Blasio Kachuchu
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 721
- 438
Mkuu wa masoko wa Africarriers Ltd Mohamed Ladha (kushoto) akielezea zaidi ubora wa magari kwa Menejimenti, Wafanyakazi na Wateja wa Benki ya Exim Tanzania baada ya utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Africarriers na Benki ya Exim Tanzania yenye lengo kufadhili na kurahisisha ununuzi wa magari kwa watu binafsi, wajasiriamali, biashara ndogo na za kati (SMEs), pamoja na taasisi mbalimbali nchini kupitia mikopo yenye masharti nafuu ya ulipaji.
Tukio hilo lilishuhudiwa na Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim Tanzania, Shani Kinswaga (wa nne kulia), Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Tanzania, Stanley Kafu (wa tano kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Africarriers Ltd Bw Fidahussein Rashid (wa tatu kushoto) jijini Dar es Salaam juni 16 2026.
Benki ya Exim Tanzania imeingia katika ushirikiano wa kimkakati na kampuni ya Africarriers Limited utakaowawezesha Watanzania kumiliki magari kwa urahisi kupitia mikopo yenye masharti nafuu, hatua inayotarajiwa kuchochea ukuaji wa biashara na shughuli za kiuchumi nchini.
Makubaliano hayo yaliyosainiwa jijini Dar es Salaam Juni 16, 2026, yanalenga kuwapatia watu binafsi, wafanyabiashara, wajasiriamali pamoja na wamiliki wa biashara ndogo na za kati fursa ya kupata ufadhili wa kununua magari mapya na yaliyotumika kwa utaratibu rahisi zaidi.
Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo, Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim Tanzania, Shani Kinswaga, alisema ushirikiano huo ni sehemu ya mkakati wa benki wa kuendelea kutoa suluhisho bunifu zinazokidhi mahitaji halisi ya wateja.
"Ushirikiano wetu na Africarriers unatuwezesha kutoa huduma rahisi na zinazobadilika za ufadhili wa magari ambazo zitawawezesha watu binafsi na wafanyabiashara kupata usafiri wa kuaminika huku wakihifadhi rasilimali zao za kifedha kwa matumizi mengine muhimu," alisema Shani.
Alisema mpango huo utasaidia kuongeza tija katika biashara, kupanua fursa za kiuchumi na kurahisisha upatikanaji wa usafiri kwa makundi mbalimbali ya Watanzania bila kuathiri mtaji wa uendeshaji wa biashara zao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Fedha wa Kundi la Africarriers, Mustafa Rashid, alisema ushirikiano huo unaunganisha uwezo wa Africarriers katika upatikanaji wa magari na uzoefu wa Exim Bank katika utoaji wa huduma za kifedha ili kuwapa Watanzania suluhisho bora la umiliki wa magari.
"Kwa kushirikiana na Benki ya Exim Tanzania, tunawapa wateja fursa rahisi ya kumiliki magari huku tukichochea ukuaji wa biashara na maendeleo ya uchumi wa taifa," alisema Mustafa.
Ushirikiano huo unaakisi dhamira ya taasisi hizo mbili ya kupanua upatikanaji wa huduma za usafiri kwa gharama nafuu na kuwezesha wananchi wengi zaidi kutimiza ndoto ya kumiliki magari kwa matumizi binafsi na ya kibiashara.
Benki ya Exim imewahimiza wateja kutembelea matawi yake au yadi za Africarriers zilizopo nchini kote ili kupata maelezo zaidi kuhusu huduma hiyo na aina za magari yanayopatikana.
Exim Bank Tanzania ilianzishwa mwaka 1997 na imeendelea kuwa miongoni mwa taasisi za fedha zinazoongoza nchini, ikiwa na shughuli pia nchini Comoro, Djibouti, Uganda na Ethiopia. Nayo Africarriers Limited, iliyoanzishwa mwaka 1976, ni miongoni mwa kampuni kubwa za biashara ya magari Afrika Mashariki na Kati.
Tukio hilo lilishuhudiwa na Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim Tanzania, Shani Kinswaga (wa nne kulia), Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Tanzania, Stanley Kafu (wa tano kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Africarriers Ltd Bw Fidahussein Rashid (wa tatu kushoto) jijini Dar es Salaam juni 16 2026.
Benki ya Exim Tanzania imeingia katika ushirikiano wa kimkakati na kampuni ya Africarriers Limited utakaowawezesha Watanzania kumiliki magari kwa urahisi kupitia mikopo yenye masharti nafuu, hatua inayotarajiwa kuchochea ukuaji wa biashara na shughuli za kiuchumi nchini.
Makubaliano hayo yaliyosainiwa jijini Dar es Salaam Juni 16, 2026, yanalenga kuwapatia watu binafsi, wafanyabiashara, wajasiriamali pamoja na wamiliki wa biashara ndogo na za kati fursa ya kupata ufadhili wa kununua magari mapya na yaliyotumika kwa utaratibu rahisi zaidi.
Kupitia mpango huo, wateja wa Benki ya Exim wataweza kupata mikopo ya kununua magari ya chapa mbalimbali zikiwemo Jetour, Eicher, Sany na JAC Motors, huku wakitakiwa kuchangia asilimia 20 hadi 30 ya thamani ya gari kama malipo ya awali na kulipa salio kwa kipindi cha hadi miezi 72 kulingana na uwezo wao wa kifedha.Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo, Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim Tanzania, Shani Kinswaga, alisema ushirikiano huo ni sehemu ya mkakati wa benki wa kuendelea kutoa suluhisho bunifu zinazokidhi mahitaji halisi ya wateja.