Nilisema tena hadi nikatamba kabisa kwamba katika mahala ambapo nikitaka kupata taarifa zake hata kama zikiwa na ugumu gani kupatikana basi ni ndani ya Klabu ya Yanga SC na tayari hivi ninavyo tiririka na kuserereka hivi nimeshapenyezewa ' nyuzi ' ambazo ni za motomoto kabisa na kama kawaida yangu naziweka wazi hapa.
Kwanza pamoja na kwamba Yanga SC wamesema wapo Kambini Mkoani Morogoro ila ukweli ni kwamba wale Wachezaji wao wa Kikosi cha Kwanza walisafirishwa ' Kimafia ' Kisiwani Pemba ili kwenda kufanyiwa Ndumba / Ushirikina kupitia Bagamoyo na aliyeliratibu hili zoezi zima ni Mkuu mmoja wa Wilaya na Mbunge mmoja ambaye Yeye na Baba yake ni wana Yanga SC wa Kindakindaki kabisa huku wakishirikiana na Mbunge mmoja wa Unguja aitwae Mr. Turki a.k.a White.
Pili hadi hivi sasa yaani ninavyoandika huu ' uzi ' ni kwamba huyo ' Mganga ' wao wa Pemba amewaambia Yanga SC kwamba ' Kinyota ' ili Kesho washinde mechi hiyo wanatakiwa wampange Golini Kipa aitwae Ben Kakolanyi ila Uongozi wa Yanga SC bado haujaafiki na sasa Viongozi wamegawanyika juu ya hili kwani Viongozi wengi wa Yanga SC hawamuanini kabisa Kipa Kakolanyi.
Tatu ni kwamba Mchezaji ambaye ametakiwa kubeba / kuvalishwa ' Hirizi ' Kesho ili ushindi uwe wa 100% ni ' Kiungo ' Thabani Scara Kamusoko ila hata hivyo Mchezaji huyo amekataa ' katakata ' kubebeshwa power bank hiyo ya Kiasili ( Hirizi ) kwa utetezi kwamba tokea aanze ' kuvalishwa / kubebeshwa ' amekuwa akipata ' majeraha ' ya ajabu ajabu sana halafu na Yeye ni mcha Mungu mzuri sana. Tayari kukataa Kwake Mchezaji huyu kumeshatengeneza ' Bifu ' kubwa kati yake na Kiongozi mmoja mwenye dhamana kubwa ya ' Utawala ' ndani ya Klabu.
Nne ni kwamba tokea juzi ' Mganga ' wao huyo wa Pemba aliwaambia Viongozi wa Yanga SC watafute Ndege aina ya ' Bundi ' lakini lazima wawe Watatu Kiidadi lakini mpaka GENTAMYCINE natiririka na naserereka hivi ' Bundi ' aliyepatikana ni mmoja tu tena ' Mtoto ' wakati ' Mganga ' aliwaambia anataka ' Bundi ' ambao ni Wahenga / Wakubwa / Wazee Watatu na sasa huko ' Kambini ' Vongozi wamechanganyikiwa.
Tano ni kwamba kuna ' Kiongozi ' mmoja wa Yanga SC wa Tawi la Zanzibar akishirikiana na ' Makomandoo ' baadhi wa Yanga SC wanafanya ' Ujasusi ' wao wa kujua ni Kikosi gani Kesho Kocha wa Simba Joseph Marios Omog atakipanga ili wakishakijua wakipeleke kwa huyo ' Mganga ' kusudi aweze kukifanyia ' Ndumba / Uchawi ' kusudi Kesho kisiwe na ' madhara ' na hatimaye Simba SC iweze kufungwa magoli mengi ila Viongozi wa Simba SC ambao wengi wao nao wanasifika kwa ' Umafia ' tena uliotukuka kabisa wamekuwa makini kuwa ' wasiri ' ambapo hadi sasa ' Kikosi ' cha Kesho bado hakijawekwa hadharani.
Sita ni kwamba wakati Viongozi wa Yanga SC wakiwa ' busy ' kuhangaika na ushindi wa Kesho kuna Wana Yanga SC wa matawi mawili makubwa yanayoongozwa na ' Kijana ' mmoja aliyekuwa ' mropokaji ' wao nao wamejipanga tokea juzi wameenda Tanga kwa yule ' Mganga ' ambaye aliisaidia Timu ya Coastal Union ya Tanga kuifunga Yanga SC katika msimu wa Ligi uliomaliza katika Uwanja wa Mkwakwani Tanga ili ' aharibu ' na Yanga SC Kesho ifungwe na Simba SC kisha wao waanzishe ' timbwili ' Klabuni halafu Viongozi Wakuu wa Yanga SC ' wafukuzwe ' na wao waweke Watu wao na warudi kwani wanasema Viongozi wa sasa wamewanyima ' ulaji ' wao na wamekuwa ' wanoko ' sana Kwao.
Saba ni kwamba Yanga SC sasa wanahangaika sana kutaka kumtafuta ' Meneja ' wa Uwanja wa Uhuru ambapo mchezo utachezwa Kesho ili waweze ' kumshawishi ' mida ya jioni waingie hapo uwanjani na kitu ( naamini mmeshakijua ) ambacho hata katika ile mechi ya Simba na Yanga CCM Kirumba Mwanza ambapo Simba ilifungwa goli 3 kwa 0 waliingia nacho na ' Kukifukia ' kisha baada ya mechi ile wakakifukua na kukirudisha katika moja ya Hospitali kubwa na Mkoni Mwanza japo baadae hili tukio liliweza kuwafukuzisha Watu Kazi.
Mpaka kufikia muda huu haya ndiyo machache niliyoweza kuyapata kutoka moja kwa moja ndani ya Kambi ya Yanga SC kama vile ambavyo nimepenyezewa na Mtu ambae Yanga SC wanajua ni mwenzao lakini kumbe Kiuhalisia ni mwana Simba SC tena wa ' Kindandaki ' ambaye ndiyo huyu huyu pia aliwasaidia Simba SC katika mechi ile ya Zanzibar na ya Ngao ya Hisani.
Nawasilisha.