Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwenyezi Mungu akipenda inshallah mwezi wa 12(tarehe sitaji) mwaka huu(2019), nitaingia rasmi katika kundi la wahenga. nitatimiza miaka kadhaa ya kuzaliwa kwangu.
kiufupi uhenga sio jambo la kufanyia dhihaka bali ni kitu la kujivunia kwa sababu sio watu wote wa kizazi changu wamebahatika kufika umri ambao mimi nimefika mpaka sasa.
mwaka huu pekee, nimezika rafiki zangu sita ambao wote walizaliwa katika muongo mmoja sawa na mimi.
binafsi najihisi mwenye bahati kuzaliwa katika kipindi ambacho wengine hukiita golden era. ni golden ara kwasababu ni nyakati ambazo dunia ilishudia mapinduzi mengi ya kimziki, sayansi, siasa, tamaduni nk.
na hizi ndio baadhi ya facts kuhusu birthday yangu.
nilizaliwa siku ya ijumaa mida ya alasiri katika moja ya hospital kubwa sana ambayo inapatikana ndani ya jiji moja maarufu hapa east africa.
kwa wale wanaomini katika masuala ya unajimu, nyota yangu ni mshale(sagittarius)
kama nitafika salama au hai katika siku ya birthday yangu, basi nitakuwa nimeishi duniani siku 14,151. pia nitakuwa nimeishi masaa 339,624.
siku niliyozaliwa, rais wa taifa kubwa duniani la marekani alikuwa ni jimmy carter kupitia chama cha democrat.
masaa machache baada kuzaliwa kwangu, mwanamziki nguli wa miondoko ya country duniani, kenny rogers alikuwa anatamba na kibao chake kitamu sana cha lady.
wakati nazaliwa, secret valley ilikuwa ndio movie iliyokuwa inaongoza kwa kutazamwa zaidi duniani kwenye kumbi za cinema.
kwa wale wapenda soka, wiki moja baada ya kuzaliwa kwangu, club ya liverpool iliongoza kwa idadi ya magoli mbele ya aston villa katika division ya kwanza ya ligi kuu ya england.
wakati nazaliwa, john d. rockefeller
ndio alikuwa mtu tajiri zaidi duniani.
nitaongeza facts zingine kadili nitakavyopata mda.