Ezekiel Kamwaga ni Simba damu!

Ezekiel Kamwaga ni Simba damu!

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,282
Reaction score
117,244
Kwa tunaomjua Ezekiel Kamwaga ni Simba damu na ameshafanya kazi hadi za kujitolea pesa yake mifukoni enzi hizo hakuna cha Mo wala nani.

Kashafanya kazi hadi ya kuwa Kaimu katibu Mkuu, watu wakiwa hakuna timu haina hela.

Wengine watakaokuja kumuita msaliti huko baadae hata Dar hawaijui wanaisikia kwa Radio.

Nimeweka hii thread kama kumbukumbu huko baadae maana yake tofauti kidogo tu za kimtazamo tunakuja kuita watu wasaliti wakati watu hao wanajitolea sana.

Na hao midomo juu kuita watu wasaliti hata mtaa wa msimbazi hawaujui ulipo.

Thread for future use..
 
Mkuu Past Deeds zinakupa Kinga ya Future Deeds za kufanya chochote kile?

Yaani usihukumiwe kwa utakachofanya kesho sababu leo ulikuwa vizuri? Nadhani ustaarabu ni kuhukumu watu kwa kila kitokeacho hapo hapo, vilevile football na vitu vya wengi ni mambo ya passion, you have to take the rough with the smooth.
 
Mkuu Past Deeds zinakupa Kinga ya Future Deeds za kufanya chochote kile ?

Yaani usihukumiwe kwa utakachofanya kesho sababu leo ulikuwa vizuri ?, Nadhani ustaarabu ni kuhukumu watu kwa kila kitokeacho hapo hapo, vilevile football na vitu vya wengi ni mambo ya passion, you have to take the rough with the smooth...
Unaamini watu wote wanaoitwa wasaliti wasaliti kweli?
 
Unaamini watu wote wanaoitwa wasaliti wasaliti kweli?
Hapana wengi sio wasaliti kwanza nadhani wasaliti walikuwepo enzi za vita baridi au vita ambapo mtu anajifanya rafiki kumbe anakuunguza ndani kwa ndani.

Kwa hivi sasa hili neno linatumika kama shield au silaha kwa watu wenye msimamo tofauti... Ila point ni kwamba kwenye mambo ya washabiki au mchezo unaoendeshwa kwa hisia tegemea kulaumiwa vitu vikienda mrama na usitegemee asante vikienda poa...
 
Kwani huko Utopolo nafasi zimekwisha?
Ni Mshabiki wa Yanga ?, Sio lazima uwe shabiki wa timu husika kutambua mchango wa mtu katika soka au tasnia husika..., na jamaa alikuwa chachu katika Soka la Tanzania, ndio maana hata hapa anaongelewa
 
Manara vile viatu vilikuwa vinamtosha barabara au kama vipi wampe position ya mwana-propaganda wa timu..., anyway anaweza akawa mpenzi mtazamaji kama watazamaji wengine walivyo
Awe mtazamaji tu..sis wengine tulikuwa tunahitaji msemaji mwenye akili na elimu. Huyu roporopo hatukumtaka nafurahi hilo limetimia. Wanaomtaka wamfuate huko aliko.
 
Pamoja na uzi wako wa kumuwekea kinga mapema akikubali kununulika kama mwenzie analiwa kichwa tu.
 
Ni ngumu Manara na Management Ya S.S.C Kufanya kazi Kama timu Kwa Kilichotokea. Haya maamuzi Yana faida Zaidi Kwa Maendeleo ya Timu. No doubt Uwezo Wa Kamwaga labda Kwa Wasiomjua. Mwishoni hapa Manara alishindwa Kudhibiti Emotions zake...!
 
Kama nakumbuka vuzuri Kamwaga aliwahi kufukuzwa Simba. Mnaokumbuka mnaweza nisahihisha
 
Ni Mshabiki wa Yanga ?, Sio lazima uwe shabiki wa timu husika kutambua mchango wa mtu katika soka au tasnia husika..., na jamaa alikuwa chachu katika Soka la Tanzania, ndio maana hata hapa anaongelewa
Tatizo alikuja kuharibu mwishoni,alilewa sifa kiasi akawa very unprofessional. Alikuwa na vimeo vingi uongozi ulikuwa unamvumilia tu, yeye akiwa mwandishi wa habari lakini always anagombana na waandishi wa habari tena kwa lugha za kihuni kiasi alikuwa anaichafua brand ya Simba ambayo alishiriki kuiinua.
 
Back
Top Bottom