Elections 2010 Fact: Church, the Force Behind CHADEMA's Popularity; will the holy union last longer?

Elections 2010 Fact: Church, the Force Behind CHADEMA's Popularity; will the holy union last longer?

Status
Not open for further replies.
Awe Mkristo au Mwislamu ;Hivi kwani lazima CCM iongoze jamani? Tumewachoka na hawana kipya tunataka mageuzi uongozi wa kimazoea hatutaki

Usiangaike na huyu jamaa inavyoonekana ana mawazo mgando,na mbaya zaidi ameadhiliwa sana na historia!
 
Kibaraka
Please, ondoa hiyo avatar. Binafsi, inatonesha madonda ya moyo!! Sijui kwa wengine..
Huyo ni jambazi na mbakaji namba tatu wa demokrasia. Nadhani namba 1&2 wanafahamika kwa waTz karibia wote sasa.
 
Kumbuka kwamba, mambo yaliyohusishwa na ufisadi katika awamu ya Kikwete ndiyo yalisababisha Edward Lowassa ambaye ni mkristo akaachia ngazi kwa mara ya kwanza tangia uhuru kwa waziri mkuu kuondoka madarakani kwa jinsi hiyo. Vita ya ufisadi si vita ya kidini kwa wanatuhumiwa hadi leo baadhi yao ni wakristo waliosombwa na upepo wa tuhuma hizo, kama vile Chenge.

NI kweli ufisadi uliofanyika awamu ya tatu ya Rais Mkapa umeleta majeraha makubwa kisiasa kwa Rais Kikwete na hilo halina ubishi lakini mkapa naye hakusalimika katika kashfa ya Kiwira na biashara zingine hadi akajadiliwi bungeni. Kilichomsaidia Mkapa kashfa hizo zimejitokeza akiwa hayuko madarakani ambapo Rais Kikwete amejikuta anabeba lawama zote za serikali ya awamu ya tatu na nne na kuwa mzigo mzito kwake kuubeba. Ni jambo la kawaida hata pale Mwinyi alipobeba mapungufu yaliyojitokeza katika serikali ya nyerere, na Mkapa akabeba matatizo yaliyojitokeza katika serikali ya Mwinyi.
 
Bila kuuma uma maneno, ni ukweli usiopingika kuwa kanisa limetoa mchango mkubwa katika kuifikisha CHADEMA hapa ilipo leo hii.
Umaarufu wa CHADEMA uliongezeka mara dufu kufuatia kanisa kutoa 'waraka' ambao jamii ya kikristo iliutafsiri vema.
Najua kuna watu watabisha kwa nguvu zote hili lakini ukweli utabaki kuwa huo. Kisingizio kuwa CHADEMA kina viongozi imara sasa hakina ukweli kwani ni viongozi hawa hawa waliokuwepo 2005 na mwenyekiti Mbowe aligombea urais.
Pia hoja ya ufisadi ndani ya CCM haina nguvu sana kwani ufisadi mwingi ulifanyika kwenye awamu zilizopita mbona CDM haikupata umaarufu huo?
Nadhani directly au indirectly kanisa liliamua kuiadhibu serikali ya awamu ya nne kwa kuvunja 'memorundum of understanding'

Mimi hofu yangu ni come 2015 elections, CCM wana turufu ambayo kama wataitumia na wameiweka kimkakati, political landscape in TZ will not be the same. Turufu yenyewe ni CCM kumsimamisha mgombea wa urais mkristo.
  1. Kanisa litaacha 'holy union' na CDM ili kufufua memorundum of understanding na serikali ya huyo mgombea?
  2. Waislamu ambao sasa wanaunga mkono CCM wataendelea kukiunga mkono ili kulinda maslahi yao?
  3. Wale walioenda CDM kwa wito wa kanisa watabaki huko, au watarudi kutetea maslahi serikalini?


1. Mbona unajihami kwamba kuna watu watabisha,hujiamini? au unadhani hoja yako haina mashiko?
2. Unasema viongozi hawa hawa waliokuwepo 2005 na mwenyekiti Mbowe aligombea urais,kwa hiyo na 2010 mbowe aligombea uraisi au?au mbowe aligombea pia ubunge 2010?
3. kwani unaona inawezekana umaarufu wa CDM uwe backdated to 2005,kwa hoja walizozivumbua 2010? au kama wewe hukula usiku wa jana,ukipata leo msosi wa mchana,utaliambia tumbo 'lunch hii iwe mbadala wa dinner ya jana? kumbuka decisions taken now,are irrelevant for past actions.shule ulipitapita walau?
4. By the way,waislam na wakristu si mambumbumbu kama wewe kiasi cha kuchagua viongozi kwa sababu ni mwislam au mkristu.Hiyo ni idea yako personally
5.mbona waislam hawakua na wazo kama lako la kulinda maslahi yao 2000,walipomchagua mkapa,au wakristu hawakulinda maslahi yao kwa kumkataa JK 2005?
6.Kanisa katoliki hutoa waraka kila chaguzi,mbona CDM haikua maarufu nyakati hizo ambazo pia kanisa lilitoa nyaraka? By the way,ulibahatika kuona waraka huo achilia mbali kuusoma.
 
This kind of flimsy extremism alkaeda type of ... endelea kulala fofofo tu.
 
CCM ni chama kilichokomaa mwaka 2015 hakitasimamisha mtu kwa msingi wa dini yake bali kwa sifa zake, Rais ajaye anaweza kuwa mwislamu au mkristo lakini hiki sio kigezo cha kuchagua wagombea ndani ya CCM ingawa kila mgombea ana dini yake kikatiba.

kwa kutambua kwamba Marais watakaokuja baada ya kikwete na baadaye zaidi wanaweza kuwa waislamu au wakristo hatuna haja ya kugombania dini sasa wakati nchi itaendelea kuendesha chaguzi mbalimbali. Watu tunakufa lakini taifa litaendelea kuwepo hadi siku ya kiama kwa wale wanaoamini hivyo na taifa halitakuwa na mwisho kwa wenzetu wasio na dini....wapagani.
 
Ndio maana kuna wakati nawapenda sana wenzetu wapagani. "Dini" yao ya upagani inaleta sana amani duniani hawana matatizo na dini za wengine, wenyewe ni kama wapo lakini hawapo lakini kumbe wapo.
 
Ni kweli maana tulishuhudia viongozi wa Kanisa wakimtetea Slaa kwa kitendo cha kuiba mke wa "Mtu"
 
Sipendi mada hii kabisa. suala la nani kuchagua chama gani au nani kamsaport nani katika uchaguzi uliopita si jambo la muhimu kwa sasa.
Ila nasikitishwa na baadhi ya SMS ambazo zilikuwa zikitumwa na watu mbalimbali zikiwa na malengo tofauti.
mfano ni SMS hii.

"SMS TOKA MEZA KUU; WAPENDWA KATIKA BWANA: WAKRISTO, MAASKOFU WAMEPINGA UCHAGUZI MKUU KUFANYIKA JUMAPILI, CHADEMA WAMETUUNGA MKONO, HILO NI JAMBO LA BARAKA NA PIA KURA ZETU HAKUNA KUIPA CCM YA KIKWETE ANAYEWADEKEZA WAISLAM WENZAKE KWA KUWAPA VYEO,OIL NA MAHAKAMA YA KADHI, TUKIJIPANGA TUTAING'OA CCM WANI KURA ZA WAISLAMU WENZAKE ZIMEGAWANYIKA CUF NA CCM, WENGINE WANAPINGA KUPIGA KURA NA HILO NI BARAKA KWETU, TUZIDISHE MAOMBI KWA KRISTO MUNGU MKUU NA MWOKOZI WETU ILI KIKWETE NA WAISLAMU WAZIDI KUGAWANYIKA. MUNGU WABARIKI WAKRISTO, MUNGU IBARIKI TANZANIA"

Nilishtuswa na SMS hii pengine nikasema huenda inatoka Usalama wa taifa. lakini nikawa nasikia MIITO mingi kutoka Makanisani eti Tusichague Chama bali Tuchague MTU. Nikajisemea, Huenda SMS ile ni Kweli.

Ninaye babangu mdogo: yeye ni Mkristo. baada ya kutoka Kupiga Kura alisema; NIMESHAUA! mshenzi yule harudi Madarakani!

Nikajisemea Moyoni "NI MUNGU GANI ANAYEWEZA KURUHUSU MWASHERATI KUONGOZA NCHI??". SI TUNAKARIBISHA LAANA???
 
Sipendi mada hii kabisa. suala la nani kuchagua chama gani au nani kamsaport nani katika uchaguzi uliopita si jambo la muhimu kwa sasa.
Ila nasikitishwa na baadhi ya SMS ambazo zilikuwa zikitumwa na watu mbalimbali zikiwa na malengo tofauti.
mfano ni SMS hii.

"SMS TOKA MEZA KUU; WAPENDWA KATIKA BWANA: WAKRISTO, MAASKOFU WAMEPINGA UCHAGUZI MKUU KUFANYIKA JUMAPILI, CHADEMA WAMETUUNGA MKONO, HILO NI JAMBO LA BARAKA NA PIA KURA ZETU HAKUNA KUIPA CCM YA KIKWETE ANAYEWADEKEZA WAISLAM WENZAKE KWA KUWAPA VYEO,OIL NA MAHAKAMA YA KADHI, TUKIJIPANGA TUTAING'OA CCM WANI KURA ZA WAISLAMU WENZAKE ZIMEGAWANYIKA CUF NA CCM, WENGINE WANAPINGA KUPIGA KURA NA HILO NI BARAKA KWETU, TUZIDISHE MAOMBI KWA KRISTO MUNGU MKUU NA MWOKOZI WETU ILI KIKWETE NA WAISLAMU WAZIDI KUGAWANYIKA. MUNGU WABARIKI WAKRISTO, MUNGU IBARIKI TANZANIA"

Nilishtuswa na SMS hii pengine nikasema huenda inatoka Usalama wa taifa. lakini nikawa nasikia MIITO mingi kutoka Makanisani eti Tusichague Chama bali Tuchague MTU. Nikajisemea, Huenda SMS ile ni Kweli.

Ninaye babangu mdogo: yeye ni Mkristo. baada ya kutoka Kupiga Kura alisema; NIMESHAUA! mshenzi yule harudi Madarakani!

Nikajisemea Moyoni "NI MUNGU GANI ANAYEWEZA KURUHUSU MWASHERATI KUONGOZA NCHI??". SI TUNAKARIBISHA LAANA???
Fabrication in full force!
Mbona usiitoe wakati wa vuguvugu?...Mwongo sana wewe...MDINI...WA KUOGOPWA KAMA UKOMA!
 
Hii yote ni baada ya ccm kuishiwa majibu ya matatizo yanayotukabili kama taifa,sasa wameamua kutumia suala la udini ili kutuvuruga.Washindwe!
 
Mchochoze yeyote ni sawa na Muuaji na Mungu atamwadhibu, Waislamu na Wakristu ni ndugu na tumekuwa tuiishi vizuri kabisa kwa kushirikiana,
Tanzania itashinda kwa nguvu ya Mungu majaribu yote ya watu wenye nia mbaya na Taifa, tutashinda na tutasonga mbele, Husipoteze muda kuchochea hisia za Kidini, Kila wakati Tanzania itaongozwa na either Mkristu au Muislamu au mtu wa dini nyingine yeyote na Nchi itaendeshwa kwa misingi ya Katiba na pale tutaopoona mambo hayaendi sawa basi serikali itakoselea bila kujali ni kiongozi wa dini gani yupo madarakani, Yeyote anayeongea hisia za upendeleo za dini moja wapo kisimsing hajui hata twakimu halisi ia Idadi wa Waislamu au wakristu kiasi cha kuamini dini moja itaweza kuingiza mtu madarakani peke yake ikiwa dini nyingine ita oppose,
 
suala la memorandam of understanding lilianza wakati wa serikali ya awamu ya pili ya Rais Mwinyi.... i stand to be corrected.... Mzee wetu Mwinyi alilikubali kwa sababu halikuwa ombi la kuibagua dini moja inufaike na mapendekzo hayo. suala hili lilihusu mapendekezo ya kanisa katika kupata unafuu wa vifaa na huduma zinazotolewa na taasisi za dini zote kwa minajiri hiyo sio dini moja. Pendekezo hili lilijengwa katika hoja kwamba, kama taasisi za serikali kama shule na mahospitali zinapata unafuu kwa nini taasisi za dini zisipate unafuu huo wakati zinatoa huduma ambazo kimsingi zilitakiwa kutolewa na serikali kwa wananchi wake.

Msingi wa lawama wa memo hiyo unajengwa katika ukweli kwamba taasisi za wakristo zina vitega uchumi vingi kuliko taasisi za waislamu kwa sababu hiyo mapendekezo hayo yangekuwa na manufaa zaidi kwa taasisi za wakristo kuliko zile za ndugu zetu waislamu kama vile mashule, vyuo na mahosptali. Lakini ieleweke kwamba, ukitembea mashule na vyuo utakuta wanafunzi wa dini zote mbili japo kwa uwiano tofauti. kwa mifano michache tu, ukitembelea hosptali za kanisa kama vile KCMC na Bugando utakuta wagonjwa waliolazwa au kutibiwa huko ni waislamu na wakristo.

Mimi nafikiri malalamiko ya waislamu yangejengwa katika hoja kwamba, wao wanakataliwa kujiunga na shule na vyuo au kutibiwa hospitali za kanisa kutokana na imani yao jambo hili ni kinyume na katiba, taratibu na kanuni za kuanzisha taasisi hizo.

kumbuka gharama za vifaa na huduma zikipanda katika taasisi za dini hazitakuwa na athari kwa wakristo tu bali na waislamu pia wanakwenda kupata huduma hizo.
 
hivi hujui hii jarida ni la chadema kuwa macho , huoni watu hawachangii tena wanawaachia wajiulize na kujijibu wenyewe usipoteze muda wako
 
Neno liandikwalo mchangani, likirudiwa rudiwa hukomaa na kufanya mwamba, naogopa sana haya mambo ya kusema udini yakirudiwa rudiwa basi ni lazima haya yatatokea! na ninaiogopa sana siku ile haya yatakapokuja kuwa kweli, eeeh Mungu muumba mbingu na ardhi tuepushe na kikombe hiki, si kwa mapenzi yangu bali kama upendavyo wewe!
 
Hapo ndipo kwenye tatizo. Watu hawa hufurahia ku-associate vyama vingine na udini kwa lengo la kuvi-discredit. Lakini hawana ujasiri wa kukubali ukweli ambao mpaka sisi huku wilayani tunaujua. Nasema, Church deserves credit for the CHADEMA's popularity. Hamuwezi kulinyang'anya kanisa haki yake hii,limefanya kazi kubwa.
Issue ilikuwa political dyamics, come 2015 kama CCM watasimamisha mgombea urais mkristo. Na CCM hawatakosea katika hili, what will happen to church-led CDM supporters?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom