Experience requirements katika nafasi za kazi zinaudhi

Experience requirements katika nafasi za kazi zinaudhi

Joined
Feb 1, 2011
Posts
21
Reaction score
5
Jamani wana JF, kuna waajiri wengine wanaudhi sana pale wanapotaka kuajiri mtu mwenye experience. Kuna watu ndo tumetoka chuo tunahitaji kazi ili tupate uzoefu wao wanasema experience....... experience? a lot of bullshit!Hivi nani alizaliwa na experience?wapi hao wenye experience walikozipata?hawakuwa na siku katika maisha yao ambayo waliita siku ya kwanza kazini?wanataka hizo experience tuzipate wapi kama hatutapata sehemu ya kuanzia? nini maana ya staff training and coaching?

Hebu tulijadili hili wana JF hasa wahanga kama mimi.
 
Private sector kwa kawaida inataka kukwepa gharama za kutrain kwa kuajiri walio na experience tayari - as long as wenye experience wanapatikana. Public sector ilpokuwa mwajiri mkuu huko nyuma ndiyo hasa iliyokuwa inapokea vijana wengi kutoka vyuoni na kuwatrain, halafu walikuwa wanahamia private sector kufuata masilahi zaidi.

Kwa vile Public sector imepunguza sana kuajiri baada ya kuacha viwanda, biashara, nk, kwa maoni yangu private sector italazimika kufanya training - kwani itakosa mahali pa kupoach.
 
Na hii nadhani hasa ndio kazi ya waziri anyehusika na ajira, kuonana na kupanga na Private sector jinsi gani ya kuwa obsorb hawa vijana wanaomaliza shule na bado hawana experience. Hapa kwetu tuna waziri anyeshughulika na ajira ila miaka yote mitano inaisha wala haijulikani anafanya nn kuhusu ajira. Haiwezekani tunasema tutatoa ajira kwa vijana wakati kazi zote zinataka wenye experience hivyo kuwaacha vijana wengi wanaomaliza vyuo mablimbali. Tunahitaji toka kwa waziri mikakati ya ajira kwa vijana wasio na uzoefu na jinsi gani watakuwa absorbed kwenye private sector. Nadhani waziri mhusika au wapambe wake huenda wanachungulia hapa. Message sent!
 
hii inafanya wanafunzi wengi kujikuta wanakosa ajira, na baadae kudumbukia kwenye sekta tofauti na tulivyosoma.inatia hasira sana kuona kuwa kila sehemu watu wanaulizia experience...sasa jamani ,mtu akitoka kazini ,atapata wapi experiences?:A S 13: hili linafaa kuangaliwa kwa undani kabisa, kwani wanafunzi wanaomaliza iwe vyuo au sekondari kila siku wanazidi kuwa wengi kwenye nchi yetu.je tufuate nani atupe hiyo experiences...!?
 
iNASIKITISHA KUSIKIA PROPAGANDA ZA VIONGOZI WETU WAKATI WA UCHAGUZI NA MWINGINEO. WANATUGDANGANYA SANA KUHUSU HILI
Haiwezekani tunasema tutatoa ajira kwa vijana wakati kazi zote zinataka wenye experience hivyo kuwaacha vijana wengi wanaomaliza vyuo mablimbali. Tunahitaji toka kwa waziri mikakati ya ajira kwa vijana wasio na uzoefu na jinsi gani watakuwa absorbed kwenye private sector
 
Ni kweli inaudhi haswa pale unapoambiwa 5 to 10 years experience,unajiuliza je graduates waende wapi?
hata hivyo ukiangalia kuna ile experience ambayo unaweza kuipata thru internship, ukiwa likizo mwanafunzi jitahidi kutafuta
mahali ukafanya internship hata kwa mwezi mmoja,mpaka umalize chuo experience unayo tya kutosha..au pia kuna kazi za kuvolunteer unaweza fanya,pia ni experience.
Tatizo letu sisi tunasubiri tumalize chuo kabisa ndo tutafute kazi matokeo yake unakutana na huo msemo 'experience' tunabaki kulalama tuu.
tujitume vijana, tufanye kazi,use ur likizo time kufanya kazi whether ni volunteer job au internship ili mradi upate experience.

Ni mtazamo tu.
 
Owkey Sweetdada I've been doing the same katika maisha yangu ya miaka minne ya chuo,Nime volunteer, nimefanya internship but unaambiwa at least 5 years experience and expertise! are they serious?illogical!
 
Back
Top Bottom