bado ni ngome zao.
Suala ambalo linaonesha kuleta mtafaruku, ni tume ya uchaguzi ya kenya IEBC kutoa taarifa kuwa robo ya vituo havina huduma ya simu ya 3G,na 4G Kuwezesha kutuma matokeo kwa njia ya electronic kwenda kituo cha taifa BOMAS.hivyo wasimamizi na waangalizi watasogea hadi katika maeneo yenye mtandao ili kuyarusha matokeo hayo BOMAS.
vituo ambavyo havina mtandao sababu vipo nje ya miji ni 11,155 Kati ya 40883.nchini .
hii taarifa ameanza pokelewa kwa mitazamo tofauti wengi wakisema ndio njia hizo, zinaanza tumika hivyo uchaguzi huu karata kubwa inaweza angukia katika chama ambacho kina nguvu katika maamuzi ndani ya *SERIKALI*
mungu awabariki wakenya, wafanye uchaguzi kwa amani.
Abdul Nondo.
0659366125
TZ.
Sent using
Jamii Forums mobile app