FACTS 11: Kama wanasayansi wangesoma BIBLIA, Technology ya sasa ingekuwa Zamani Sana

Soma Mwanzo1:28 linganisha na dhumini la hao jamaa Mwanzo11:4.
Kutokea hapo ndipo watu wakatawanyika duniani na brain zao kukua zaidi. Jaribu ukiwa umerelax mkuu. Read Bible You will never be the same again
 
Hapa mkuu kuna vitu vya kujifunza vingi kama Building ground kabla ya kujadili hiki ulichokileta(BIBLE(which inspired scientists) and Religious sect).
1:History of reformation Hasa kipindi cha Luther 1517–1521
2:Situation of the church that time of reformation
3:Formation of Jesuit order by ignatus loyola during reformation (spanish 1495 -1556)
4:The greatest war ever fought in history of europe (Thirty years war 1618-48)
5:The age of reasoning/ The enlightenment(1685-1815)
6:Industrial revolution 1760 -1840


Vyote hivyo vipo kwa mfuatano na vinaushawishi mkubwa kwa tunachojadili na Utagundua kwa upana hakuna uhusiano na USOMAJI WA BIBILIA ninaouzungumzia kwenye bandiko hili.

Mfano Huyu Bruno pamoja na Galileo wote walikuwa wanaresearch kile ambacho Copernicus alikiasisi. Lakini wote watatu walikikuwa inspired not by Church but Bible and its recommendation of studying nature. Kulikuwa na Vita vya kisayansi kati ya hawa na Pro-aristosle kama nilivyoongea mwanzoni huko. Chochote ambacho kingeonekana ni Uzushi na kuhatarisha uwepo wa organization ilikuwa ni kosa la kifo. Wengi waliuwawa sio kwa sababu ya Sayansi bali Hofu ya watawala(Kanisa) wanashindwa kuwatwala watu kama kirahisi tena wakianza kusoma bibilia wao wenyewe. Kuna reliable sources zinazosema sababu ya kuuwawa Huyo Bruno inawezekana isiwe tu kama unavyosema maana mbona Gallileo alisema hivyohivyo na akaongezewa mshahara na pope, lakn pro-aristotle scientists kwa kuona kijicho waliwashawishi wengi watawala ili aonekane anaeneza uzushi. Wengi waliuwawa Sio kwa kupinga bibilia bali kwa kupingana na taratibu za kanisa la kirumi. Usomaji wa bibilia kwa watu binafsi ulikuwa unahatarisha uwepo wa kanisa maana mambo mengi yalikuwa yanahojiwa. Ila wengi bibilia iliwafungua kichwa. Copernican was a creationist.

Mfano:Michael Servetus he studied bible at its orgin language which inspired him in his career. Remember he participated in protestant reformation.

Hoja ni BIBLE AND SCIENTISTS sio SCIENTISTS with the church affairs and interests or Scientists who were against Greece philosophic ideas. Nilijitahidi kuwa makini nisiingize taasisi wala chochote katikati ya Bibilia Na Scientists na hapa ndipo tunapojadili tena most of them creationsist.


Tuanzia hapo kwanza. Pitia zile Hints 6, ndio utajua what was going on in europe mida hiyo
 
Nimeweka mpaka mzuri kabisa (Scientists na Bibilia), Madhehebu ya dini mengi wenda walitumia bibilia kama kofia, au kwa kuhofia kuathiliwa na mabadiliko. au Kuwahukumu kwa uzushi bila kufanya deep analysis na invenstigation sijui. Ila Mimi nipo kati ya Bibilia na Wanasayansi walivyogundua hazina nzito ndani ya bibilia na nature. Hapo walichomwa moto wengi tu sio wanasayansi, Hata bibilia haikutakiwa kumilikiwa au kusomwa na mtu binafsi maana iliaminika kasisi ndio mwenye uwezo wa kutafsiri. Kila aliyeisoma aligundua vingi vilivyokuwa either havisemwi na wakuu au Viko kinyume. Martin Luther aligundua haki inapatikana kwa imani sio kama wanavyofundisha haki kwa matendo akaonekana mzushi na muasi. Ila wanasayansi wengine Walionekana hicho walichogundua tena wengi wakiwa inspired by bible kitasababisha hayo maeneo yasitawalike. Hii likuwa ni hofu tu ya kupandikizwa au kutokuju. Na pia hii ilikuwa sio kweli walikuwepo wapinzani wao waliokuwa wakichochea uzushi maana walivyokuwa wanavigundua inspired by bible vilikuwa kinyume na wengi walivyokuwa wanafundishana based on classical Greece philosophies.

Narudia BIBLE AND SCIENTIFIC ACCURACY
 
Hii nadharia ya Vicarius Filii Dei ilitengenezwaje? Maana nilisoma mada fulani humu JF na baadae google nikaona ni jinsi watu walivyopika theory za kupinga RC
 
Ni kazi sana ku convince mtu ambaye tayari amesha made up his mind.

Ni Mungu tu ndo anaweza kuingilia kati..
 
Naona baada ya kukoswa pa kukosoa umejaribu kuja kivingine.
Kwanza sio hayo tu;
1: Elisha alitupa kijiti kwenye maji kichwa cha SHOKA(Chuma kikaelea), UNSCIENTIFIC. Where was g?Archmedes, Floatation principle?
2: Waebrania watatu walitupwa motoni, HAwaKUUNGUA isipokuwa kamba walizofungiwa na Waliowatupa wakafa kwa mionzi ya moto.UNSCIENTIFIC, energy transformation
3:Eliya alichukuliwa na Gari la farasi la Moto likapotea nae Mbinguni kama movie lakini ni kweli.
Upande huo ni Beyond science ndio maana hawawezi wataishia kusema tu yesu alitembea juu ya barafu, wakishindwa wanasema Yesu hakuwepo.UNSCIENTIFIC maana hapa alivunja Gravitation force.

LAKINI KWENYE HIYOHIYO BIBILIA, wakati wasomi magenius wa dunia nzima walipokutana BABELI na kuagiza nyama, Masupu, mavyakulaya kila aina, Daniel, Shedrack, MEshack na abednego wao waliomba maji, Cereals na Plant products kwalipotestiwa hawa wa bibilia walikuwa na akili mara kumi zaidi ya hao waliokula kila kitu, THIS GIVES ROOM FOR SCIENTIFIC RESEARCH AND PREDICTIONS maana This was what God Proposed as food to Human Race before Sin. Kuna mambo ambayo yamesemwa na ni halisi kuhusu ukuu wa Mungu. Mengi saana sana Hayana uhusiano na Miujiza bali ni reality they inspired humble scientists and changed the face of the world. THREAD HII inazungumzia Bible as a tool for scientific innovation and predictions. You can explore What it said and enjoy the reality. Hapa ndipo wanapopenya Evolutionist scientists ambao wao kazi yao kushirikiana na Ethiests kupinga bibilia. Wanashindwa kujua Gregol Mendel founder wa Genetics alikuwa creationists na alivyokugundua kilisababisha wafanye faster kumuokoa jamaa yao Darwin asijekuaibika ndio wakaja na uongo wa genetic-evolution.

Nakushauri tena Soma thread njoo tujadili
 
Hii nadharia ya Vicarius Filii Dei ilitengenezwaje? Maana nilisoma mada fulani humu JF na baadae google nikaona ni jinsi watu walivyopika theory za kupinga RC
Mkuu hii naona ni mambo ya imani na theology. tukiingia huko tutapoteza mwelekeo maana najua kuna watu wanasubiri upenyo tu waingize mambo yao. Hapa tunazungumzia Bibilia its accuracy in many scientific finding and predictions (japo kuna evolutionits scientists wao hata kwa makusudi wako tayari kupindisha ukweli bibilia isionekane iko safi).
Mfano watakwambia wamempima kwa Carbon 14 yule sokwe wa Oldvai Gourge wamemkuta anamiaka Mamillioni wakati Scientifically uwezo wa Carbon 14 kuwepo kwa organism ni kati ya miaka 50000 hadi 60000..
 
Hahahaaa...naona una urge kisiasa sana.

Wewe unalazimisha watu tuamini kwamba Bibilia ingesaidia kuharakisha maendeleo ya kisayansi wakati Bibilia imesheheni mambo lukuki ambayo hayachunguziki kisayansi bali kuamini tu.

Je unaposema Bibilia ingefaa kutumika kama Scientific manual ili hali imejaa mambo yasiyochunguzika kisayansi, una maana kuwa sayansi ingebadili msingi wake wa kutafuta facts kutoka experiments kuja kwenye imani?
 

Sayansi na biblia ni kama East and West. Haviendani kabisa. Katika concepts nyingi na methodologies za interpretation.

Pia katika vitabu vya imani vilivyotumika katika science ni Vedas na Eastern Spirituality. Zimezidi Biblican ideologies katika kuleta elimu. Mfano Tesla alipata wazo la Free Energy kutoka kwa Swami Vevakananda aliyekuwa mwalimu wa kihindi na explorer. Alimpa idea ya free energy exists na Tesla akaweza kuprove kwa kugundua umeme. Akaita kiini cha umeme AKASHA, ni neno la kihindu linalomaanisha the core of energy. Huo ni mfano mmoja wenye ushahidi.

Nipatie ugunduzi au elimu iliyopatikana kwenye biblia, nipatie na jina la mwanasayansi aliyetumia.

Elimu iwe unique kwenye biblia tu, yaani iwe imepatikana kwenye bible tu. Kwa sababu mpaka leo sijaona. Na pia kanisa now days linadanganya kuwa biblia inasema dunia inazunguka jua na inajizungusha na jua ndio centre of the universe na bible imesema hivyo, lakini sio kweli. Christianity haikujua elimu hiyo na ni mojawapo ya dini zilizojua dunia ni flat na inazungukwa na jua. Just like Quran nayo ilivyokosea. Na waliua wengie waliosema dunia ni duara na leo hii mnasema bible said its round. Then why killing of scientists kama biblia ni scientific!

Pia usisahau kuna zaidi ya scientific contradiction 100 kwenye bible.
 
Nimeisoma historia ya Europe vyema sana.

Mwanzoni Church ndio zilikuwa na power kubwa. Archives na antiquities za collections kubwa zilikuwa zinamilikiwa na churches na royal families. Library collections, museum collections, antiquities na pesa walikuwa wanamiliki makanisa. Kulikuwa na sponsorships.

Churches zilikuwa zinalipa explorers kusafiri na kukisanya taarifa. Interests za church zilikuwa ni kufundisha societies mpya walizozigundua. Angalia safari ya Columbus, Vasco na explorers wengi walikuwa wanasafiri mpaka na misalaba na walidhaminiwa na royal families na churches. Hapo ni miaka ya Renaissance period.

Kuna wanasayansi waliokuwa wanasayansi kutokana na kusoma collections zilizopo museum. Mfano early stone tools zilikusanywa na kanisa na angalia theory ya Thunder bold myth. Kanisa lilisema yale mawe yamechongwa na radi. Nakumbuka kuna historia alisema zile ni tools akafukuzwa kazi na alikuwa museum curator. You can search thendebolt myth.

Kuna waliokuwa ndani ya kanisa waliokuwa wanafanya kazi au kuwa karibu na mali za kabisa ambazo ni chanzo cha elimu kama botanical garden, mfano G Mendel.

My point is kanisa ndio lilianza kulea wanasayansi. Lilikuwa linadhamini ili kueneza dini. Pia kanisa lilikuwa na power. Papa alikuwa wa pili kutoka royal families. Watu wakienda vitani lazima ashiriki maamuzi, ndoa za monarchs alishiriki na pia maamuzi makubwa ya states alishiriki. Ilikuwa ni era tu.

Then conflict ikaanza pale wasomi au waliobahatika kutembea maeneo mengi na kujifunza mengi. Kuna explorers waliokuwa wanathaminiwa na church kama Knight of Templar waliporudi waliacha ukristu na kanisa likataka kuwaua na liliwaua wengi na wengine kukimbia nchi nyingine.

Role ya explorers na mercenaries kushikiliwa na kanisa ilikwepo mpaka hata mojawapo wa wazo la Berlin Conference katika sababu za kutawala africa walisema ni kueneza Ukristu waafrika wamjue Mungu wa kweli na kitabu cha kweli.

Wanasayansi hawakuwa wanataka kuanzisha churches mpya. Hawakutaka kupinga bali walitaka Christianity na bible yake vibadilike kuendana na wakati. Kitu ambacho ni kigumu. Ndio maana hata baada ya kabisa kuchoma wanasayansi wengi, waliojificha walikutana pamoja na kuishi kwenye basements lakini mpaka leo hakuna dini waliyoanzisha wao kama wao. Hao kina Luther na Protestant wengine hawakuwa upande wa scientists ni movement nyingine kabisa iliyokuwa kidini.

Threat ya wanasayansi sio kuanzisha movement yao bali kanisa liliona wana logics na itapelekea watu kutoamini biblia na kuanza kutaka kuichunguza zaidi. Biblia ilionekana jibu la kila kitu.

Na angalai kipindi cha Enlightenment period serikali nyingi zilianza kujitoa katika udini na papa kushushwa madaraka na kuwa mtu wa kawaida. Pia serikali na tawala zilizopo zikaona michango ya wanasayansi na kuleta uhuru wa kuamini chochote lakini before hakukwepo na uhuru wa kuamini.

Tawala nyingine zilikosana na papa na kuanzisha mathehebu yake mfano Britain na Anglican.

Hakukwepo na uhuru wa kuamini lakini taratibu kanisa lilipoanza kupoteza power ndipo wakaanza kushuka nguvu na uhuru ukaanza.

Pia hatuwezi kujadili kwanza contribution za bible kwenye sayansi wakati bible ndio kipingamizi mojawapo hata katika historia. Bible followers walijitahidi kuua na kutesa scientists ili wasikubalike. Makanisa yalitumia power waliyonayo na influence yake kushawishi watu kukataa science. Leo hii mtu anakuja kusema science imechangiwa na bible.

Kwa msomi wa historia atakuambia ukweli.


Biblical followers ndio waliochangia science kuchukua muda kukubalika kutokana na kupinga science na kuua watafiti.

Contribution ya Church ni zile collections, utajiri wa mali uliodhamini watafiti, kudhamini explorers, kuanzisha museums, libraries na antiquities. Hizo ndizo positive contribution za church lakini katika idea hawajafundisha lolote ambalo ni scientific. Its much on material support than ideologies.
 
Hata hii novels ungiosoma kujua mengi.



Kuna kitabu cha Trigger "History of Archaeological Thought" niliwahi kuandikia paper ya "From Medieval period to Enlightenment period". Kipo vizuri kufafanua historia ya Europe na scince na role of Christianity, monarchies and scientists. Please soma, nina hard copy. I wish to have a softcopy to share a PDF yake, ila nadhani ipo Google Books you can read free.



Kuna lots of sources you can read.





 
kwa mujibu wa argument yako ulioleta miujiza ili kunullify dhumuni la mada. Mungu anahamasisha wanadamu wachunguze packages za his creative work. hii kazi ingeanza zamani tungekuwa mbali. nikatoa mifano ya hydrology, electromagnetism and telecomunicaton, cosmology, archtectural designing, sea transportation, mfano newton kapatent few constants ambazo zimesaidia revolutions za aironautics na space navigation, wind formation. hata wale brothers waliopatent aircraft invention were creationists trying to explore his creative powers. mbona mambo mepesi unataka kuforce ubishi ili iugurahishe moyo.
 
Bibilia haiwezi kupatana na sayansi kwa maana Bibilia imejaa mambo mengi yasiyochunguzika kitu ambacho ni kinyume na sayansi ambayo ni lazima ichunguze kila jambo.

1.Unakubali kwenye Bibilia kuna mambo mengi yasiyochunguzika?

2.Unakubali kwenye sayansi ili jambo liwe fact ni lazima lichunguzike?
 
Good food of thought.
 
Yaani biblia inatuaminisha kwamba Mungu aliumba kila kitu... in 6 days... embu tukumbusheni/tujulishane ni kama miaka mingapi iliyopita?? Na ni kwanin bible inaassume Mungu aliumba dunia kwanza...mbingu inatafsiriwa kama space... hahaha ninachoshindwa kuelewa... ninachojiuliza, why niamini haya wakati siwezi kuyaprove... inshort hayaingii kwenye akili hata chembe.... Mimi ustaraab wangu ni kwamba nadeal na vile ambavyo vinanizunguka. Ya kale yameshaondoka na wenyewe...
 
Thread yako wataielewa werevu tu lakini wengine wataishia kutusi maana uliyonena yanahitaji mtu kufahamu both SPIRITUAL WORLD AND PHYSICAL WORLD. Barikiwa
 

1.Rudia kusoma thread ndio ujue thread ina maanisha nini. A bible is the sure book for scientific predictions because it provides accurate information which came to be proven scientifically after 3000 years. Haya maelezo hayajumuishi Miracle part of the bible because bible is like a tree with varieties all kinds of good fruits. Leo hapa tunazungumzia sayansi.

2:NIKOLA TESLA:
Kwanza alikutana na Huyo Muhind Marekani akiwa na Miaka kama 38.Huyo jamaa kamkuta tesla akiwa ameshafanya karibu kila kitu, Na yeye ndie aliyemuandikia barua wakutane. Tesla alikutana ili aprove mathematically zile theory za huyo muhindi. Japo zoezi halikufanikiwa lakini walibadilishana Ujuzi kiasi. Ila unapaswa Kumjua Tesla, Kwanza alizaliwa serbia marekani kaenda akiwa kijana mkubwa, baba yake alikuwa Mchungaji, Akiwa mdogo mama yake alikuwa anamuadithia kuhusu Maporomoko ya Niagara, Tesla alifanya imagination ya Turbines zikizunguka kwenye waterfall bila hata kuona waterfall kwa macho akiwa na miaka 9. Alipofika US akakamilisha hiyo project practically na kuwa mtu wa kwanza kuinvent hydroelectric power stations. Na alifika US kama Muajiliwa wa kampuni ya Genera electric alipohamishiwa kutoka branch ya france. Kuita vitu kwa jina la hao jamaa sio kwamba wao ndio waliminfluence. Signal ya kwanza katika first telecommunication tower aliyoidisign alipoipokea alisema amesikia sauti za maraika. Hakuwa na dini kwa sababu 90 ya maisha yake aliishi lab lakini he had bible based background.

3: Ugunduzi wa kibibilia Refer Thread hapo usome utaelewa namaanisha nini. Pia Father of oceanology
Matthew Fontaine Maury he was investigating Psalm 8:8 na kubadili sura nzima ya dunia na Usafiri wa maji.


4:Tunajadili wasomi waliokuwa inspired na bibilia au kuinvestigate and research scientific biblical facts na kuja na findings ambazo zimeisaidia dunia Sio Dhehebu la dini liliwafanyaje hao watu na kwa maslahi ya nani? Kwa sababu hata haohao wayahudi waliokuwa na kila maandiko yaliyomtabiri yesu walimuua haimaanishi maandiko hayakuwa sahihi ila ni upotofu wao kwa kujua au kutokujua. Sasa hawa wote walikuwa watu wa bibilia na wasiokubaliana na Ethiesm na Mauongo ya kigiriki.,
Nicholas Copernicus (1473-1543)
-Copernicus referred sometimes to God in his works, and did not see his system as in conflict with the Bible.
Sir Francis Bacon (1561-1627)
"It is true, that a little philosophy inclineth man’s mind to atheism, but depth in philosophy bringeth men's minds about to religion"
Johannes Kepler (1571-1630)- Aliamini anaweza kupata concepts za trinity katika universe
Galileo Galilei (1564-1642)
Galileo expressly said that the Bible cannot err, and saw his system as an alternate interpretation of the biblical texts.
Rene Descartes (1596-1650)
Rene Descartes and Francis Bacon (1561-1626) are generally regarded as the key figures in the development of scientific methodology.Na huyu alidevelop model ya existence of God.
Blaise Pascal (1623-1662)
Maneno yake wakati anakufa "May God never abandon me."
Isaac Newton (1642-1727)

Aliamini Mungu yuko nyuma ya kila kila kilichopo katika universe, "The most beautiful system of the sun, planets, and comets, could only proceed from the counsel and dominion of an intelligent and powerful Being."
Robert Boyle (1791-1867)
Alifund mapesa mengi kutafsiri bibilia kwenye lugha za kituruki na kiirish, Hiki ndicho alichokisema kuhusu hizo imani za kigiriki watu wanazozihusudu 'the notion that atheism is a modern invention is a myth'
Michael Faraday (1791-1867)
Bible influenced him to Significantly interpret nature
Gregor Mendel (1822-1884)
William Thomson Kelvin (1824-1907)



Albert Einstein (1879-1955)-He wanted to explore how God created this world.
"Science without religion is lame, religion without science is blind."

HIKI ALICHOKISEMA MZEE ALBERT NDICHO NINACHIKZUNGUMZA HUMU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…