Heshima kwenu viongozi wangu.
Wakuu natumai hamjambo na mnaendelea vyema na shughuli za ujenzi wa taifa letu.
Wakuu baada ya kusikia wengi wetu wakisifia sana kilimo cha vitunguu nikapata muamka na mimi nikaingia katika kilimo cha vitunguu.
Nilikodisha ekari sita pale Ruaha Mbuyuni.
Kwa kweli sitaki kusema mengi ila ninachoweza kusema ni kwamba kutajirika kwa kilimo cha vitunguu LABDA inawezekana lakini sio kiurahisi kama wengi wetu wanavyohubiri humu.
Kwa EKARI ZOTE SITA nilizolima nilivuna gunia mia moja na tano tu.
Gunia moja niliuza kwa shilingi elfu thelathini tu.
Nilivuna mwezi wa saba mwaka huu ,2014.
Nilitumia shilingi karibia MILIONI KUMI NA TATU kulima ekari zote sita halafu nilipovuna nikapata shilingi milioni tatu laki moja na elfu hamsini hivi.3,150,000 kutoka kwenye mavuno ya ekari zote sita.
Nilikua makini sana kutimiza mahitaji yote niliyoambiwa nikitimiza nitavuna na kupata faida.
Anayetaka kuingia kulima na aingie ila tuwaeleze wenzetu ukweli,hichi kilimo ni very risky.
Anyway,mwakani nitalima tena maana jamaa wamenishawishi sana wakidai hasara ya mwaka huu isinikatishe tamaa.Nashindwa kusema kama kinalipa au hakilipi kwa sababu nimelima mara moja tu.Matokeo ya mwaka kesho ndio yatanipa uamuzi wa kujikita kwenye kilimo au kujitoa na kuwaachia kina
Malila.
Kitu nilichogundua ni kuwa watu wengi humu hawasemi ukweli kuhusu hichi kilimo.