Ezekiel olochu anatia aibu.

Ezekiel olochu anatia aibu.

Nsele

Member
Joined
Dec 7, 2013
Posts
80
Reaction score
8
Mwenzenu mimi kama Mwalimu naona aibu kuangalia Bunge kutokana na michango mibovu inayotolewa na mwalimu mwenzangu Olochu katika kikao cha bunge. Kweli inaniuma kama yeye ni mwakilishi wetu wa chama cha walimu sidhani kama walimu tutaweza pata haki zetu katika katiba mpya.
 
Toa mifano ya michango hiyo mibovu aliyoitoa huyo Oluochi sijui nani!
 
Kivipi? Mbona mie naona anachangia vyema tu? Ila nahisi ajaifahamu vyema sheria ya mabadiliko ya katiba.
 
mwenzenu mimi kama mmwalimu naonaaibu kuangalia bunge kutokana na michango mibovu inayotolew na mwalimu mwenzangu olochu katika kikao cha bunge.kweli inaniuma kama yy n mwakilishi wetu wa chama cha walimu sidhani kama walimu tutaweza pata haki zetu katika katiba mpya.

Mbona wewe umechangia ovyo? Wewe ayatollah Wa tengeru nani?
 
_73372430_021391240-1.jpg
Weka picha
 
Jamaa jembe sana anachangia point. Haya wewe mwalimu usiyejua kuandika vizuri,tuambie ametoa mchango gani ambao ni mbovu.
 
Mwenzenu mimi kama Mwalimu naona aibu kuangalia Bunge kutokana na michango mibovu inayotolewa na mwalimu mwenzangu Olochu katika kikao cha bunge. Kweli inaniuma kama yeye ni mwakilishi wetu wa chama cha walimu sidhani kama walimu tutaweza pata haki zetu katika katiba mpya.

wewe ndo unatia aibu manake Hueleweki
 
No jamaa mbona yuko poa sana, na mi points kibao yenye facts tatizo anajisahau tu mpaka anaonekana anaboa ni muda tu atatembea poa....

Mwalimu huyu ni kuji control tu but ni poa sana.
 
No jamaa mbona yuko poa sana, na mi points kibao yenye facts tatizo anajisahau tu mpaka anaonekana anaboa ni muda tu atatembea poa....

Mwalimu huyu ni kuji control tu but ni poa sana.

Huyu jamaa yuko safi,namfananisha na Na J.Mnyika.ni mtu mwelewa na binafsi nimemkubali ila Ma sisiem yanaona nongwa tu.
 
mbona anachangia vzuri tuu! labda utupe angalau mfano mmoja tu wa ulchokiona kachangia ovyo
 
Kivipi? Mbona mie naona anachangia vyema tu? Ila nahisi ajaifahamu vyema sheria ya mabadiliko ya katiba.

Ninaomba utulie mwalimu huyu jamaa nilivyomuangalia ni mtu makini hapendi kuona kitu kinapitishwab hivi bila kuhoji uhalali wa kanuni hiyo.
Niombe kwamba uwe mvumilivu kinachoendelea kwa hizi week mbili hadi sasa ni utungwaji wa kanuni zitakazoongoza bunge hili kwenye mjadala wenyewe wa katiba.Nina imani itakapofika kuzungumzia masilahi yenu waalimu nina imani hatawaangusha kuwatetea kuwa mvumilivu mkuu.
 
Huyu Ezekiel nilidhani ni mwanasheria kwa sababu anazungumza kwa umakini, na kuonyesha kuwa anaelewa vizuri masuala ya sheria
 
Ungetuambia amekosea wapi au wewe unataka achangiaje?!
 
Huyu Ezekiel nilidhani ni mwanasheria kwa sababu anazungumza kwa umakini, na kuonyesha kuwa anaelewa vizuri masuala ya sheria

Huyu jamaa ni MWALIMU by kusoma, pia ndio katibu mkuu wa CWT kama sijakosea...

ALisema aitwe mh. mwalimu... weee yule mrembo (nampenda sana kwani ananiii... UMMI MWALIMU alikuja juu kweliii.
 
No jamaa mbona yuko poa sana, na mi points kibao yenye facts tatizo anajisahau tu mpaka anaonekana anaboa ni muda tu atatembea poa....

Mwalimu huyu ni kuji control tu but ni poa sana.

Yeah hata mimi nakubaliana na wewe, jamaa anatoa points nzuri tu, ila sema yuko kama vile amepania achangie sana labda ili ajipatie umaarufu.!
 
Mwalimu olouch ni mchangiaji huru aso na makundi
 
Back
Top Bottom