Exclusive: Wachezaji wa Uganda Cranes Okwi na Murshid wasema akipangwa Mkude katika Kiungo watafungwa Kiurahisi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Ninachokiweka hapa na sehemu tu ya Maongezi yangu ya Kirafiki ambayo huwa nafanya na Wachezaji wengi wa Kiganda hasa hawa wanaocheza hapa Tanzania hasa kutokana na Historia yangu binafsi na hiyo nchi na Waganda kwa ujumla hali ambayo imenifanya niwe Rafiki yao wakiwa hapa Tanzania.

Katika ' Kuchati ' Kwangu na Wachezaji wa Kiganda wanaocheza pia Timu ya Simba akina Emanuel Okwi na Juuko Murshid wameonyesha Kukisifia mno Kikosi cha Taifa Stars na hasa hii ' Morale ' kubwa iliyopo huku wakisema kuwa hiyo Jumapili Kazi wanayo ila wakasema kuwa wanamuomba sana na mno Mwenyezi Mungu kuwa Kiungo Jonas Gerald Mkude ambao Wao wanamuona ndiyo ' Injini ' na ' bora ' kwa sasa nchini Tanzania asipangwe kwani kama akipangwa basi kwa aina ya ' Uchezeshaji ' wake kuna uwezekano mkubwa Wao ( Uganda Cranes ) wakafungwa mengi na Taifa Stars.

" Bother GENTAMYCINE naomba Mungu Mkude wetu huyu asipangwe na aendelee tu Kukaa benchi kwani kwa ninavyomjua na anavyojua Kuchezesha Timu kama akipangwa basi akina Samata, Msuva na Kichuya watatuumiza mapema mno na Waganda tutaumbuka. Tunamuogopa "...maelezo ya Okwi haya.

" Ssebo GENTAMYCINE huna Mganga ili utupeleke Waganda kusudi tumfumbe Macho Kocha Amunike asahau Kumpanga Mkude kwani kama kuna Mtu ambaye endapo akipangwa Siku hiyo anaweza kutibua Shehere yetu ya Kufuzu AFCON ni Yeye kwani ni Kiungo mwenye macho makali ya kujua wapi aupenyeze Mpira huku akijua Kutuliza Timu na nadhani hata Wewe Ssebo huwa unaona Timu yetu ya Simba ikiwa inacheza Kazi ya Mkude "....maelezo ya Murshid.

Akina GENTAMYCINE tukisema kuwa kwa sasa hakuna ' Defensive Midfielder ' bora hapa Afrika Mashariki kama Jonas Gerald Mkude kuna Watu huwa hamuelewi ila sasa kumbe hata Wachezaji wenzake wa Simba SC na wa Timu ya Taifa ya Uganda akina Emanuel Okwi na Juuko Murshid wamesema na kukiri kuwa ni Mchezaji mzuri, muhimu na amebarikiwa Kucheza sehemu ya Kiungo cha Chini ( Namba Sita )

Kazi Kwenu sasa mtakaopanga Kikosi cha Taifa Stars cha Jumapili dhidi ya Uganda Cranes ila Jonas Mkude ndiyo ' Lulu ' yetu.

Nawasilisha.
 
Ha ha ha ha ha
 

Kwanini isiwe kinyume chake kwamba wanataka apangwe huyo Mkude ili waweze kumdhibiti kwani pengine wanajua namna ya kumdhibiti?? Kwanini tusiamini kuwa mleta uzi huu anatumika na maadui?? Mbinu na fitina za mpira zipo nyingi sana...hizo huko juu zinaitwa 'mind games'...Watanzania tusitumike kirahisi na maadui wetu kuhusu mchezo huu...tusilete pressure zisizo na maana kuhusu nani apangwe dhidi ya Uganda...naichukulia habari hii kuwa ni kampeni ya kumshinikiza mwalimu (Amunike) ampange Mkude...Tumwache mwalimu afanye maamuzi yake yake...
 
Acha kupotosha watu wewe hizi stori zako za kufikirika hadithia wajinga wenzako chumbani sijawahi kuona mtu mkurupukaji kama wewe kama huna data uwe unakaa kimya TAPELI MKUBWA WEWE .
 
Hili ni jibu lakini ni makala pia [emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Genta nakukubali sana. Kiukweli utakuwa umeongea nao. Maana hata mimi niliwahi kumsikia okwi akisema katika vipaji adimu kuwahi kupatikana hapa Tz, basi mkude ana kipaji cha kutisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
GENDAMYCINE Wakati fulani badala ya kukuchukia kwa kunipotezea muda kusoma makala zako lakn kuna kitu fulani huwa unanifurahisha sana mdogo wangu..... ''kuelezea hali halisi ya hisia za moyo wako na kile unachokipenda na kukiamini bila kujali nani atakupinga kwenye hoja zako''. big up sana!!!!
 
Mkude pass zake nyingi ni squar pass ambazo hazipeki timu mbele zinafanya timu ionekane inapiga pass nyingi zisizo na faida ndio maana kukosekana kwa Mkude game ya Simba na AS Vita ya Congo timu ilikuwa inakwenda mbele haraka sioni kama kuna ukweli wa unachosema ila ni mtego ili tupoteze game waambie hatudanganyiki......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…