Mimi nadhani tatizo letu kubwa zaidi ni kukosa uzalendo.Kuna stori flani ya kuchekesha hapo zamani kuhusu Mkenya na Mtanzania.It goes like this: Kulikuwa na wakandarasi watatu wa mradi wa ujenzi wa daraja.Ilipofika wakati wa kuonyesha mafanikio ya mradi huo Mkenya akaonyesha daraja na bangaluu moja la haja.Akadokeza kuwa licha ya kufanikisha mradi huo,yeye nae amenufaika kwa kujenga kibangaluu chake.Mwingine (again,sikumbuki ni Mkenya au Mganda).Ilipotimu zamu ya Mtanzania,hakukuwa na daraja wala nini bali bonge la bangaluu na vimwana kadhaa.Akajigamba kuwa hela yote ya mradi imeishia kwenye masuala yake binafsi.It's a joke that makes sense.
Kenya kuna rushwa na ufisadi kama ilivyo sehemu nyingine za Afrika na dunia ya tatu kwa ujumla.Lakini angalau wenzetu wanaweka uzalendo mbele katika baadhi ya maeneo.Hao waliopewa mradi wa kuitangaza Kenya watakuwa wamefisadi kidogo lakini angalau wametekeleza jukumu walilopewa.Huo mradi wa matangazo ya London ukiambiwa namna unavyonufaisha watu badala ya nchi utatamani kulia.Kuna watu wamefanya mradi huo kuwa full time jobs zao sio kwa vile wako effective katika fani hiyo bali kuwakilisha maslahi yao na wanaowapa tenda hiyo.
Zimeshafanyika conferences kadhaa hapa London zenye lengo la kuwavutia wawekezaji na kuwashawishi wazawa wachangie uchumi nyumbani.Yetu ilijaa hadithi nyiiingi lakini ukiangalia,kwa mfano,ya Rwanda,usingeshindwa kubaini kuwa hawa wenzetu sio tu walikuwa wamejiandaa vya kutosha bali pia walikuwa wanatekeleza mission iliyo deep in their hearts.Ni vijana wadogo tu ambao kwa hakika wangeweza kum-impress any UK-based Rwandan graduate arudi nyumbani kuchangia maendeleo ya nchi yake.
Angalia msafara wa JK na watalii waliokwenda USA kama delegation ya wafanyabiashara.Yaani mpaka mission town nao walijumuishwa (pengine katika jitihada za kuonyesha kwanini nchi yetu inaitwa Bongo).Wajanja wakachangamka chap chap kutengeneza websites ili waonekane wafanyabiashara halisi (rafiki yangu mmoja alidakishwa pounds kadhaa kumtengenezea website ya chap chap mjanja mmoja aliyepata mwaliko wa safari ya US na JK).I was once told kwamba akina Kinje waliwahi kupewa tenda ya kuwa-encourage vijana wa Kitanzania warejee nyumbani kujenga taifa.One couldnt be serious!
Bila uzalendo,hata tukileta watalii wangapi tutaishia kuwa masikini zaidi na akina Severe (sijui yuko wapi siku hizi) wataendelea kunufaika hapo Maliasili na Utalii.Si mnakukumbuka Mkutanom wa Sulivan ambapo Waziri Mwangunga alijiumauma katika kutoa presentation pale alipoulizwa kuhusu suala la ujambazi dhidi ya Watalii?Na alikuwa na takriban mwaka mzima wa kujiandaa kwa ajili ya shughuli hiyo.
Tanzania ni kituo kizuri sana kwa "watalii" wanaokuja mikono mitupu na kuondoka na mamilioni ya dola.