Akiliccm, ni kudhani matumizi ya mabavu yanaweza kunyamazisha watu!
Walipiga watu mabomu ya machozi na virungu... watu wakanyamaza...
Wakaiba kura na kutengeneza matokeo walivyotaka kura watu wakanyamaza...
Wakang'oa watu meno... watu wakanyamaza...
Wameendelea kutishia watu silaha za moto na vitisho vingine... watu wamenyamaza...
Mauaji ya viongozi wa serikali na askari yasiyo na majibu.. watu wamenyamaza...
Utekaji na uvamizi unaoendelea vitatufikisha wapi? Je watu watanyamaza hadi lini?
Wanadamu hususan katika nchi zetu hizi hukata tamaa! Je kabla hawajakata tamaa nini kinafanyika kuzuia matukio ovu yatakayopelekea hali ovu kutokea?
Watu waovu hushabikia uovu ambao mwisho wa siku pia wao hauwaachi salama!