Facts Muhimu kuhusu WCB

Facts Muhimu kuhusu WCB

kombaME

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2015
Posts
2,115
Reaction score
2,818
1. Kuna wanaolalamika eti madogo pale WCB wanalaliwa na Mondi, naomba mjue kwamba WCB ni biashara ya Mondi so yupo pale kumake hela kupitia akina Rayvanny, Mbosso, Lavalava, Tale, Sallam, Laizer n.k, kwa maana nyingine WCB ni mali ya Mondi so ndo kitega uchumi chake kile.

2. Watu wanamsema Harmonize kwamba ameishiwa, kufikisha views 1m you tube imekuwa mbinde, ambacho hukijui ni kwamba ukiwa Wasafi automatic mashabiki wa Mondi wote ni wa kwako, so wanaokushabikia sio kweli kwamba ni mashabiki wako pekee wapo pia wa Mondi na WCB kiujumla, so unapotoka WCB sasa ndo unaanza kutengeneza mashabiki wako, na automatic mashabiki wa Mondi na WCB watakuwa against wewe, ndo kipindi ambacho anapitia Harmonize, hata hivyo bado anajitahid sana, Kumbuka Mavoko baada ya kutoka kilitokea nini? Itakuwaje siku akiaamua kutoka Lavalava nadhani itabidi akafanye kilimo tu.

3. Diamond platnumz ni mjanja sana na tayari amefikia level ya kutoshuka tena labda aamue tu kuacha mziki na bado atakapoamua kurudi atatikisa tena, ni kama Mzee Yusuph kwenye taarabu, tangu aache taarabu pengo lake linaonekana na mziki wa taarabu unammiss siku atajayeamua kurud ataanzia pale alipoishia kwenda juu kamwe hawezi kuwa chini ya pale.

4. Harmonize, Yes huyu jamaa ndo definition halisi ya kijana mpambanaji, dogo alijipanga muda mrefu sana kufanya kitu chake tangu akiwa ndani ya WCB, pale Wasafi ni kama alikuwa shuleni na ile kupata bahati ya kuwa karibu na Mondi ni kama alipata nafasi ya kuwa karibu na El chapo na huku ukiwa na ndoto ya biashara ya mihadarati, unachokifanya ni kuandaa note book kubwa na kuandika kila kitu, then baadae unajisomea na kufanya utekelezaji

5. Diamond anammiss Harmonize, hakuna msanii kama Harmonize Wasafi, ule ndo ulikuwa usajili bora na nachelea kusema unaweza ndo ukawa usajili bora zaidi kt historia ya Wasafi, Nyimbo alizoimba Mondi na Harmo zimesafiri umbali mrefu sana kuliko collable yoyote east africa, Harmo alimbeba Mondi ndani yake, alipokuwepo Harmo hapakuwa na sababu sana Mondi awepo.

6. Rayvanny, This guy is multi-talented hakuna ubishi juu ya hilo, anaimba, anatunga, anarap, ana vocal kali sana lakin kuna kitu anakosa, Focus... katika miaka hii michache ni kama tayari amemaliza kutoa kila kitu alichokuwa nacho, anaimba muziki ambao ukiusikia utakimbilia kuudownload lakin kesho jioni ndo utakuwa wa kwanza kuufuta, amelimbilia kujijenga kibiashara zaidi kabla ya kujijenga kimuziki.

Hapa ndo Mond anapowin, kabla ya kuubadilisha muziki kuwa biashara na kuleta janja janja zake alianza kwa kufanya muziki kwanza, watu wakapenda muziki wake then alipoanza kuleta ujanja ujanja tayari alikuwa na mashabiki wengi so si rahisi kumkimbia tena, unataka kujua utofauti wa muziki mzuri na muziki biashara kwa mondi simple nenda kasikilize Mbagala, Moyo wangu, Nitarejea, utanipendaga na uje usikilize Baba lao, Jeje n.k. Harmo amelielewa hilo ndo maana kwenye album yake kuna muziki mzuri kwa wingi kuliko muziki biashara, jamaa amepata kitu kwa Mondi, tena sana, Rayvanny akitoka wasafi leo baada ya miezi 6 mtamkuta Tukuyu analima mpunga

7. Lazima ujue WCB kwasasa ni bonge la Platform, mtu yoyote akiwa pale ataonekana na kusikika, unadhan Lavalava ana ukali sana kuliko Jux, Ben pol, Marioo.. lakin dogo anasikika sana eti, Ni Wasafi hiyo inawabeba

8. Mbosso, Yes huyu dogo ana kitu, hataki janja janja yeye anataka kufanya mziki, baada ya miaka mitano huyu dogo tumuangalie mwa jicho la 3 anaweza kufika mbali, japo mziki wake ni kama anatarget sana wanawake lakin ana kitu fulan kipo, na mimi nadhan bado Mbosso ana kitu zaidi tunamdai, hajatupatia bado.. ila kitendo cha kuwa Wasafi ambayo ni biashara ya Mondi anaweza akajikuta anabanwa na kutotoa baadhi ya vitu, lakin Yes mbosso tuendelee kumtazama..

Naomba niishie hapo.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"5.Diamond anammiss Harmonize, hakuna msanii kama Harmonize Wasafi, ule ndo ulikuwa usajili bora na nachelea kusema unaweza ndo ukawa usajili bora zaidi kt historia ya Wasafi, Nyimbo alizoimba Mondi na Harmo zimesafiri umbali mrefu sana kuliko collable yoyote east africa, Harmo alimbeba Mondi ndani yake, alipokuwepo Harmo hapakuwa na sababu sana Mondi awepo."

How Harmo anambebaje?Sawa na kusema Swala anambeba tembo.Alafu ubora unaupima vipi?In term of shows or awards au mauzo kwenye digital platforms au hisia?

"3.Diamond platnumz ni mjanja sana na tayari amefikia level ya kutoshuka tena labda aamue tu kuacha mziki na bado atakapoamua kurudi atatikisa tena, ni kama Mzee Yusuph kwenye taarabu, tangu aache taarabu pengo lake linaonekana na mziki wa taarabu unammiss siku atajayeamua kurud ataanzia pale alipoishia kwenda juu kamwe hawezi kuwa chini ya pale"

Diamond sio mjanja mjanja,yupo juu sababu anajituma na hana tabia zile za wabongo walio wengi kulizika na kufanya kazi kwa mazoea.Pili Diamond ana mentality kama aliyokuwa nayo Cristian Ronaldo au Lebron James,hawa jamaa ukiwatizama wewe unawaona kimafanikio wapo juu,lkn wao wanavyojiona wajiona kama maunderground ndio maana CR na LBJ ni watu wanaitumia mda wao mwingi kufanya mazoezi.

Vitu vinachomfanya Mondi kuwa juu sio ana imba sana kuliko wenzie bali kufanya kazi ,kwa bidii,kutokurizika na kila siku anajiona kama ana anza.

Mwisho hata maji yawe ya moto vipi lazima yataurudia ubaridi wake ,Mondi kushuka atashuka wakati na muda wake ukifika na si kwa ramli hizi za JF zilizoanza tokea 2013.
 
Akifanya Diamond ni biashara alipokuwa akifanya Ruge ni mnyonyaji...
Kweli hapo ndipo utajua kwamba aliyesema binadamu wote ni sawa aliongopa aisee
Diamond anafanya msaada na pia anafanya biashara angalia alipowatoa kina Rayvanny, harmonize alafu angalia walivyo sasa harmo alikuwa mmachinga wa kuuza vitu vidogovidogo hata baisketi alikuwa haiwezi kumiliki huyo Rayvanny alifeli four 4 Hana mbele Wala nyuma mboso ana mwaka 1 na nusu ndani ya WCB teyali amewanunulia wazazi wake nyumba kali lakini pia kawafanya wasanii wake wafanye vizuri international kuliko hata watu Kama benpol, Jux ambao wameanza game kuliko hata Rayvanny.Tukija kwa ruge niambie msanii gani amemsaidia kufika level ya international from scratch?barnaba ni msanii fundi lakini Hana maisha mazuri Wala Hana mafanikio ya mziki.
 
Ruge kupitia THT kawatoa wasanii wengi sana nadhani kuliko mtu yoyote yule walau kawapa kazi ya kufanya. Usiringanishe kawafikisha wangapi international, ila tazama namba ya wasanii ambao wametengenezwa na THT na wanaoishi kwa mziki huu kama njia ya kuingiza kipato?
Kila mtu kafanya yake kwa uwezo wake, Huyu kawatoa wengi wanatamba EAST AFRICA na tanzania huyu kawatoa wachache mnaodai ameafikisha International.
 
Niambie msanii yupi anatamba East Africa wa THT?
 
Niambie msanii yupi anatamba East Africa wa THT?
Wasanii wengi tu wa THT nyimbo zao zinafanya vizuri kenya. Na ukisikiliza nyimbo nyingi hasa za madada zinazopigwa kwenye vituo vingi vya redio ni zao la THT yani watakuwa kapita THT.
Ni vile tu basi alikuwa na damu ya Kunguni ila he did what he did...
Na kumpeleka mtu kimataifa siyo jambo jepesi, salam alikuwa meneja wa Mr Nice hapa aliporudi achana na Mr Nice wa zamani, kuna kipindi Mr Nice alijaribu kurudi akshindwa, hapo hapo Mbosso allikuwa chini ya Saidi Fella lakini alifika wapi.
Nakuonyesha mfano wa mameneja wawili wa Diamond na wasanii wawili waliochini ya Diamond ambao chini ya hao hao mameneja wa Diamond walishindwa wafikisha kokote.
Ravy Vanny alikuwa chini ya Tip Top ambayo Babu Tale alikuwa akiiongoza lakini hakuwa mfikisha popote achilia mbali kumta hata akasikika hapa hapa Tanzania.
 
Mzee baba ebu uache kidogo utani nimekuuliza wataje hao wasanii wa THT wanaofanya vizuri East Africa? Mbona swali rahisi usizungukezunguke
 
Mzee baba ebu uache kidogo utani nimekuuliza wataje hao wasanii wa THT wanaofanya vizuri East Africa? Mbona swali rahisi usizungukezunguke
Wengi tu ukifuatilai mziki unaohit kenya ni watanzania
Kuanzia akina Barnaba
Ruby
J melody
Nandy
the list goes on wote kwa namna moja ama nyingine wamepita THT
Jamaa katoa vipaji vingi sana tatizo ilikuwa kwa hivyo vipaji kujiendeleza vyenyewe.
Na mimi nimekuuliza swali hao mameneja wa diamond mbona hao wasanii kabla ya kujiunga WCB wakiwa chini yao walifail wapi kuwaendeleza?
Halafu Huyo Ray Vany mbona unamwita msanii wa kimataifa wakati maisha yake siyo ya kimataifa au ananyonywa?
Juzi juzi tu katolewa kwenye nyumba aliyokuwa kapanga salasala...
 
nimeandika nikafuta, nikaandika tena nikafuta sasa sijui ndo dalili za corona?? mwenye kujua anisaidie
 
Mi nawaza rayvanny awe anaimba nyimbo za slow , show zake ziwe za kimahaba Zaid ajitengenezee jina la king of romantic upande huo anaweza Sana , usku wa rayvanny safi kabisa ana nyimbo tamu Sana na pia nataman afanye korabo na msanii kama Adelle hvi au Ariana Grand, nyimbo za kubembeleza jamaa anazijua , bas Tu ndo kama hv analoose focus Sana , amepiga nyundo Kali ya ex boyfriend mara anakuja na miss buza sjui korona aah kero somtyme
 
Konde boy hauwezi muziki wa mond .video anazotolea kwa hanscana haziendi mbali tofaututi na alivyaokuwa wcb madarector wakubwa barani Africa aliwajua .akatapa kumsajili hamisi wa bss kashindwa ..mpaka saivi mond kashafanya vyote tuzo kubwa kazileta nchini show nyingi duniani kashafanya.harmonize hata kuwa na jipya la kuwashangaza watanzania
 
Back
Top Bottom