F-15 Fighter Jet ya IDF almanusura kudakwa na Iran

Sun Zu

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2022
Posts
761
Reaction score
2,115
Ripoti ya Channel 12, kwa mara ya kwanza imefichua hadharani kuwa, ndege ya kivita ya Israel F-15 ilikaribia kutua katika ardhi ya Iran wakati wa vita vya siku 12 kati ya Israel na Iran.

Ndege hiyo ilipata hitilafu ya mfumo wa tanki la mafuta wakati ikifanya kazi ndani ya anga ya Iran.
Rubani alitambua tatizo haraka na kutoa taarifa kwa wakati muafaka.

Vikosi vya Israel vililazimika kutayarisha mpango katikati ya misheni ikiwemo kutuma ndege ya tanki kusaidia ndege hiyo.

Mpango wa dharura ulitayarishwa iwapo ndege hiyo ya mafuta haikuweza kufikia F-15 kwa wakati, ili kuruhusu ndege kugeuza na kutua katika nchi jirani.

Ndege ya kujaza mafuta hatimaye ilifikia F-15 kwa wakati, na kuruhusu ndege hiyo kuendelea na misheni pasipo kutua kwa dharura.
 
mbona hizi taarifa hatuelewi ukweli wake mara kobazi wanaisifia Iran imetungua ndege nyingi za F 35 na wamemshika rubani wa kike sasa ukweli ni upi maana kobazi nao kwa propaganda

Sent from my Infinix X663 using JamiiForums mobile app
 
Chanzo! Au ndio by mimi mwenyewe.
 
Ukisikia watu waswahili hasa basi ndio hao mnaowaita kobazi kwa sababu wao ni watu wa maneno mengi lakini hamna lolote na unafiki kibau.
 
Yale yale ya aliyekua mke wa Manara kumwambia Zungu hadindi ila anakula ma house girl kobazi kuu si alisema hakuna ndege ya Myahudi iliingia anga lake na zilipiga kwa mbali haya hii nayo iliyokua inavinjari huko imefikaje
 
Uongo mwengine mkadanganye watoto wenzenu huko mtaani yaani ndege ijaze mafuta juu ya anga ya iran wakati inajulikana tanker uwezo wake kujificha kwenye rada ni mdogo sn kulinganisha na fighter jet ingetunguliwa dakika 2 tu
 
Yale yale ya aliyekua mke wa Manara kumwambia Zungu hadindi ila anakula ma house girl kobazi kuu si alisema hakuna ndege ya Myahudi iliingia anga lake na zilipiga kwa mbali haya hii nayo iliyokua inavinjari huko imefikaje
HUWEZI kuwa serious mkuu.
Tanker iingie katika anga lenye ADS na isilipuliwe!?
Huu ni uongo kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…