Facebook ni nini?

Facebook ni aina ya mtandao wa jamii - social network hapo mwanzo ulikuwa zaidi katika kukutanisha watu na kujadili masuala kadhaa au kubadilishana taarifa kutokana na mtu anavyoishi maisha yake ya kila siku siku hizi imebadilika kodogo kwa sababu hata kampuni nyingi duniani zinafungua kurasa zake huko kwa ajili ya mashabiki wao wau wateja wao waweze kuuliza maswali au kuwasiliana nao kwa njia ya kijamii zaidi , hata wanasiasa siku hizi imekuwa rahisi sana kujua watu wao kwa njia ya mtandao kutumia facebook zaidi ya ilivyokuwa kwenye blogu na huduma zingine za mawasiliano mtandao -- kwahiyo facebook ina faida zake tena nyingi sana watu wanaweza kufaidika sana kibiashara kama wakipata ushauri mzuri na jinsi ya kuwekeza katika utangazaji au utafutaji wa matangazo ya mitandao kama facebook .

Tatizo lake kubwa ni moja kwamba watu wengi haswa wengine huwa wanaweka taarifa zao binafsi humo na wengine wanaweza kuona na kuzichukuwa kwenda kutumia kwingine bila ruhusa za wenye mali hizo nadhani mnakumbuka enzi ya zeutamu , wengine wanaingiza taarifa potofu kutumia picha na profile za watu bila ya wao kuwajua na mambo mengine kama hayo
 
facebook ni mtandao wa kijamii..
kupita mtandao huu unaweza kuunganishwa na watu ulikuwa unafahamina nao au ambao unafahamiana nao na kujulisha habari za kijamii.
watu wengi sasa wamekuwa wakitumia mtandao huu na wengi wao wamekuwa mateja wa mtandao huu maana kuna nafasi ya watu wengine kuandika chochote kile walichonacho kwenye mawazo yao na hicho kitu kuwa kikionekana kwenye kurasa za kila ambae ni rafiki wa mtu huyo.
kwa kweli mtandao huu unafahamika sana na hii imepelekea wenyewe kutumiaka hata kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mkuu..
nadahani nimeskusaidia kiasi, usisite kuuliza zaidi kama unapata taabu na mtandao huu..
ila kwa kujua zaidi unaweza kujisajili kwenye Welcome to Facebook ili uweze kufhamu zaidi na usipo pendezwa nayo sana unaweza kujitoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…