Explanation ya Waziri Simba usalama wa Viongozi!

Explanation ya Waziri Simba usalama wa Viongozi!

Kuhani

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2008
Posts
2,944
Reaction score
64
Shambulio dhidi ya Rais Mstaafu Mwinyi laizindua serikali

Waziri Simba asema ni aibu kwa taifa, ulinzi waimarishwa


Na Jackson Odoyo
MWANANCHI
3/14/2009



KIBAO cha shavuni alichopigwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi kimeichanganya serikali na kuvilazimu vyombo vyake vya ulinzi na usalama kujipanga upya kuhakikisha viongozi wanakuwa salama wakati wote.

Habari ambazo zimepatikana jijini Dar es Salaam na kuthibitishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sofia Simba, zinasema tukio hilo limeifedhehesha serikali na hivyo kuamua kuchukua hatua za haraka kuepuka hali hiyo.

Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni kuimarisha ulinzi wa viongozi wakuu ili kuepuka aibu hiyo.

Kauli ya waziri imekuja ikiwa ni saa chache baada ya kijana Ibrahim Said ‘Ustaadhi' (26) aliyemshambulia Mwinyi kwa kisingizio cha kuzungumzia matumizi ya kondomu kwenye hadhara ya kidini, kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili kwa njia ya simu akiwa safarini kuelekea Kigoma, Simba alisema, "Tukio hilo limetufedhehesha kwa kuwa hakuna aliyetegemea kama mtu huyo atachukua hatua kama hiyo.

"Kutokana na tukio hilo tumeamua kuongeza ulinzi katika ziara zote za viongozi wakuu wa kitaifa na kimataifa hapa nchini hasa katika nyumba za ibaada," aliongeza Waziri Simba.

Alipoulizwa kama serikali ilizembea katika kusimamia ulinzi wa viongozi hao, alikana akisema kuwa tukio hilo lilipotokea ulinzi ulikuwepo wa kutosha.

"Sio kweli kwamba hakukuwa na ulinzi, lakini yawezekena walijisahau kwa sababu Mzee Mwinyi alikuwa katika eneo la usalama wa kutosha, na ni eneo la ibada ambapo hakuna aliyetegemea kuwa tukio hilo lingetokea," alisema Waziri Simba.

Aliongeza kuwa hivi sasa kutakuwa na ulinzi mkali hadi makanisani na misikitini ingawa awali ilizoeleka kwamba ni sehemu za amani na utulivu, lakini kwa tukio hilo la kufedhehesha na aibu kwa taifa hili ni lazima wajipange upya.

Walinzi wa viongozi wanafundishwa kujilegeza sehemu za amani, ibada, na utulivu? Mtu akitaka kumdhuru kiongozi ataenda kwenye sehemu ya ghasia na ulinzi mkali au ya utulivu asipotegemewa? Kama ulinzi ulikuwa unatosha ataimarisha nini sasa?

Wataimarisha ulinzi misikitini na makanisani, kwa hiyo next time kiongozi akipigwa mkuki kwenye msiba watasema hawakutegemea mashambulizi kwenye kilio?

Huyu Mama mzima?
 
Walinzi wa viongozi wanafundishwa kujilegeza sehemu za amani, ibada, na utulivu? Mtu akitaka kumdhuru kiongozi ataenda kwenye sehemu ya ghasia na ulinzi mkali au ya utulivu asipotegemewa? Kama ulinzi ulikuwa unatosha ataimarisha nini sasa?

Wataimarisha ulinzi misikitini na makanisani, kwa hiyo next time kiongozi akipigwa mkuki kwenye msiba watasema hawakutegemea mashambulizi kwenye kilio?

Huyu Mama mzima?

Kuhani,

Kote umeenda sawa, ila comment yako ya mwisho umeteleza! Au ni 'mfumo dume' syndrome? Sidhani kwamba kama maneno hayo yangelitamkwa na Waziri Mkuu Pinda ungelisema "Huyu Baba mzima?"

Mama Simba ni mzima na aliyoyasema yanaweza kusemwa na kiongozi ama mtu yeyote katika kujihami kutokana na aibu iliyotokea ya kiongozi wa ngazi ya juu kitaifa kupigwa mbele ya kadamnasi na walinzi wakiwepo.

Alichotakiwa kusema ni kukiri kwamba ulinzi ulikuwa mbovu, hasa yule mlinzi wa karibu wa Mzee Mwinyi. Sikuliona tukio zima kwenye TV lakini nahisi aliyekuwa mlinzi wa Mzee Mwinyi siku hiyo ni kijana mzembe. Kama hivyo ndivyo, tukio hilo limedhihirisha ubovu katika mafunzo ya walinzi wa viongozi (bodyguards) wa sasa. Angelikuwa ni mmoja wa wale walinzi 'mababu' nina hakika yule kijana aliyempiga Mzee wetu, aliponyanyuka tu na kuanza kuelekea kwenye meza kuu, mlinzi angeenda haraka kumzuia na kumhoji kinachompeleka meza kuu.

Kama alivyosema Mama Simba, ni kweli walinzi waliokuwepo kwenye eneo lile walijisahau kutokana na mazoea ya kudhani kwamba bado tuko kwenye enzi za amani na utulivu!

Kuhani, bado nasisitiza kwamba pamoja na uhuru wote tunaoufurahia wa kufanya mambo ambayo ni kinyume na maadili yetu, na kutoifanyia kazi misingi bora tuliyojengewa kitaifa tunajipalia makaa. Wapo wanaobisha, lakini ukweli ndio huo.
 
Kuhani,

Hili la uzembe la ulinzi halijaanza leo. Miaka kadhaa iliyopita nikiwa nyumba ya ibada, nilipata nafasi mara kadhaa kusimama nyuma ya mmoja wa kiongozi mkuu mara baada ya kumaliza misa.

Hata tukiwa ndani ya nyumba ya ibada, ukaribu ulikuwa sawa na zero distanti, nikajiuliza, siku anakuja mwenye akili chafu itakuwaje, je hawa jamaa walinzi watazinduka saa ngapi?

Naona sasa wanazinduka kwenye ibada, bado mazikoni na hata wakiendesha magari isije yale ya Tsvangarai!
 
Back
Top Bottom