Exhaust kujaa Carbon bila gari kutoa moshi mweupe

Exhaust kujaa Carbon bila gari kutoa moshi mweupe

Makobus

Senior Member
Joined
Jul 30, 2012
Posts
169
Reaction score
110
Wadau habarini.

Shida yangu nilishaileta humu mkanisaidia japo tatizo halijatibika. Leo naileta kivingine.

Kila nikipima oil asubuhi kwa dipstick naona oil inashuka chini. Gari haitoi moshi ule mweupe, bali inatoa carbon na maji maji tu kwenye exhaust. Wala hakuna leakage yoyote kule uvunguni. Carbon, kwa ufafanuzi ni masizi meusi.

Siwezi kukimbilia tatizo la oil kuchomwa na mafuta kwani ningekuwa ninaona moshi na exhaust ingekuwa inalowa oil. Lakini ninachoona ni hiyo carbon na maji tu.

Shida ni nini wataalamu?

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Point of correction!

Exhaust manifolds ikijaa carbon, moshi utakaotoka ni mweusi na si mweupe.
 
Japo hata huo moshi mweusi hautoki. Kinachoonekana ni carbon ilolowa maji ukigusa lile bomba.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Oooh! Moshi kumbe unatoka wa kawaida tu? Then hapo shida ni oxy sensor au air filter chafu mno!

Hewa inaingia ya kutosha ila oxygen inachafuliwa kwenye filter. Jaribu kuangalia hivyo vitu.
 
Oooh! Moshi kumbe unatoka wa kawaida tu? Then hapo shida ni oxy sensor au air filter chafu mno!

Hewa inaingia ya kutosha ila oxygen inachafuliwa kwenye filter. Jaribu kuangalia hivyo vitu.
Sawa. Ila tatizo kubwa linaloenda sambamba na hili ni oil kupungua siku kwa siku. Nilidhani inachomwa pamoja na mafuta. Lakini, mbona hakuna dalili hizo kwenye exhaust kulowa oil na kutoa huo moshi?

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Sawa. Ila tatizo kubwa linaloenda sambamba na hili ni oil kupungua siku kwa siku. Nilidhani inachomwa pamoja na mafuta. Lakini, mbona hakuna dalili hizo kwenye exhaust kulowa oil na kutoa huo moshi?

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Moshi wa gari yako ni wa kawaida?

Nyongeza, huenda coolant au oil ikawa inachomwa na mafuta kwa kiasi kidogo. Usidharau hili pia. Hivyo bado haijafika hatua ya kuona oil kwenye exhaust!

Kujua hili, kagua spark plugs na injectors utagundua! Pia head gasket ina uwezekano ikawa inavuja. Ni hayo!
 
Back
Top Bottom