Yona F. Maro
R I P
- Nov 2, 2006
- 4,201
- 236
Facebook ni aina ya mtandao wa jamii - social network hapo mwanzo ulikuwa zaidi katika kukutanisha watu na kujadili masuala kadhaa au kubadilishana taarifa kutokana na mtu anavyoishi maisha yake ya kila siku siku hizi imebadilika kodogo kwa sababu hata kampuni nyingi duniani zinafungua kurasa zake huko kwa ajili ya mashabiki wao wau wateja wao waweze kuuliza maswali au kuwasiliana nao kwa njia ya kijamii zaidi , hata wanasiasa siku hizi imekuwa rahisi sana kujua watu wao kwa njia ya mtandao kutumia facebook zaidi ya ilivyokuwa kwenye blogu na huduma zingine za mawasiliano mtandao -- kwahiyo facebook ina faida zake tena nyingi sana watu wanaweza kufaidika sana kibiashara kama wakipata ushauri mzuri na jinsi ya kuwekeza katika utangazaji au utafutaji wa matangazo ya mitandao kama facebook .
Tatizo lake kubwa ni moja kwamba watu wengi haswa wengine huwa wanaweka taarifa zao binafsi humo na wengine wanaweza kuona na kuzichukuwa kwenda kutumia kwingine bila ruhusa za wenye mali hizo nadhani mnakumbuka enzi ya zeutamu , wengine wanaingiza taarifa potofu kutumia picha na profile za watu bila ya wao kuwajua na mambo mengine kama hayo