Kuhani
JF-Expert Member
- Apr 2, 2008
- 2,944
- 64
Shambulio dhidi ya Rais Mstaafu Mwinyi laizindua serikali
Waziri Simba asema ni aibu kwa taifa, ulinzi waimarishwa
Na Jackson Odoyo
MWANANCHI
3/14/2009
KIBAO cha shavuni alichopigwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi kimeichanganya serikali na kuvilazimu vyombo vyake vya ulinzi na usalama kujipanga upya kuhakikisha viongozi wanakuwa salama wakati wote.
Habari ambazo zimepatikana jijini Dar es Salaam na kuthibitishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sofia Simba, zinasema tukio hilo limeifedhehesha serikali na hivyo kuamua kuchukua hatua za haraka kuepuka hali hiyo.
Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni kuimarisha ulinzi wa viongozi wakuu ili kuepuka aibu hiyo.
Kauli ya waziri imekuja ikiwa ni saa chache baada ya kijana Ibrahim Said ‘Ustaadhi' (26) aliyemshambulia Mwinyi kwa kisingizio cha kuzungumzia matumizi ya kondomu kwenye hadhara ya kidini, kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela.
Akizungumza na Mwananchi Jumapili kwa njia ya simu akiwa safarini kuelekea Kigoma, Simba alisema, "Tukio hilo limetufedhehesha kwa kuwa hakuna aliyetegemea kama mtu huyo atachukua hatua kama hiyo.
"Kutokana na tukio hilo tumeamua kuongeza ulinzi katika ziara zote za viongozi wakuu wa kitaifa na kimataifa hapa nchini hasa katika nyumba za ibaada," aliongeza Waziri Simba.
Alipoulizwa kama serikali ilizembea katika kusimamia ulinzi wa viongozi hao, alikana akisema kuwa tukio hilo lilipotokea ulinzi ulikuwepo wa kutosha.
"Sio kweli kwamba hakukuwa na ulinzi, lakini yawezekena walijisahau kwa sababu Mzee Mwinyi alikuwa katika eneo la usalama wa kutosha, na ni eneo la ibada ambapo hakuna aliyetegemea kuwa tukio hilo lingetokea," alisema Waziri Simba.
Aliongeza kuwa hivi sasa kutakuwa na ulinzi mkali hadi makanisani na misikitini ingawa awali ilizoeleka kwamba ni sehemu za amani na utulivu, lakini kwa tukio hilo la kufedhehesha na aibu kwa taifa hili ni lazima wajipange upya.
Walinzi wa viongozi wanafundishwa kujilegeza sehemu za amani, ibada, na utulivu? Mtu akitaka kumdhuru kiongozi ataenda kwenye sehemu ya ghasia na ulinzi mkali au ya utulivu asipotegemewa? Kama ulinzi ulikuwa unatosha ataimarisha nini sasa?
Wataimarisha ulinzi misikitini na makanisani, kwa hiyo next time kiongozi akipigwa mkuki kwenye msiba watasema hawakutegemea mashambulizi kwenye kilio?
Huyu Mama mzima?