Blasio Kachuchu
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 721
- 438
Huduma hii ni sehemu ya mikakati ya benki hiyo kuleta ubunifu unaoendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia pamoja na uhalisia wa maisha ya kila siku ya wateja. Aliyekaa kushoto ni Meneja Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Tanzania, Kauthar D’souza. Uzinduzi huo umefanyika Mei 21, 2026 katika za makao makuu ya Benki ya Exim jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
Huduma hii inawawezesha wateja kupata huduma mbalimbali za kibenki moja kwa moja kupitia WhatsApp. Huduma hizo ni pamoja na kuangalia salio, kuhamisha fedha, kutuma fedha kwenda simu za mkononi, kufanya malipo kwa wafanyabiashara, kulipia huduma za Serikali kupitia GePG pamoja na huduma zinazohusiana na kadi za benki. Mteja anaweza kupata huduma zote hizi kupitia jukwaa la WhatsApp bila uhitaji wa kupakua programu nyingine yoyote wala haja ya kutembelea tawi la benki.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha Mifumo Mbadala ya Kidijitali wa Benki ya Exim, Bw. Silas Matoi, alisema mfumo huo umebuniwa kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki na kuimarisha ubora wa huduma kwa wateja.
“Kupitia Exim WhatsApp Banking, wateja wetu sasa wanaweza kuangalia salio kwenye akaunti zao, kutuma fedha kwenda kwenye mitandao ya simu, kulipa bili na malipo mbalimbali ya Serikali, kupata huduma zote zinazohusiana na kadi pamoja na kufanya miamala mingine moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Hii inaondoa ulazima wa aidha kupakua au kubadilisha programu mbalimbali au kupitia mifumo migumu, kwani sasa huduma zote muhimu za kibenki zinapatikana sehemu moja, iliyozoeleka, rahisi na inayopatikana kwa watu wote,” alisema Matoi.
Katika hatua nyingine, Matoi alieleza kuhusu ubora wa teknolojia iliyotumika kubuni mfumo huo na kutoa hakikisho kuhusu usalama wa huduma hiyo.
Huduma hii mpya ya Exim WhatsApp Banking inawawezesha wateja wa Benki ya Exim kufanya miamala yao ya kila siku kupitia jukwaa hilo wanalolitumia kila siku, hivyo kuondoa ulazima wa kupakua programu tofauti huku wakifurahia huduma za kibenki zilizo rahisi, za haraka na zilizozoeleka.
Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Tanzania, Kauthar D’souza, alisema kuanzishwa kwa huduma hiyo kunadhihirisha dhamira endelevu ya benki hiyo katika kuleta ubunifu na kuboresha huduma kwa wateja.
Aliongeza kuwa uzinduzi huo ni sehemu ya mikakati mipana ya benki ya kuendelea kuleta ubunifu unaochochewa na mahitaji halisi ya wateja na kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia.
“Tunazingatia namna wateja wetu wanavyoishi, tunaelewa mifumo na majukwaa wanayoyaamini, na kisha tunabuni suluhisho rahisi linaloendana na maisha yao ya kila siku. Huduma ya benki kupitia WhatsApp si tu njia mpya ya kutoa huduma, bali pia hatua inayodhihirisha kuwa Benki ya Exim ni benki inayokua sambamba na wateja wake, inayosikiliza mahitaji yao na kufanya maisha yao ya kifedha kuwa rahisi zaidi kila siku,” alisema.
Wateja wanaweza kupata huduma hii kwa kuanzisha mawasiliano kwa njia ya ujumbe kupitia namba rasmi ya WhatsApp ya Benki ya Exim Tanzania (+255 675 800 100), ambapo wataelekezwa kupitia mchakato rahisi wa usajili ikiwemo kuweka PIN kabla ya kuanza kutumia huduma mbalimbali zinazopatikana.Benki ya Exim pia imeeleza kuwa ina mpango wa kupanua huduma hii kwa kuongeza vipengele vingine ikiwemo maombi ya mikopo na huduma za uwekezaji, ikiwa ni sehemu ya mkakati wake endelevu wa mageuzi ya kidijitali.