tindikalikali
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 4,854
- 1,129
Mkubwa katika usimamizi nilikua makini.
Tatizo SOKO.
Mtu unalima kwa gharama kuubwa halafu unaishia kuuza gunia elfu 30.
Inasikitisha sana.
Pole. Mie ningezimia.
Ngoja niendelee na miti kwanza japo risiki pia ni nyingi
Pole. Mie ningezimia.
Ngoja niendelee na miti kwanza japo risiki pia ni nyingi
Ndo hivyo.
Inabidi kukaza roho
Kuna Risk gani kwenye miti??
Kuna moto unaweza ingia shambani kwa miti ikiwa na umri fulani.
Hiyo Risk nadhani ni manegeable hasa kupalilia kuzunguka shamba na kufyeka majani. Nataka kununua shamba la miti na mimi nadhani utanisidia mkuu au Malila anisaidie nipate shamba la miti na mimi.
Mkuu Malila naomba no. Yako wewe ni muhimu.
Mimi nitakusaidia kupata shamba la kuotesha miti, bei ni Tsh 60,000/ kwa eka. Unataka eka ngapi? Halafu Mamdenyi si ungemkatia kile kipande chako cha upande wa mashariki pale njiani mbona hakina miti !!!!!!
Kilimo kwa nchi yoyote maskini na serikali tapeli lazima jasho likutoke..ndo maana nchi za wenzetu walioendelea wachache wanajishughulisha na kilimo na serikali zao zinawaenzi kweli wakulima maana wanajua ni biashara kichaa..with very high risk, hasa zama hizi za vimbunga, ukame, mabarafu yasiofuata misimu yake ya asili.Kulima Tanzania ni kazi kubwa sana.
Masoko sio ya uhakika.
Mimi nitakusaidia kupata shamba la kuotesha miti, bei ni Tsh 60,000/ kwa eka. Unataka eka ngapi? Halafu Mamdenyi si ungemkatia kile kipande chako cha upande wa mashariki pale njiani mbona hakina miti !!!!!!
Kwa sasa siuzi tena,
Nilikuwa kwenye project ingine
Ila Mungu akipenda mwishoni mwa mwaka huu nitahamia shambani ili
kupanda na kuweka mambo sawa.
Hata hivyo mie sijanunua hizo za bei hiyo,
Mi niko mjini zaidi na bei iko juu pia.
Mkubwa katika usimamizi nilikua makini.
Tatizo SOKO.
Mtu unalima kwa gharama kuubwa halafu unaishia kuuza gunia elfu 30.
Inasikitisha sana.
Niko vijijini ndani ndani sana, huko hata 1000 unapata,kama unataka za mjini aliko Mamdenyi pia utapata. Bei zinatofautiana, mjini miche inauzwa kimjinimjini, na kule kwetu vijijini bei iko poa, ila wastani wa kitalaam wa miti ya mbao ni vizuri usizidi miti 530/540 kwa eka. Vijana wanapiga hadi 600 kwa makosa. Kama ni boriti, eka moja inaweza kwenda hadi miche 1000/1200
Heshima kwenu viongozi wangu.
Wakuu natumai hamjambo na mnaendelea vyema na shughuli za ujenzi wa taifa letu.
Wakuu baada ya kusikia wengi wetu wakisifia sana kilimo cha vitunguu nikapata muamka na mimi nikaingia katika kilimo cha vitunguu.
Nilikodisha ekari sita pale Ruaha Mbuyuni.
Kwa kweli sitaki kusema mengi ila ninachoweza kusema ni kwamba kutajirika kwa kilimo cha vitunguu LABDA inawezekana lakini sio kiurahisi kama wengi wetu wanavyohubiri humu.
Kwa EKARI ZOTE SITA nilizolima nilivuna gunia mia moja na tano tu.
Gunia moja niliuza kwa shilingi elfu thelathini tu.
Nilivuna mwezi wa saba mwaka huu ,2014.
Nilitumia shilingi karibia MILIONI KUMI NA TATU kulima ekari zote sita halafu nilipovuna nikapata shilingi milioni tatu laki moja na elfu hamsini hivi.3,150,000 kutoka kwenye mavuno ya ekari zote sita.
Nilikua makini sana kutimiza mahitaji yote niliyoambiwa nikitimiza nitavuna na kupata faida.
Anayetaka kuingia kulima na aingie ila tuwaeleze wenzetu ukweli,hichi kilimo ni very risky.
Anyway,mwakani nitalima tena maana jamaa wamenishawishi sana wakidai hasara ya mwaka huu isinikatishe tamaa.Nashindwa kusema kama kinalipa au hakilipi kwa sababu nimelima mara moja tu.Matokeo ya mwaka kesho ndio yatanipa uamuzi wa kujikita kwenye kilimo au kujitoa na kuwaachia kina Malila.
Kitu nilichogundua ni kuwa watu wengi humu hawasemi ukweli kuhusu hichi kilimo.
Mimi nitakusaidia kupata shamba la kuotesha miti, bei ni Tsh 60,000/ kwa eka. Unataka eka ngapi? Halafu Mamdenyi si ungemkatia kile kipande chako cha upande wa mashariki pale njiani mbona hakina miti !!!!!!
mhh!!hayo Mashamba ya sh.60000 kwa ekari moja yako wapi mkuu,ni hapa hapa Tanzania!!!?