father-xmas mimi nakubaliana na wewe kwamba uhalisia kamili wa biashara hauzungumzwi.
Mimi nina miti ya teak niliipanda 1994, watu wanasema miti ya teak inatafutwa sana. Lakini mi nimetafuta hao wanunuzi mpaka sasa sijapata. Maneno tu meengi lakini ukweli wenyewe tofauti
Miti ya Teak ina maelezo ya hivyo mengi sana, ila ninachojua ni kwamba, ni kwa scale kubwa ndio unaweza pata soko la maana. Sasa kama una scale ndogo ya shamba itakuwa taabu kidogo. Mfano eka kumi za Mitiki kule Kigoma, mnunuzi anayetaka magogo kama laki moja atakuja kweli? Kwa small scale, teak ni hasara sababu inachukua miaka mingi sana mpaka kukomaa,ndio maana kwa watu binafsi ni mtihani kidogo.
Habari ya mitiki kama unaitaka hasa, basi nenda Longuza Tanga, Kilombero na Lindi ktk misitu ya serikali ambako hata mvunaji anaweza leta mitambo toka nje akijua atapata faida.