Ezekia Dibogo Wenje anajua sana, ni mwanasiasa Smart

Ezekia Dibogo Wenje anajua sana, ni mwanasiasa Smart

Chetikungu

Member
Joined
May 22, 2018
Posts
15
Reaction score
29
Naenda moja kwa moja kwenye hoja ya msingi,

Hivi umejaribu kutumia hata dakika tano kumsikiliza huyu jamaa anaitwa Ezekia Wenje Mbunge Mstaafu wa CHADEMA wa jimbo moja huko Mwanza, jamaaa anajua na anajua tena. Jamaa akiwa anaongea unaona hadhira wanatulia kama wamemwagiwa maji, anajua jinsi ya kutengeneza hoja na kuitetea anaijua Tanzania vizuri anakupa data anakupa na alternative.

Jamaa alikua Canada kwa kipindi cha miaka miwili nadhani, ameenda kupata exposure kubwa sana na kujifunza mambo mengi, huyu akipewa mikutano akazunguka nchi njima imapact yake ni kubwa sana, ukisikiliza mkutano wake lazima utoke na akili tofauti kabisa.

Kuna haja ya CHADEMA kumtumia vIzuri na ukizingatia chama kimeanza kupokea ruzuku, hivyo wataweza kufanya mikutano mingi ya kutoa elimu ya uraia na kuwafikia wengi zaidi.

Wenje ni asset ya chama anatakiwa kutumika vizuri.
 
Wenje umekuja kujianzishia thread?
Eti smart.... hahahaha
 
Wenje ndivyo alivyo, siku zote ni mtaratibu haongei kwa sauti ya juu kama wengine, hoja zake anakuletea taratibu kwa mpangilio mzuri zinapenya masikioni mwa msikilizaji vizuri, yule jamaa angetakiwa hata awe mchunga kondoo wa bwana.
 
Wenje alikuwa chaguo la Tundu Lissu kama angeshinda awe Waziri Mkuu; Mbowe alikuwa amechagua awe Waziri Fedha (You-Know_Why). Lakini wote wakaanguka chini pu: Tundu 87%-13% Wenje 71%-29% Rorya na Mbowe 88%-12% Hai.
 
Wenje ndivyo alivyo, siku zote ni mtaratibu haongei kwa sauti ya juu kama wengine, hoja zake anakuletea taratibu kwa mpangilio mzuri zinapenya masikioni mwa msikilizaji vizuri, yule jamaa angetakiwa hata awe mchunga kondoo wa bwana.
yah sure siasa yake ni ya kuongelea vitu na sio watu, kuna haja ya wanasiasa wachanga kujifunza kwake.
 
Back
Top Bottom