Face to Face with Zitto Kabwe: Kuhusu Kupika Data, "Namheshimu Sana Rais Magufuli ila Sio Mkweli!. Uchumi Umesinyaa!.

Pasco umeamua kuwatukana watanzania yaani rais ni mzazi wa wananchi wa Tanzania?
 
Kukubali na kushangilia kila kinachosemwa na wakubwa wa Lumumba ndiyo ilani ya chama chao
 
Mtani asante sana. Umempa Mh. Zitto nafasi nzuri ya kujieleza. Na kama mwanahabari nguli hukumuingilia katika maelezo yake.

Mimi sio mwana-habari lakini najiuliza, Mh. Zitto anataka kutueleza nini hapa (what is the NEWS content)?

Serikali imetuambia kitu kimoja na yeye anatuambia kingine. Serikali inatuambia uchumi unaimarika na yeye anasema uchumi unasinyaa. These are finer points for the Economists to ponder.

Je, kutokana na mchakato wake:
☆ Serikali imeiba hela za wananch?

☆ Kuna mchezo mchafu unaofanywa na serikali kuwadhulumu wananchi?

☆ Serikali ina malengo maovu juu ya wananchi wake kutokana na matamshi yake?

☆ Na mengineyo mengi.

Kama serikali inajaribu kwa uwezo wake wote kuwahudumia wananchi wake na kuleta maslahi mema ya taifa letu, kwa nini Mh. Zitto anajaribu kuivua nguo (embarrass) hii serikali?

Kuna mengine mengi ya kujiuliza. Kama anachosema ni kweli:
* Anataka serikali ifanye nini sasa?

* Kuna kitu tofauti ambacho kingepaswa kufanyika nchini hapo nyuma kama anachosema kingejulikana awali?

* Ni kitu gani tofauti kingefanyika leo kama anachokisema Mh. Zitto kikibainika ni kweli?

Sitaki kukuingilia katika taaluma yako mtani lakini haya ndio yangekuwa maswali yangu kwa mgeni wako Mh. Zitto Kabwe.
 
Naona unauliza majibu sijui swali atauliza nani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…