Extraction ya Chris Hemsworth mmeionaje?


Niki download kwenye simu naweza ihamishia kwa laptop au kwenye flash kwa watu wanaotumia Iphone?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Movie: Extraction
Year: 2020
Genre: Action
Country: USA
Language: English

Huu mzigo naanza kwa kuupa rate ya 7.9/10...

Bonge moja la mzigo, Sijaona muda sana type ya namna hii ya mizigo ya Action...Humu kuna Choreography nzuri sana, Mtu anapigwa mpaka unatamani uende kumpa pole.

Chris Hemsworth wengi tunamjua kama Thor humo kakichafua sana akicheza kama Mercenary wa nguvu na anaegopeka zaidi humu tunamkuta kama Tyler Rake, mbavu nene na experience ya kutosha...Anapewa mission ya kwenda kumuokoa mtoto wa gaidi mmoja(Drug lord) ambae alikuwa ametekekwa na kundi jingine la Kingpins (yes yeye anafanya for cash)..Utata unaanza hapo mission ilikuwa ngumu, na upande wa malipo Ya tyler unazingua, kuna wahuni wana kanda mikandiko yote humo, unapata Chapati, mandazi, mikate mpaka sambusa.

Kuna sehemu jamaa alipigwa banzi la mkono akaenda kujipangusa kwenye ukuta Vupppp! [emoji3][emoji3][emoji3],



Noma,...Wale wa Telegram nyie andaeni tu Mb's zenu tu.
____________________________________________
Karibu ujipatie Movies/Series mbalimbali

Tunapatikana Igoma, Mwanza

Contacts: Telegram| WhatsApp| SmS| Call | 0710995752

, Delivery 10 km kutoka Ofisi zetu TZS 2,000.

Unataka kujiunga na huduma ya Telegram Premium? Tuandikie kupitia whatsapp/sms au call sasa upatiwe utaratibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HI inshu HATA MIMI BADO INANICHANGANYA MAANA ovi alikuwa na bodguard na huyo bodguard alipewa alifa ya kumtafuta muajili wake ilihali tayali mr taylor nae kapewa dili la kumsakua dogo[OVI] alafu pind wanapo kutana tena kunakuwa na vita baina ya bodguad na mr taylor swali ni nani aliye toa hili dili mara mbili ?
 
Nadhani hii ndio sababu fan wengi wanasema it was too much holywood
 
Naona watu wengi mnaulizia jinsi ya kupata hii Movie ila ni simple tu.

Download app inayoitwa TeaTV inapatikana Google.

Ni app nzuri sana haijawahi niangusha ina kila aina ya machaguo unayo taka kwa wale wenzangu na mimi ambo mb kwetu ni shida basi hii app ndio yenyewe.

Pia unaweza kuangalia Movie hapo hapo online.
Picha hizo hapo chini.

Hapo nimeweka kuanzia unapo ipakua app kutoka Google mpaka hatua ya mwisho una Download move yako.

View attachment 1442668View attachment 1442669
 
Admin wa group hili mkaksi kweli, ila tutafanyaje tunataka burudani.
hiyo link bado ipo active.


kwa wale wanaosema wanadownload na hawaziona zilipojisave, au wale wanaosema ina load tuu bila kushusha mzigo...

cha kwanza hakikisha device yako ina nafasi yakuweza kupokea mzigo huo na nafasi nyingine ikabaki.

pili unadownload movie huwa inajifgicha ktk folder la telegram lililojificha sana kiasi kwa mtumiaji wa phone ambaye hayuko smart sana itampa shida, japo kuna option ya kusave katk galery baada yakua imeshashuka ila kitakachofanyika utakua una movie moja mara mbili iliyopo mafichoni na hiyo ya kwenye galery!

chakufanya ingia kwenye file/folder system... then folder la Android.... then Data.... then org.thunderdog.challegram, humo ndio kuna kila ulichokidownload kutoka telegram then uta cut na ku paste upatakapo.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wafanya biashara hapa mmepiga sana pesa hii kitu inauzikaaa


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Me naonaga bora nikatoe buku au buku mbili niweke movie nijikate kuliko kuangaika na kudownload ndo maana wanaomba link sjawajibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 



Alibarikiwa pesa nyingi akanyimwa uhuru wa kuzitumia..jela ikamuamrisha atoe amri akiwa nyuma ya nondo..ni tajiri haswa,maadui lukuki na watumishi wanaotii...

mahajan akaamrisha mtoto wake awekwe kwenye uangalizi wa hali ya juu mpaka yeye atakapotoka jela...

...haikuwa hivo..

...Kosa moja la kukosa umakini lilimsafirisha mtoto ovi kutoka india mpaka bangladesh..mikononi mwa adui mkubwa wa babaake..chini ya himaya ya nusu mtu nusu shetani...

babake kama ni don wa india...huyu ni mwasisi wa waasi wa bangladesh...taarifa ikamfikia mahajan akiwa jela na amri akatoa...hata kwa gharama ya kitovu cha nchi..alimuhitaji mwanae kwa lazima...

.....Picha likaanza....

...Ni tayler rake..black-market mercenary and former Australian Special Air Service Regiment soldier..
mtu aliepoteza kila kitu kwenye maisha yake na kubaki yeye na pumzi..wawili tu...

mke asiejua alipo na mtoto aliekufa kwa pumu..vilimfanya aamue kuishi maisha yake..yasiyoogopa kufa..

...Ni mafia wa kukodiwa...kazi inayohitaji liende jeshi..alienda yeye..bunduki ilikuwa inakubali kutii kila analosema na vita ndo maisha aliyochagua..

akawekewa pesa mezani..akapewa wajibu wa kumrudisha mtoto ovi kwa babaake...mwanaume akaingia kazini..

...Ni bangladesh ndipo tyler alionja uchungu wa ugumu wa vita...alimpata mtoto lakini hakurudi na mtoto...

Aliamini kwenye pesa...akaamini kwenye uwezo wake wa mapambano...Alipofanikiwa kumpata mtoto..akafanikiwa kujua kuwa amezungukwa kwenye pesa na wanaotakiwa kumlipa...

...Tyler hajui amuache mtoto aondoke yeye...au awe na huruma japo pesa kaikosa... mji umewekwa lockdown..

Hakuna mahali pa kupita yeye bila kujulikana...Alihitajika akiwa hai..na jeshi ndo lilichukua dhamana ya upatikanaji wake...

tyler alihitaji kuwa mwanajeshi kweli mbele ya jeshi la waasi...ni mtu mmoja dhidi ya nchi nzima...

....Akafunga mkanda akamwamrisha mtoto ovi amuamini...mtoto alipojua yupo kwenye mikono salama akakubali kusikia risasi zikipishana mbele yake...

tyler kaamua ni yeye afe...mtoto afike....

..ilipigwa vita ya karne..

..Chris Hemsworth anapoionesha dunia kwanini yeye ni msanii wa pili kulipwa pesa nyingi duniani kwenye filamu..

....Moja kati ya action movie ya mwaka 2020 isiyochosha...
...#Latest movie 2020..lets go
...#EXTRACTION..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…